Hili nakubali 100%. Kuna mama nilikuwa naipenda mno kabla sijaishi nae tukapendana sana pia na kuniita pet names mara we HB n.k!
Akapendekeza tuishi wote baadae nikaridhia ni shake well before use. Kuishi nae mwanzo ilikuwa raha mno. Sio mawivu hayo alikuwa nayo akikuta na chat na rafiki yeyote wa kike...Atalalamika mno na ilinipa shida but nilimtuliza nafsi mapenzi yakasonga.
Mawasiliano yalikuwa ni full time kupigiwa kuwa im missed nami nilifanya hivyo pia. Huduma zote napewa bila excuse, mama anafua,anapika tunakula,mtoto usafi wa mwili na mazingira ndio usiseme, game ilikuwa nikitekenya ziwa tu mtoto katepeta.
Mama alikuwa na adabu na msikivu ajabu haskii haambiwi mpaka nikawaza mke wa kuoa si ndio huyu jamani. Alikuwa ananijali hamna mfano kwa hali na very supportive. Haiba ya upole na aibu haikuwa kificho na hakika alijua kukirimu wageni wangu mno. Nikashukuru sana mungu. Kifupi niliinjoy mapenzi awamu ya kwanza.l9
Tulikuwa separate kwa miezi km 6 hivi. Kurudi mambo yakawa tofauti. Mawasiliano yalianza kupungua taratibu. Nikaanza ona rangi zake sasa, licha ya mazuri yote mwanzo mama akaja kuwa mbinafsi ajabu. Anataka umfanyie cares ila ye kwake ni kama ananifanyia favor kunijali.
Yeye ndio akawa anajipa priority zaidi kwa kila jambo. Gubu ndio kila saa yani ikawa kero sasa, kila nifanyalo lazma akandie akawa kama mpinzani wangu na si mpenzi tena.
Sex hakuna tena excuse za ubize na ukipewa ni kama unagonga jiwe. Anaanzisha ugomvi wa kijinga tu usio na maana kila dakika mtoto kiburi kimemjaa na nkimwambia ukweli anadai nalalamika sana...
Mwishowe nkaona isiwe tabu, kama mapenzi ni furaha kwanini nivumilie nikajiengua zangu. Pata picha halisi umeoa mwanamke wa hivyo kwa kurupuka itakuaje??? Kuishi na mwanamke ni muhimu mno kabla hujaoa???