Tabia za wenye magari

Tabia za wenye magari

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Mimi jamani sio mwanzilishi wa haya maneno, nime copy na ku paste.....
Zijue tabia za wenye magari:
1. Wenye GX100 na Noah - wanaongoza kwa fujo barabarani, wanapenda kuingizia
watu na gx100 hukimbiza sana gari hata kama wanaenda kusimama mita tano
mbele
2. Wenye gari asili ya teksi, yaani carina T.I na corolla limited - hua wanapenda
kuingia barabarani bila kukadiria mwendo na ukaribu wa gari ambayo tayari ipo
barabarani, utawaona wanakuja huku wanawaza "nimuingizie nisimuingizie" hadi
wanakaribiana na wa barabarani na kuanza kuoneshana ishara za "we vipi?"
3. Wenye vijigari vidogo kama vya kuchezea watoto, yaani Toyota Runx, Raum,
Alex, Allion, Vits, Duet na kile kidaihatsu kama duet - wanakera kishenzi, wakiwa
mbele yako utadhani mbele kuna foleni jinsi wanavyoendesha taratibu, usiombee
wakutane na shimo au bumps, hapo ndipo utakapowaovateki na kugundua kumbe
muda wote huu mlikua barabarani peke yenu, wanaongoza kwa kufanya watu
wachelewe taa
4. Wenye gari asili ya kubebea maiti, yaani caldina, corolla ndefu, ipsum, wish,
gaia, nadia na opa - hua hata hawajielewi wanafanya nini barabarani, wanaweza
kuendesha pasipokua na foleni tu, sijui nani aliwaambia wanunue magari madogo
marefu na barabara hazitoshi
5. Wenye SUV, yaani Rav4, Harrier, x-trail, nissan murano na Toyota Rush - hawa
nadhani hua wanatamani barabarani wawe peke yao, hata kama mbele mnaende
kusimama, akiwa nyuma yako lazima akupigie honi kumaanisha uongeze mwendo,
na usipoongeza atahamia mstari wa pembeni, sijui hua wana maana gani
6. Wenye vigari visivyoeleweka kama ni sedan au hatchback au SUV, yaani fun
cargo, porte, terios, sienta, cube, kei na swift - hawana tofauti sana na wale wa
maiti
7. Wenye gari za kiutu uzima, kuanzia GX110, Mark X, Prado, VX, BMW, Range
Rover, Mercedes na mengine ya kiutu uzima - hawa hawana shida na mtu
barabarani, wanaendana na hali, kama foleni wanatulia, zikitembea wanatembea
8. Wenye magari ya kisistaduu na kibrazameni, yaani IST, verossa, altezza na
brevis, wajuajiiiiii wakati hamna kitu, nawafananisha na wanafunzi wa UDSM na
Mzumbe, wanajiona wanacheza kama CR7 kumbe wanacheza kama Fred (9) Brazil
9. STK na DFP ndo wanajiona wanamiliki nchi
10. Wenye vigari vya ajabu ajabu sijui renault sijui peugeot wanajionaga wapo
sawa na wenye magari ya kiutu uzima ingawa nimewastukia wengi magari yao ni
ya mkopo na usiombee ubahatike kupaona wanapolaza ubavu usiku
 
mmh! aina ya gari yangu na maelezo yaliyopo hapo juu yameniçhosha!
 
Uongo mtupu,Kwani wewe huwa unaendeshea barabara za wapi mkuu
Nadhani utafiti Huu haujazingatia sisi wa mikoani,Kifupi haujakamilika
 
Hahaaaa..... Kwasababu ni copy n paste badi sina comment
 
Namba 10 ni ukweli kabisa.....halafu ni watu wa kukopakopa
 
Mkuu kwani Le Mutuz ana gari gani?

Ana Noah inapiga mziki mnene muda wote.
Kwa ufupi huu utafiti murua nimeuunga mkono kwa 100% na naomba mchango wangu uingie kwenye hansard moja kwa moja.
Makofi kwa kwa kwaaa!
 
Back
Top Bottom