Tabia za wanaume zisizowapendeza wanawake!

Tabia za wanaume zisizowapendeza wanawake!

Heri yake anayaweza,
Mie ndio wa kuringa ili nibembelezwe ati!kwa raha zangu,
Raha ya kuringa niringe mie na mapozi ya kutosha lol!
Nyie ndo wanawake mliopitwa na wakati, siku hizi mwanamke gani anaye ringa, waringieni walio baki usingizini.

Siku hizi kuna wasichana wazuri tena wana adabu zao, wana kazi zao za maana, na wengine wana pesa kuliko huyo mwanaume wanabembeleza kuolewa, mwanaume anaye jiweka down kwa mwanamke inabidi akasomewe dua ili arudishe akili zake.

Sio wanaume wote wanaweza kuwa wanaume, wewe utawaringia wale wanao jidai wanaume mbele za watu lakini sio mwanaume akiwa mbele ya mwanamke.

Kuna wanaume wengi wanatilisha aibu, unakuta janaume tena pandikizi la baba afu linamlilia mwanamke, na mengine yalivyo majinga wanawake wao wanabebwa na wanaume wengine yenyewe yanijidai kama hayaon... hao ndo wanakufaa wewe nadhani mana utawaringia, usije ukakosea step ukaolewa na mwanaume type kama mimi umeumia mana ukifanya hayo unapelekwa kwenu tena kwa nyimbo za kina Ali kiba.
 
Faza Bado hujajisikia ile ya kuwakera kina dada
 
Nyie ndo wanawake mliopitwa na wakati, siku hizi mwanamke gani anaye ringa, waringieni walio baki usingizini.

Siku hizi kuna wasichana wazuri tena wana adabu zao, wana kazi zao za maana, na wengine wana pesa kuliko huyo mwanaume wanabembeleza kuolewa, mwanaume anaye jiweka down kwa mwanamke inabidi akasomewe dua ili arudishe akili zake.

Sio wanaume wote wanaweza kuwa wanaume, wewe utawaringia wale wanao jidai wanaume mbele za watu lakini sio mwanaume akiwa mbele ya mwanamke.

Kuna wanaume wengi wanatilisha aibu, unakuta janaume tena pandikizi la baba afu linamlilia mwanamke, na mengine yalivyo majinga wanawake wao wanabebwa na wanaume wengine yenyewe yanijidai kama hayaon... hao ndo wanakufaa wewe nadhani mana utawaringia, usije ukakosea step ukaolewa na mwanaume type kama mimi umeumia mana ukifanya hayo unapelekwa kwenu tena kwa nyimbo za kina Ali kiba.
Faza unaonekana mshari?
 
Nengenekeni weeee namijtabia hii Mara hle.......kweli amnaga.Hizo zote mbwembwe,zann?.Heshma fut 6.
 
Ngoja nizidadavue hapa chini kama ifuatavyo...............

1. Aina ya kwanza ni ile ya mwanaume ambaye anatatabirika. Wanawake hawapendi wanaume wanaotabirika kwa sababu wanaelewa ni jinsi gani watalipokea jambo lolote linalotokea. Mwanamke anaweza kujua kabisa kwamba, leo atatolewa outing au hapana, ataletewa zawadi au la. Yaani hakuna kitu tunachokiita surprise. Wanawake wanataka kiasi fulani cha kutotabirika toka kwa wanaume. Ndio maana utakuta anaishi au kuolewa na mwanaume jeuri au mwenye roho mbaya . siyo kwamba anampenda kwa jeuri yake, bali kwa kutotabirika kwake.

2.
Aina ya pili ni ile ya mwanaume anayejisikia (mwenye maringo). Huyu kwa kawaida ni mbinafsi sana. Ni jeuri siyo kwa mpenzi wake tu, bali hata kwa mtu yeyote ambaye anamuona yuko chini yake. Kuwaringia watu wengine ni sawa na kumringia mpenzi wako moja kwa moja.

3. Aina ya tatu ni ile ya wanaume jeuri. Mtu jeuri hana aibu! Wakati mwingine anaonesha waziwazi kwamba anamtamani mwanamke mwingine mbele ya mpenzi wake! Anafikia hatua ya kumsimulia mpenzi wake kuhusu marafiki zake wa kike wa zamani na hata u.p.u.u.z.i waliokuwa wakifanya! Kwa ujumla anawadharau wanawake.

4. Aina ya nne ni ile ya mwanaume bahili. Hamnunulii mpenzi wake zawadi hata siku moja! Kila wakati watokapo outing yeye na mpenzi wake huagiza vyakula vya bei rahisi sana pamoja na kwamba, anazo hela. Anataka kumfanya huyo mpenzi wake atishike naye aagize vya bei rahisi. Na wakati wa kulipa anahesabia fedha mfukoni, anatoa fedha utadhani bajeti inabana sana au utadhani yeye na mpenzi wake wamekubaliana “kukaza mikanda.” Mwanaume anaonesha ana mkono wa birika namna hiyo katika siku za kwanza tu za mapenzi! Je huko baadaye itakuwaje? Si atahesabu hata vipande vya nyama jikoni!

5. Aina ya tano ni ile ya mwanaume mbishi. Hata majadiliano ya kawaida tu, yeye anataka kubishana! Anapomtoa outing mwanamke, anakuwa kama amempeleka kwenye mashindano ya mdahalo! Mwanamke hajisikii kuwa huru kutoa maoni au kusema hisia zake, maana atabishiwa.

6.
Aina ya sita ni ya mwanaume asiyekosea. Huyu bwana anapenda sana kuhumu wenzie. Inawezekana hanywi wala havuti sigara, anataka hata wenzie wamuige yeye, wasinywe wala wasivute sigara. Toka siku ya kwanza anayotoka na mwanamke anaanza kumhubiria anayoyataka yeye, siyo asiyoyataka mwanamke. Huyu hataki kabisa mwanamke akawa huru kama yeye, bali angependa yeye amuamulie awe nani na afanye kipi au asifanye kitu gani, ebo! Sasa hapo ni mtu na mpenzi wake au mtu na mtumwa wake!

7. Aina ya saba ni ile ya mwanaume kuwachukia wanawake. Hafichi chuki yake kwa wanawake. Huyu huonesha dhihaka nyingi kwa mpenzi wake na kuwaponda wanawake kwa ujumla wao. Mazungumzo yake yote yatakuwa ni kuwadharau, kuwadhalilisha na kuwanyanyapaa wanawake. Hivi ni mwanamke wa namna gani ambaye atamkubalia mwanaume mpondaji namna hii? Labda mwanamke mwenye mkabala wa kufujwa peke yake au yule mwenye kutaka tu kuchuna buzi na kusepa zake.

Nitaendelea kuwamwagia Tabia za wanaume zisizowapendeza wanawake siku zijazo....

Hello guys!
 
-wanukao sigara kinywani,kuvuta sigara kunaweza kusiwe tatizo lakini kinywa kunuka sigara kama kinu cha kuchambulia tumbaku ni kero kubwa kwa wanawake!chukua hatua
 
-kulewa,kunywa pombe kwa ajili ya kiu na afya haiwezi kuwa kero kwa mkeo ni mpaka pale unapolewa chakari kiasi wakati mwingine huishia kulala kibarazani au sebuleni!jirekebishe unamkera mkeo!
 
-mwanaume kuwa mpole,amini usiamini mkeo haitaji utumie diplomasia kwenye mambo yanayohusu familia yenu hususani mnapohusiana na watu wengine!the more you harshy and manly to other people the more she admires you!fanya kinyume chake utakumbuka maneno haya!
 
-mwanaume mtulivu,kiasili wanaume ni watulivu hivyo wakisikia jambo huwa hawafanyi mambo yao kwa pupa,amini nawaambieni,tunapokuwa watulivu wenzetu hudhani hatujali,tunawakera!akili kichwani mwako sasa!
 
-kuendelea na mambo yetu!mwanaume kumtoa mezani akiwa anasoma magazeti yake,sebuleni akiwa anaangalia taarifa ya habari,au ktk pc,laptop,ipad,au simu anaperuzi jf ni kazi kwelikweli,mkeo anapokuita,au kukuongelesha ukawa unaendelea na mambo yako hapo juu hata kwa sekunde kumi za ziada,umemuumiza na mtihani wa kwanza utakaokutana nao ukimaliza mambo yako umkute kitandani kalala uanze kumgeuzageuza...wee..utalala njaa siku hiyo!
 
-mwisho kabisa fanya makosa yote lakini sio uvivu kwenye lile tendo kwani ndio ndoa yenyewe!all the best ktk kuimarisha ndoa zetu
 
Sipendi mwanaume asiyejua kujistiri nakikwapa,lol..halafu kwenye naniliu anakuwekea kwapa lake puani kabisa lol

heee hahaha lol sa kwann humuogeshi na kumsafisha vizuri kwanza kbla ya......ndo kazi yako mwanamke hiyo!
 
Dah, aina zote mbaya ila mwanaume mbahili ndio staki hata kumsikia. Lol
 
Kuna kabila fulani wanafahamika kwa No. 4, natamani wadada wajihadhari na wa kabila hii. Maana kula, kuumwa, kuoga pia bajeti.
 
Back
Top Bottom