Tabia za Watanzania ambazo hazijulikani zimetokea wapi

Tabia za Watanzania ambazo hazijulikani zimetokea wapi

Heisenberg blue meth

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
1,310
Reaction score
1,633
Hivi kwanini
- Ukitoka safarini lazima ununue mkate?
- Inakuaje mgeni ndio alie kwenye sahani ya udongo?
- Eti mtu akitoka dar lazima aje na machungwa
- Chupa ya chai ikivunjika inakuwa ya kuwekea chumvi, huu si uchawi huu?
- Kuku ikichinjwa lazima mapaja ale baba, na shingo ale aliechinja kuku.
- Shati lililochakaa ndio dekio jipya

Kama kuna vingine ongezea.
 
Siku hizi bado kuna wageni kwenye majumba ya watu,maisha yamebadilika yako utafanya saa ngapi kutwa vijumbani kwa watu kupeleka kunguni
 
Hivi kwanini
- ukitoka safarini lazima ununue mkate?

- inakuaje mgeni ndio alie kwenye sahani ya udongo?

- eti mtu akitoka dar lazima aje na machungwa

- chupa ya chai ikivunjika inakua ya kuwekea chumvi, huu si uchawi huu?

- kuku ikichinjwa lazima mapaja ale baba, na shingo ale aliechinja kuku. .

- shati lililochakaa ndio dekio jipya





Kama kuna vingine ongezea.
Lakini watu mnao ishi vijijini mnashida yote hayo ni mageni kwangu duh "eti ukitoka safarini eti lazima ununue mkati'........ ....wakati kila asbh unapatikana nyumbani
 
IQ ndo tatizo, IQ ndogo inamfanya binadamu ajione mnyonge, tunathamini zaidi wageni klk sisi wenyewe, vyombo vinanunuliwa shauri ya kumfurahisha mgeni na siyo watoto wa familia, Baba anakula nyama nzuri na watoto mabaki baki badala ya baba kujitoa na kuwa mwisho baada ya watoto kushiba yeye ndo anakuwa wa kwanza kula, halafu anajiita kichwa cha familia, wazazi hawali chakula wanachowanunulia watoto wao wanakula nje nyama choma, kwa nini hiyo nyama choma asiwachukulie na familia pia? Huo ni ubinafsi.

Lakini tunaweza kujifunza na kubadilika tukiamua, mambo mengi tunafanya kwa mazoea tulilelewa hivyo tukiona baba zetu wakifanya hivyo na sisi tunafanya, tunaona ni kawaida kwa kuwa kila mtu anafanya.
 
IQ ndo tatizo, IQ ndogo inamfanya binadamu ajione mnyonge, tunathamini zaidi wageni klk sisi wenyewe, vyombo vinanunuliwa shauri ya kumfurahisha mgeni na siyo watoto wa familia, Baba anakula nyama nzuri na watoto mabaki baki badala ya baba kujitoa na kuwa mwisho baada ya watoto kushiba yeye ndo anakuwa wa kwanza kula, halafu anajiita kichwa cha familia, wazazi hawali chakula wanachowanunulia watoto wao wanakula nje nyama choma, kwa nini hiyo nyama choma asiwachukulie na familia pia? Huo ni ubinafsi, ...
Tunashukuru awamu ya 5 kwa juhudi hizi.

TUNATEKELEZA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu huo ulazima umeamua kuongezea tu
Ila nikuambie kitu kwenda ugenini mikono mitupu sio vizuri kwani unaenda kuona watu wa rika tofauti
Kuna wazee na kuna watoto, sasa umepita njiani unaona wanauza nanasi au machungwa ambayo it won’t cost you a leg
Huko kuna watoto hata kununua pipi wafurahi inakuwa mzigo kweli[emoji848]
Siwezi kwenda kwa mtu mikono mitupu Haya nimejifunza kwa wazee na mimi naona ni njia nzuri sana ya kuonyesha upendo

Niko nchi ambayo Ina kila kitu na utajiri mkubwa lakini pindi nikiamua kwenda kusalimia jamaa lazima nipite supermarkets na kununua chochote
Hata kama nimesikia ndugu yangu kapata mtoto lazima ninunue nguo za mtoto
Sio kwamba uwezo hawana la hasha bali ni ukarimu tu mila na desturi
Haina cha mtoto wa mjini wala nini kwani nipo nchi ya wenzetu ambapo hii tabia wanayo pia
Yaani lazima abebe kitu kama anakuja kwako hata mzinga wa champagne [emoji898]
Kwa hiyo endeleza utamaduni huo kwa wanao kwani watajifunza ukarimu na uungwana



Sent from my iPhone using Tapatalk
 
IQ ndo tatizo, IQ ndogo inamfanya binadamu ajione mnyonge, tunathamini zaidi wageni klk sisi wenyewe, vyombo vinanunuliwa shauri ya kumfurahisha mgeni na siyo watoto wa familia, Baba anakula nyama nzuri na watoto mabaki baki badala ya baba kujitoa na kuwa mwisho baada ya watoto kushiba yeye ndo anakuwa wa kwanza kula, halafu anajiita kichwa cha familia, wazazi hawali chakula wanachowanunulia watoto wao wanakula nje nyama choma, kwa nini hiyo nyama choma asiwachukulie na familia pia? Huo ni ubinafsi, ...
Ubinafsi sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dhana nzima ya "Watanzania" kama kitu kimoja ni hadithi ya kutungwa.

Kwa Lowassa unafikiri ni sawa na kwa Mkulima wa Katavi?
 
Dhana nzima ya "Watanzania" kama kitu kimoja ni hadithi ya kutungwa.

Kwa Lowassa unafikiri ni sawa na kwa Mkulima wa Katavi?
Sio kwamba wengi wape? Kwa maana katumia collective meaning.
 
Duuh labda huko kwenu hapa nilipo mkate tunautengeneza wenyewe asubuhi, yani unaamka asubuhi unachukua mahitaji unaweka kwenye kifaa unaendelea kufanya mambo mengine, baada ya dk kadhaa unasikia kimlio tiii tiii tiii unaenda kuchukua mkate wako
 
Back
Top Bottom