Tabia yangu ya kutojipendekeza, kusujudia maboss na kutokuwa mfitini inanisotesha mtaani

Tabia yangu ya kutojipendekeza, kusujudia maboss na kutokuwa mfitini inanisotesha mtaani

Ny
Kama kawaida baada ya kumaliza chuo nikaingia mtaani kusota na maisha bahati nzuri nikapata intern kwenye moja ya taasisi za serikali zinazolipa vizuri.​

Changamoto ikawa kumbe kwenye taasisi hizi za serikali inatakiwa ufanye kazi kwa bidii bila kusahau kujipendekeza kwa boss.​
Kwa jinsi nilivyo tabia yangu ya kutopenda kujipendekeza wala kufitini wafanyakazi wenzagu mm nikawa natimiza Majukumu kama kawaida.​

Kumbe ilitakiwa niwe naenda hata kumuona boss personly angalau mara moja kwa wiki kumsalimia tu ambavyo wengine hufanya sasa mm nawaza nikamuone manager nimweleze nini Cha zaidi wakati meeting za Kila wiki tunakutana na kila mtu anawasilisha ripoti yake?.​

Basi bwana boss akaanza kulalamika ooh sina msaada kwenye office ikabidi nifuatilie kujua ninakwama wapi bassi wadau wakanitonya jipendekeze nenda hata mara moja peleka umbea wowote ule atakukubali tu.​

Asikwambie mtu hakuna kazi ngumu Kama kuwa mmbeya eneo la kazi Kama hauna tabia hiyo.​

Mm nikasema potelea mbali ilimradi natimiza Majukumu yangu na nipo qualified siwezi kujipendekeza kwenye ofsi hii nitapata kazi hata kwingine.​

Mkataba wa intern ukaisha boss Kama kawaida akaaniambia nitafute kazi sehemu nyingine.​

Mwamba nikaona siyo kesi nikaingia mtaani nikapata kazi kampuni nyingine ya kibongo aisee kule ndo ikawa balaa bila kuwa mbeya humalizi mwezi unatimuliwa boss anataka kila siku mpishane na wafanyakazi ili apate taarifa mara huyu kapeleka fulani mwizi kaiba mafuta, kifusi.​

Daah nikaona pia isiwe kesi nikaacha kazi.​
Sasa Nina mwaka nasota mtaani nimezunguka kinoma hamna kazi kila Kona patupu wadau wanashauri tafuta hata viongozi wa kisiasa ujipendekeze kazi siku hizi kujuana mm naona wananisumbua tu.​

Natafuta kazi nikiamini qualifications zangu zitanibeba lakini patupu nimeapply sehemu nyingi hata kuitwa hakuna.​

Nikatafuta mpaka sehemu za vibarua patupu. Sasa nawaza hii tabia ya kutojipendekeza nitaachaa vipi maana kubadili tabia ni ngumu kama kubadili ngozi, atakueleza waziwazi jinsi wafanyakazi wenzako wanavyompelekea umbeya kukuhusu ww.​

Safisha nyota tu, yaani badala ya wewe kujipendekeza kwa boss inakua vice-versa boss ndo anajipendekeza kwako.
 
Wanakupa changamoto uwe mjasiliamali na wewe uajiri watu wajipendekeze kwako.

Yani bosi hata ukivaa vibaya mdela haueleweki utasikia unasifiwa tu.
Utasikia "Bosi hii ya leo umeitoa wapi, Dubai au Paris".

Wakati wewe unaona kabisa hapa hamna kitu mtu anajikomba tu.
Haa haa[emoji16]
 
Unajua nimekaa hapa natafakari ya mtoa mada, kwamba kutokujipendekeza kunaweza kuwa sababu ya mtu kukosa kazi, naona kama haliingii akilini, labda kama kuna lingine ambalo mtoa mada anatuficha.

Hakuna anaepinga ya kuwa makazini kuna fitina, ila hakuna watu wanao kubalika makazini kama watu wanao jikubali, wachapa kazi na wasio na tabia ya kuwalamba miguu wakubwa, hili mimi nina ushahidi nalo na mpaka leo kutokana na kujiamini kwangu linanipa ugali, sambamba na kupiga kazi, yaani kazi ya fani yangu ukinipa naipiga mpaka una unafurahi.

Hayo mengine anayo yasema mtoa mada ni sahihi, lakini hili la kujipendekeza kidogo napingana nalo kwa mtindo huo.

Kwa ufupi ajira ni ngumu na upatikanaji wake ni mgumu pia.
Ndiyo maana nikasema kutojipendekeza kumenifanya niendelee kusota mtaani kwani ningejipendekeza bado ningekuwa kwenye Ile ofsi.​
Fikiria mtu anashituka kabisa sijamsalimia boss mda hebu ngoja nikamuone ofsini tuongee mawili matatu, wakati asubuhi kipindi cha kuingia kazini wamesalimiana, Unaenda kuongea nini na boss tena muda wa kazi ambao unatakiwa kushughulika na kazi kwenye ofsi yako.​
 
kwenye kujipendekeza kwa kuchongea wengine siwezi ila kusifia mtu nipo vizuri..nakumbuka nipo chuo nilikosa test moja ya DBMS halafu mwaka wa mwisho...Dokta alikuwa anafundisha soma ilo alikuwa mtata sana ana anajulikana sana kwa sifa ya kushika watu..niliendea nikiwa nimejipanga kweli kweli nalianza kwa kumuita dokta nyingi sana na kumsifia sana kwamba sijapata kuona mwalimu kama yeye tangu nizaliwe nikimuuliza kwanini hakuenda havard kwa siyo level ya nchi hii kabisa....mwisho kabisa nilipewa maksi mbili nikiwa na lengo huwa najipendekeza sana mpaka kieleweke
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji1787]
 
daah kumbe tuko wengi hum...!!hili swala limewahi nikutaa nikaachaachishwa kazii kwa kushitukizwaaa..
kuja kuchunguzaa bos ni mtu wa sifaa na wakupokea vijimaneno na mtu anayetaka ujipendekezee
sasa hivyo vyote mimi sinaa....!!
 
Mimi tabia yangu ya Kutopenda Unafiki, Ujinga, Utoto, Upuuzi, Upumbavu, Kujikomba na Kuongopa imenifanya nichukiwe sana kuliko hata Shetani.
Mm boss ashaniweka kwenye kundi la wajeuri na kila kosa hata wafanye wengine nitatajwa mm kisa simshobokei na cna time nae, ofisini kwake siwezi kwenda kama sna shida ya kiofisi, mm ni kiongozi wa wafanyakazi so alitegemea niimpelekee umbeya na jinsi wanavyomzungumzia, yy ni mtu wa kagera katibu wangu ni muha wa kigoma walitaka kunifanyia mapinduzi waniondoe ili wapange safu yao lakini nguvu ya umma iliwashinda.Usipozaaliwa na tabia za uongo, umbea kujikomba fitina yaani hata uigize yaani huwezi, mtu anapofukuzwa kwa maneno yako ya fitina mshahara wake huwezi kupewa ww, lakini familia yake pamoja na wategemezi wake wote watataibika kwa ajili yako, wengine tuna huruma huwa tunafikiri nje ya box before.
 
Ul
Yule jamaa inawezekana nilimkuta yupo katikati ya stress za madeni.

Jamaa alikuwa eccentric Professor fulani hivi kawa frustrated na maisha, rafiki zake aliosoma nao wote wametoboa maisha, mmoja alikuwa rais Europe. Yeye alikuwa anajiona kalosti.

Mimi nilivyousoma mchezo tu na kuona hapa hamna respect nilijikata zangu.

Tatizo jamaa ni bonge la passive aggressive. Leo kakuzodoa hivyo, kesho anakupa offer vizuri akununulie lunch kama bosi poa tu.

Nikasema hapa hapanifai.

I had the exact opposite problem, ofisi ike ukijipendekeza ndiyo unaleta tatizo, watu hawana muda wa kuendekeza kujipendekeza.
Ughaibuni huko....
 
Nimewahi kuacha kazi sehemu kadhaa kwa huu utopolo wa unafiki na kujipendekeza + umbea.


Yaani Mimi nikishaona sehemu yoyote Kuna hizo tabia najikata that's my basic and primary principle hata siku nikikuta mbinguni Kuna umbea umbea lazima niombe nirudi zangu duniani.
 
Nimewahi kuacha kazi sehemu kadhaa kwa huu utopolo wa unafiki na kujipendekeza + umbea.


Yaani Mimi nikishaona sehemu yoyote Kuna hizo sehemu najikata that's my basic and primary principle hata siku nikikuta mbinguni Kuna umbea umbea lazima niombe nirudi zangu duniani.
Kwel baba kim jong bora urudi kurusha makombora ya nuclear
 
Mimi kuna kasehem nlikuwa nimejishkiza miez 3 tu wamenichongea baada ya kuwakarbisha geto walitaka kufaham nnapokaa nkaona haina shaka, wakakuta chupa kazaa za spirit kwenye cabin "ooh jamaa mlevi, jamaa anapenda madem ana boksi la ndom, jamaa atakuwa mpiga dili, jamaa kazini anapendeza zaid ya boss" nkapigwa chini unemployed and broke

Yan ntanunua Bastola 1day...
[emoji1787][emoji1787][emoji16][emoji16][emoji16][emoji28][emoji16][emoji1787]

Asee mbavu zangu zinaniuma balaaa

Kosa kubwa usirudie kumkaribisha any staff kuja geto kwako!

Kuna jamaa job hadi alifiwa na mtoto akasema anaumwa anaomba likizo ya 2 weeks! hii yote hataki mazoea na staff wenzie, ( maana anasema yalishamkuta)

Staff ni wachunguzi na kupeleka taarifa kwa mabosi, so usiwaruhusu wakakujua kiviile
 
Back
Top Bottom