Tabia yangu ya kutojipendekeza, kusujudia maboss na kutokuwa mfitini inanisotesha mtaani

Ny

Safisha nyota tu, yaani badala ya wewe kujipendekeza kwa boss inakua vice-versa boss ndo anajipendekeza kwako.
 
Haa haa[emoji16]
 
Ndiyo maana nikasema kutojipendekeza kumenifanya niendelee kusota mtaani kwani ningejipendekeza bado ningekuwa kwenye Ile ofsi.​
Fikiria mtu anashituka kabisa sijamsalimia boss mda hebu ngoja nikamuone ofsini tuongee mawili matatu, wakati asubuhi kipindi cha kuingia kazini wamesalimiana, Unaenda kuongea nini na boss tena muda wa kazi ambao unatakiwa kushughulika na kazi kwenye ofsi yako.​
 
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji1787]
 
daah kumbe tuko wengi hum...!!hili swala limewahi nikutaa nikaachaachishwa kazii kwa kushitukizwaaa..
kuja kuchunguzaa bos ni mtu wa sifaa na wakupokea vijimaneno na mtu anayetaka ujipendekezee
sasa hivyo vyote mimi sinaa....!!
 
Mimi tabia yangu ya Kutopenda Unafiki, Ujinga, Utoto, Upuuzi, Upumbavu, Kujikomba na Kuongopa imenifanya nichukiwe sana kuliko hata Shetani.
Mm boss ashaniweka kwenye kundi la wajeuri na kila kosa hata wafanye wengine nitatajwa mm kisa simshobokei na cna time nae, ofisini kwake siwezi kwenda kama sna shida ya kiofisi, mm ni kiongozi wa wafanyakazi so alitegemea niimpelekee umbeya na jinsi wanavyomzungumzia, yy ni mtu wa kagera katibu wangu ni muha wa kigoma walitaka kunifanyia mapinduzi waniondoe ili wapange safu yao lakini nguvu ya umma iliwashinda.Usipozaaliwa na tabia za uongo, umbea kujikomba fitina yaani hata uigize yaani huwezi, mtu anapofukuzwa kwa maneno yako ya fitina mshahara wake huwezi kupewa ww, lakini familia yake pamoja na wategemezi wake wote watataibika kwa ajili yako, wengine tuna huruma huwa tunafikiri nje ya box before.
 
Ul
Ughaibuni huko....
 
Nimewahi kuacha kazi sehemu kadhaa kwa huu utopolo wa unafiki na kujipendekeza + umbea.


Yaani Mimi nikishaona sehemu yoyote Kuna hizo tabia najikata that's my basic and primary principle hata siku nikikuta mbinguni Kuna umbea umbea lazima niombe nirudi zangu duniani.
 
Kwel baba kim jong bora urudi kurusha makombora ya nuclear
 
[emoji1787][emoji1787][emoji16][emoji16][emoji16][emoji28][emoji16][emoji1787]

Asee mbavu zangu zinaniuma balaaa

Kosa kubwa usirudie kumkaribisha any staff kuja geto kwako!

Kuna jamaa job hadi alifiwa na mtoto akasema anaumwa anaomba likizo ya 2 weeks! hii yote hataki mazoea na staff wenzie, ( maana anasema yalishamkuta)

Staff ni wachunguzi na kupeleka taarifa kwa mabosi, so usiwaruhusu wakakujua kiviile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…