Tabora: Mathias Maganga, adaiwa kufia mahabusu ya polisi

Tabora: Mathias Maganga, adaiwa kufia mahabusu ya polisi

Punguza jaziba, ukiwagusa polisi utaguswa zaidi na mtajikuta mmeumizwa
Mimi nashauri tu maana dawa ya ukatili ni ukatili zaidi kwa hiyo polisi wakienda kinyume wasiguswe?kwa taarifa yako hizo zama zimeisha nasisitiza wauze N'gombe wadeal na Ocs liwe fundisho ila usitishe watu kinachotakiwa ni Hela tu mbona huwezi kusikia Ndugu wa Mwigulu au Makamba au mnene yoyote kafia lock up ya polisi?na je ni utaratibu kisheria. Kumuweka mtu mahabusu ya polisi kwa zaidi ya masaa48 acha kuwatishia watu mambo ya kijinga blaza
 
Mkuu wa kituo siyo tatizo. Narudia, mkuu wa kituo siyo tatizo. Tatizo ni sisi wananchi kwa umoja wetu kukubali kuiacha CCM iendelee kututawala. Hili nalo litapita, na siku mbili tatu, mwingine atauawa tena.
Na pia kuweka chama kingine pia sio suluhisho kwani anaetuongoza ni wale wale
 
Na pia kuweka chama kingine pia sio suluhisho kwani anaetuongoza ni wale wale
Watanzania wengi hatutaki kutafakari mambo hivyo tunajikuta tukikata tamaa kila tuna-face challenge za maisha. Sikiliza kwa makini kabisa: Serikali yoyote inapokuwa na hofu ya kuondolewa madarakani, inabidi ifanye mambo yake kwa kufuata matakwa ya wapiga kura. Kwa upande mwingine, isipoona uwezekano wa kuondolewa kwenye uongozi, basi hubweteka na kujisahau, na haitajali wapioga kura wake. Hili ndilo tatizo linalotukabili watanzania. Sisi wananchi inabidi tuondoe hii hali. Tujenga hali ya ushindani. Tusione kama chama fulani ndiyo suluhisho. Suluhisho liwe ni yule anayewajibika kwa wapiga kura wake na siyo vinginevyo.
 
Na Abdallah Amiri – Igunga

Mathias Maganga (31) mkazi wa Kitongoji cha Kinambuga Kijiji cha Majengo, Kata ya Chabutwa, Tarafa ya Simbo Wilaya ya Igunga mkoani Tabora anadaiwa kufia Kituo kidogo cha Polisi Simbo.

Baba wa marehemu, Maganga Hanga (67) akizungumzia kifo cha mwanawe juzi, alisema Usiku wa Septemba Mosi mwaka huu alipokea taarifa kutoka kwa wasamaria wema wakimjulisha kuwa mtoto wake, Mathias Maganga anashikiliwa Kituo cha polisi Simbo.

Alisema kwakuwa ilikuwa usiku hakuweza kwenda muda huo na kulipopambazuka alimtuma mwanawe mkubwa kwenda kituo cha polisi kwa ajili ya kujua sababu za kukamatwa kwa kijana wake.

“Mwanangu mkubwa alipofika Kituo cha Polisi Simbo aliambiwa mdogo wake yupo mahabusu lakini alipoomba kumuona Mkuu wa Kituo hicho aliyefahamika kwa jina la Sajenti Omari alimkatalia bila kuambiwa hata kosa la nduguye.

“Hata hivyo baada ya kuhangaika sana hatiamaye aliruhusiwa kumdhamini ndugu yake kwa masharti

mawili ikiwa ni pamoja na barua kutoka kwenye uongozi anakoishi pamoja na Sh 70,000.”alisema baba mzazi wa marehemu.

Mzee Hanga aliongeza kuwa licha ya kukamilisha taratibu za barua walizoelezwa awali Mkuu huyo wa Kituo cha Simbo aligoma kutoa dhamana.

Alisema ilipofika siku ya tatu, yaani Septemba 3 mwaka huu bila mwanawe kupatiwa dhamana polisi walikusanyika ndugu pamoja na wanakijiji wengine na kwenda kituo hicho cha polisi Simbo kushughulikia suala hilo.

“Hata hivyo mkuu wa kituo aliendelea na msimamo wake wa kutukatalia kumuona kijana wetu wala kutoa dhamana.

“Lakini katika hali ambayo hatukutarajia, tukiwa nje mahabusu mmoja aliyekuwa ndani alichungulia dirishani atatunong’oneza tusiondoke mpaka tujue hatima ya suala hilo kwani mtoto wangu alishafariki tangu jana yake na yumo mule mahabusu.

“Huyo mahabusu aliyekuwa ndani alitwambia kwa kutunong’oneza, jamani mbaneni huyo mkuu wa kituo cha polisi kwani mtoto wenu tunaye humu mahabusu lakini amefariki tangu jana na ndiyo maana mkuu wa kituo anawapiga chenga.

Alisema baada ya kupata siri hiyo ndipo wanafamilia na wananchi walianza kupiga kelele na kupaza sauti wakishinikiza kumuona mtoto wao.

“Tukiwa pale tulisogezwa mbali na kituo na baadaye tulishuhudia gari likiwa hapo kituoni kabla ya kuondoka kwa kasi na kuelekea Kituo cha Afya Simbo kilichopo jirani na eneo hilo.

“Baada ya muda mfupi tuliitwa na mkuu wa kituo hicho cha polisi na kutueleza kuwa mtoto wangu amefariki dunia.”alisema Mzee Hanga.

Taarifa zaidi kutoka kwenye familia ya marehemu zilieleza kuwa mwili wa kijana huyo ulifanyiwa uchunguzi na kubaini kuwa aliuawa kwa kupigwa na kitu chenye ubutu.

Marehemu ameacha watoto wawili, Sabina Mathias (7) na Brighton Mathias (3) mke Furtunata Helman (30) ambaye ni mjamzito.

Kufuatia kifo hicho wazazi wa marehemu wamemuomba Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Camillius Wambura kufuatilia tukio hilo na kutoa fidia kwa familia ya marehemu ambayo imebaki bila kuwa na mtu wa kuitunza.

Mmoja wa wanakijiji wamelaani unyama uliofanywa kupitia kwa mkuu wa kituo cha Simbo hakipaswi kufumbiwa macho, huku wakiziomba taasisi zinazohusika na masuala ya haki jinai kukitupia macho kituo hicho pamoja na wialaya ya Igunga kwa ujumla.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Constatino Mbogambi alithibitisha kufariki kwa kijana huyo na kwamba alifariki akiwa anapatiwa matibabu katika kituo cha afya Simbo.

“Alisema jeshi hilo wanamshikilia mtu mmoja kuhusika na tukio hilo sanjari na kumhamisha mkuu wa kituo hicho kutokana na kulalamikiwa sana na wananchi wa eneo hilo.
Huyo RPC naye achukuliwe hatua eti amefia wakat anapatiwa huduma kituo Cha afya wakat wamemuua ndio wakampeleka huko hospital.

Hawa polisi ni majanga sana aisee huko kwenye vyuo sijui Huwa wanasomea kitu Gani.
 
Wamtafute huyo mkuu wa kituo wamuue kwa nmna yoyote Ile maana hyo kauli ya kuwa alifariiki akifanyiwa matibabu sio ya kweli la msingi wauze N'gombe wadeal nae wamezidi Hawa maku
Hiyo sio kauli ya mkuu wa kituo Bali ni ya RPC
 
Mtu hawezi kufa mahabusu afu akae hata saa zima, wanamtoa mapema mno.
Lengo la familia ni fidia
Wangemtoa vipi na raia wako nje wamejazana na ndio maana wakakaa na kufikiri wakaona watumie mbinu za kihuni kuwatimulia vumbi raia ili wampeleke maiti hospital kabla mambo hayajasambaa.
 
Sema na nyie wanyawezi wasukuma watu wa ajabu sana mnaambiwa ndugu yenu kafariki msiondoke, mnaenda kukaa mbali ya kituo mpaka gari inakuja inaubeba mwili mnatizama tu pumbafu kabisa

Pale ilikuwa ni vita mura tena vita kweriri tata
 
Wangemtoa vipi na raia wako nje wamejazana na ndio maana wakakaa na kufikiri wakaona watumie mbinu za kihuni kuwatimulia vumbi raia ili wampeleke maiti hospital kabla mambo hayajasambaa.
Tatizo lako umekaza fuvu, kwamba raia wanaweza zuia polisi wasimtoe mtu polisi?
 
Yan mtu ameua , adhabu mnayompa ni kumuhamisha KITUO? Lengo ni akaue mwingne huko au?
 
Elezea kisayansi ni kwa namna gani kuwatoa ccm madarakani kutafanya polisi wasiendelee kunyanyasa raia
Mkuu wa kituo siyo tatizo. Narudia, mkuu wa kituo siyo tatizo. Tatizo ni sisi wananchi kwa umoja wetu kukubali kuiacha CCM iendelee kututawala. Hili nalo litapita, na siku mbili tatu, mwingine atauawa tena.
Socrates aliwahi kusema “The heaviest penalty for deciding to engage in politics is to be ruled by someone inferior to yourself”
 
Back
Top Bottom