Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Jumla ya maeneo matatu kutoka wilaya ya Uyui, mkoani Tabora yanatarajia kurudia uchaguzi wa serikali za mitaa kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo vifo vya wagombea siku chache kabla ya uchaguzi na mwingine kupigiwa kura nyingi za hapana katika uchanguzi uliofanyika Novemba 27 mwaka huu.
Akizungumza na Jambo TV Mratibu wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa mkoa wa Tabora, Elihuruma Nyera amesema wagombea wawili walifariki, mmoja wa kata ya Ilolanguru, kitongoji cha stesheni kupitia Chama cha ADC na mgombea wa kata ya Igalula, kijiji cha Ipululu mgombea kundi mchanganyiko, huku mgombea pekee wa kata ya Roya kijiji cha Maguriati akipata kura nyingi za hapana.
Aidha, Nyera amebainisha kuwa kutokana na changamoto hizo tayari ameshatoa maelekezo kwa wasimamizi wa uchaguzi kufanya maandalizi ya kurudia chaguzi hizo na kwamba zoezi hilo litafanyika ndani ya siku 40.
Vilevile, Nyera ametoa pole kwa familia ambazo zilipoteza wapendwa wao, huku akitoa wito kwa wananchi wa maeneo hayo kujitokeza katika kukamilisha zoezi hilo ili waweze kupata viongozi watakaowaongoza kwenye maeneo hayo.