Ungependa uwe tajiri siku moja? Nahisi unachukia utajiri wewe! Hahahaaaa! Huo ni uchaguzi wako kubaki ulivyo. Kuchukia matajiri ni kuchukia utajiri. Kama unandoto nawe uwe tajiri penda matajiri, penda njia zao utajifunza uwe kama walivyo kisha nawe utatesa. Jambo lolote lile ukishalichukia kamwe haliwezi nalo likakupenda, utazidi kuwa mbali nalo! Kuchukia matajiri ni kuchagua umasikini ni kuchagua mateso duniani.
Dini zimeturoga masikini tuchukie utajiri wakati viongozi wa dini ni matajiri na wanaishi kwenye Kasri, wanafanya watu kuchukia matajiri na utajiri eti wanafundisha kwamba HERI walio MASIKINI duniani maana ufalme wa mbinguni ni wao! Kwamba ni rahisi ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuingia mbinguni! Kwa hiyo Ulaya yote, Marekani na Uarabuni wote watakwenda motoni na sisi masikini waaafrika tuchekelee maana tukifa mbingu ni yetu ata kama mbu wanatuuma leo kwa kushindwa kununua net, tunaharisha kwa kunywa maji machafu, tunashindwa kusomesha watoto kwa kukosa hela, tunashindwa kujitibia, barabara mashimo tu, njaa haiishi pamoja na kwamba tunaishi kando ya mito! Hahaaa matajiri watakiona mbinguni wakati masikini wanapeta!! Tazama na upande wa pili wa matajiri ili uwapende uweze kushiriki vita ya kupigana na dhambi ya umasikini! Hatuwezi kujikwamua iwapo hatutajifunza kitu kwa matajiri maana matajiri wote duniani wanafanya yale yale ambayo masikini hawafanyi kiasi kwamba mataifa mengine ni tajiri na mengine ni masikini! Matajiri wote wananidhamu fulani. Usitazame mabaya ya matajiri tu wanamazuri mengi ikiwamo kutoa ajira, hata masikini wanamabaya yao kwa mfano ni wahalifu sana, hahahahahaaaaa !!