Tabia za matajiri wa kibongo zinafanana

Tabia za matajiri wa kibongo zinafanana

Hapana, tatizo la masikini wa Tanzania wanadhani ukiwa na pesa basi unatakiwa kuwagawia bure bure, sina pesa lakini nadhani ni busara kusubiri pesa sawia na jasho nimevulia. Ukiogopa wenye pesa katu huwezi pata pesa milele ustabaki kulalama matajiri wa kibongo wana sifa so and soo!

Asante Mkuu Maswitule nawe umeliona.
 
Mi siamini kama bongo kuna matajiri kama wapo ni wachache sana..wengi ni waizi wa waziwazi na madhulumat tu.

Masikini kazi yao kuvuna wasichopanda, kuombaomba tu, wavivu kufikiri na kuchukua hatua, wanamawazo mazuri na wanakufa nayo bila kuyafanyia kazi, wakipata pesa hawajui kuwekeza bali ni watumiaji wazuri, kazi yao kubwa kulalamika tu!!!! Matajiri wako kila mahali usijilinganishe na nchi nyingine au mkoa mwingine kila mahali wapo, ni wale wanaokuzidi kipato na wamejikomboa kutoka kwenye kulia lia.
 
Hapana, tatizo la masikini wa Tanzania wanadhani ukiwa na pesa basi unatakiwa kuwagawia bure bure, sina pesa lakini nadhani ni busara kusubiri pesa sawia na jasho nimevulia. Ukiogopa wenye pesa katu huwezi pata pesa milele ustabaki kulalama matajiri wa kibongo wana sifa so and soo!

Ila bwaan siku hizi ukiwa na vihela vya kubadilishia mboga mtaani watu wanakuita Freemason!! Wabongo bwana,kaazi kwelikweli
 
Masikini kazi yao kuvuna wasichopanda, kuombaomba tu, wavivu kufikiri na kuchukua hatua, wanamawazo mazuri na wanakufa nayo bila kuyafanyia kazi, wakipata pesa hawajui kuwekeza bali ni watumiaji wazuri, kazi yao kubwa kulalamika tu!!!! Matajiri wako kila mahali usijilinganishe na nchi nyingine au mkoa mwingine kila mahali wapo, ni wale wanaokuzidi kipato na wamejikomboa kutoka kwenye kulia lia.
Sijui nikuelewesheje, lakini naona hutonielewa bac naamua kukupuuza maana utanipotezea muda/
 
Usijali nimeshakuelewa unaabudu umasikini. Ila punguza hasira maana utaishia kulalamika kila siku.
 
Lowasa hana hizo tabia ndo maana anatoa sana makanisani ili mumpe urahisi
 
bongo kuna matajiri au vitajiri???mtu akiendesha range sport/vogue basi tayari watu wanamuona tajiri wakati hayo ni magari ya kawaida tu, kwa mtu na kazi yako ukilitaka unatembea hadi garage wanakupa unalilipia kidogo kidogo ...ukilichoka unarudisha unachukua discovery easy....bongo tatizo gari ni issue kubwa haahaaha...unakuta eti mtu anajiona tajiri hata nairobi tu hajakanyaga teehteeh. eti mtu anajiona tajiri kwa kwenda kuwagawia wanamuziki wa ngwasuma elfu kumi kumi x 30 ...ni kama laki 3 tuu hivi hio ni kama dollar 187 ....pesa mbuziii kabisa hio but huyo wenyewe wanamwita pedegee kwikwikwiii....tajiri bhakresa hapo takubali sio hao wajinga wajinga na pesa ya kubadili mboga na kunywa castle lite.
 
Hawa watu balaa, ka mimi nimepigwa danadana na mmoja tokea 21st last month had leo hakijaeleweka.
 
mi nawapenda ili nijue wamefikaje, ukiangalia mema yao utafaidika ukiangalia mabaya yao utaishia kuwachukia
kuanzia tu huwa napenda tabia yao ya kutokuwa na muda wa kufatilia watu bali kazi au vitu, kuwa na kiasi ktk matumizi yao, kuwa na upendo kusaidia wengine lakini zaidi kuwa na kiu ya kuwekeza ili kupata zaidi.
Matajiri wanapaswa kuwa ndio role model wetu ktk kutafuta na sio kuwachukia ingawa sisifii wale wanaopata kwa njia za dhuluma au wizi. Ni mtazamo wangu tu.
 
Ungependa uwe tajiri siku moja? Nahisi unachukia utajiri wewe! Hahahaaaa! Huo ni uchaguzi wako kubaki ulivyo. Kuchukia matajiri ni kuchukia utajiri. Kama unandoto nawe uwe tajiri penda matajiri, penda njia zao utajifunza uwe kama walivyo kisha nawe utatesa. Jambo lolote lile ukishalichukia kamwe haliwezi nalo likakupenda, utazidi kuwa mbali nalo! Kuchukia matajiri ni kuchagua umasikini ni kuchagua mateso duniani.

Dini zimeturoga masikini tuchukie utajiri wakati viongozi wa dini ni matajiri na wanaishi kwenye Kasri, wanafanya watu kuchukia matajiri na utajiri eti wanafundisha kwamba HERI walio MASIKINI duniani maana ufalme wa mbinguni ni wao! Kwamba ni rahisi ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuingia mbinguni! Kwa hiyo Ulaya yote, Marekani na Uarabuni wote watakwenda motoni na sisi masikini waaafrika tuchekelee maana tukifa mbingu ni yetu ata kama mbu wanatuuma leo kwa kushindwa kununua net, tunaharisha kwa kunywa maji machafu, tunashindwa kusomesha watoto kwa kukosa hela, tunashindwa kujitibia, barabara mashimo tu, njaa haiishi pamoja na kwamba tunaishi kando ya mito! Hahaaa matajiri watakiona mbinguni wakati masikini wanapeta!! Tazama na upande wa pili wa matajiri ili uwapende uweze kushiriki vita ya kupigana na dhambi ya umasikini! Hatuwezi kujikwamua iwapo hatutajifunza kitu kwa matajiri maana matajiri wote duniani wanafanya yale yale ambayo masikini hawafanyi kiasi kwamba mataifa mengine ni tajiri na mengine ni masikini! Matajiri wote wananidhamu fulani. Usitazame mabaya ya matajiri tu wanamazuri mengi ikiwamo kutoa ajira, hata masikini wanamabaya yao kwa mfano ni wahalifu sana, hahahahahaaaaa !!
Wengi tunachochanganya ni kudhani kuwa ni mali/fedha za tajjiri ndo zinamfanya tajiri awe na tabia flani. Tunasahau kuwa tajiri ni binadama km yeyote yule na anatabia zake asilia. Ile fedha inachofanya ni kukoleza ile tabia harisi ya mtu huyo tu. Fedha haipandikiza tabia bali fedha inafanya tabia asilia ya mtu kuwa visible zaidi. So ni makosa sana kufkiria matajiri wote wana tabia moja. Wapo matajiri wana roho nzuri sana kuliko majority ya watu maskin.

Unachosema ni kweli, utapochukia matajiri, utajiri uusahau. Ila pia kuchukia matajiri ni kichaka walicho/wanachokitumia maskin kujiplease kwa wao kuwa maskin. Ni kweli kanisa limetudanganya sana katika kutushawish tuwe maskin wakati ukigeuka upande wa pili kanisa hilo hilo linawafagilia sana matajiri.

Nenda leo hii kwenye harambee za kwenye makanisa yetu uone jinsi Baba Askofu anavyotetemeka mwili na mapaja akimuona Tajiri katka harambee na muangalie pia reaction yake akimuona maskin. Pia angalia kwenye maharambee jinsi kanisa linavyowatafuta wenye pesa wawe wageni rasmi. Sijawahi kuona mkristu mwenye imani kali na asiye na pesa kaitwa kuwa mgen rasmi kwenye harambee. Mambo mengine ya kanisa tuyapokee na sisi tujiongeze.
 
Mkuu umeiweka vizuri zaidi nimeipenda sana hadi mwili unasisimka. Kama ilivyo kwa masikini kuna wema na wabaya matajiri nao wapo wema na wabaya, ila matajiri wema ni wengi zaidi maana katika biashara akifanya uharamia ukadhihirika anakimbiwa na wateja na inakuwa mwisho wa utajiri wake. Wakati sisi waafrika tunaamini kuwa huwezi kuwa tajiri bila kufanya kitu mbaya, watu wa nchi zilizoendelea na tajiri wanafundisha watoto wao kuwa kila mtu alizaliwa awe tajiri, kwahiyo umasikini au utajiri inategemea na makuzi na mafundisho uliyoyapata utotoni tu. Kama utotoni kwako kila ulikogeukia walikueleza matajiri na utajiri ni mbaya matokeo yake ndiyo hiyo orodha ya thread hii. Hata kama mtu umeridhika kubaki masikini huna sababu kuchukia tajiri kiasi hiki maana tunategemeana, iko siku na tajiri nae atakuja kuchambua jinsi tabia za masikini wa Bongo zinavyofanana, hahahahaaaa!!! Ninaingoja hiyo siku.
 
Ungependa uwe tajiri siku moja? Nahisi unachukia utajiri wewe! Hahahaaaa! Huo ni uchaguzi wako kubaki ulivyo. Kuchukia matajiri ni kuchukia utajiri. Kama unandoto nawe uwe tajiri penda matajiri, penda njia zao utajifunza uwe kama walivyo kisha nawe utatesa. Jambo lolote lile ukishalichukia kamwe haliwezi nalo likakupenda, utazidi kuwa mbali nalo! Kuchukia matajiri ni kuchagua umasikini ni kuchagua mateso duniani.

Dini zimeturoga masikini tuchukie utajiri wakati viongozi wa dini ni matajiri na wanaishi kwenye Kasri, wanafanya watu kuchukia matajiri na utajiri eti wanafundisha kwamba HERI walio MASIKINI duniani maana ufalme wa mbinguni ni wao! Kwamba ni rahisi ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuingia mbinguni! Kwa hiyo Ulaya yote, Marekani na Uarabuni wote watakwenda motoni na sisi masikini waaafrika tuchekelee maana tukifa mbingu ni yetu ata kama mbu wanatuuma leo kwa kushindwa kununua net, tunaharisha kwa kunywa maji machafu, tunashindwa kusomesha watoto kwa kukosa hela, tunashindwa kujitibia, barabara mashimo tu, njaa haiishi pamoja na kwamba tunaishi kando ya mito! Hahaaa matajiri watakiona mbinguni wakati masikini wanapeta!! Tazama na upande wa pili wa matajiri ili uwapende uweze kushiriki vita ya kupigana na dhambi ya umasikini! Hatuwezi kujikwamua iwapo hatutajifunza kitu kwa matajiri maana matajiri wote duniani wanafanya yale yale ambayo masikini hawafanyi kiasi kwamba mataifa mengine ni tajiri na mengine ni masikini! Matajiri wote wananidhamu fulani. Usitazame mabaya ya matajiri tu wanamazuri mengi ikiwamo kutoa ajira, hata masikini wanamabaya yao kwa mfano ni wahalifu sana, hahahahahaaaaa !!

..Chukua Tano Mkuu. Huko mbinguni Kwenyewe sijui nani aliisharudi akatuhakikishia kuwa Matajiri wanaipata freshi huko!!!!:A S 39:
 
Back
Top Bottom