Tabora: Mwanaume amuua Mke wake na kuhukumiwa miaka minne jela. Hii ni mara ya pili kuua Mke na kuhukumiwa

Tabora: Mwanaume amuua Mke wake na kuhukumiwa miaka minne jela. Hii ni mara ya pili kuua Mke na kuhukumiwa

Hakimu hapo kwenye hukumu aliposema muuaji alikuwa na hasira akampiga mke wake mateke, ngumi, na vipande vya tofali napata shaka.

Hii kitu wanaita "heat of passion" pale unapofanya jambo ghafla, mfano, unamtukana mtu tusi la nguoni then anakufyatua risasi ya kichwa, lakini pale ambapo mtu anapiga mateke, ngumi, na vipande vya tofali huko kwangu ni kukusudia, kwani alikuwa na muda wa kutosha kupoza hasira zake.

Na kutokana na historia ya mshtakiwa kuwa ameshawahi kumuua mke wake wa kwanza, hakimu alitakiwa kutumia hicho kielelezo kama tabia mbaya ya mshtakiwa, anaonesha hakujifunza kwa kosa lake la mwanzo hivyo this time around alistahili adhabu kubwa zaidi.

Wakate rufaa.
 
Siajabu jaji naye huwa na hasira za ghafla so ametumia hisia kutoa hukumu, baada ya miaka mi4, ataua tena kisha hatofungwa kabisaaa, maana looh!
Looh Jamhuri imebwagwa kizembe!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
hamjui sheria za tanzania na wahalifu wanavyocheza nayo..gerezani ni shule ya kupangua makosa labda kingewekwa kipengele cha utashi wa hakimu aau jaji...na ndumba zipo
 
Kweli hata kama kaua bila kukusudia, safari hii angepewa adhabu kubwa kidogo.
Hakimu hapo kwenye hukumu aliposema muuaji alikuwa na hasira akampiga mke wake mateke, ngumi, na vipande vya tofali napata shaka.

Hii kitu wanaita "heat of passion" pale unapofanya jambo ghafla, mfano, unamtukana mtu tusi la nguoni then anakufyatua risasi ya kichwa, lakini pale ambapo mtu anapiga mateke, ngumi, na vipande vya tofali huko kwangu ni kukusudia, kwani alikuwa na muda wa kutosha kupoza hasira zake.

Na kutokana na historia ya mshtakiwa kuwa ameshawahi kumuua mke wake wa kwanza, hakimu alitakiwa kutumia hicho kielelezo kama tabia mbaya ya mshtakiwa, anaonesha hakujifunza kwa kosa lake la mwanzo hivyo this time around alistahili adhabu kubwa zaidi.

Wakate rufaa.
 
Kesi za msingi tunazipuuza na zile kesi za kupuuza ndy tunafunga watu miaka 30 au maisha..

Inji hii hatari sana.
 
Akirudi huyu mwamba lazima tuje tumsome hapa kahukumiwa miaka minne kwa mauaji ya bila kukusudia kwa mke wake wa tatu.

Si hawataki kumfunga na wala hawataki kumfanya aache kuua.....!
 
Aisee hizi sheria sometimes watu wanazipindisha makusudi kbs. Haiwezekani kesi ya kubaka mtu anapigwa nyundo 30, afu kesi ya kuuwa watu wawili mtu anapigwa nyundo nane tena nusu nusu.
 
Kuna Jamaa Mkoa fulani alitoka kulewa pombe akachelewa kurudi nyumbani,alirudi mida ya sa 7 usiku Jamaa akagonga mlango mke yupo ndani tu ametulia kitandani alivunjaa mlango akaingia ndani alimpiga Mke mpaka akaua.baada ya miezi 6 alitoka kwa kuua bila kusudia.
 
Hio ndio tafsiri ya sheria ama kuna mahali sheria inatafsiri vingine tofauti na ilivyo? Miaka minne kesi ya mauaji, Miaka 30 kesi ya ubakaji.
 
Sio bure.

Ako kajamaa ni kachawi kwelikweli yaan ni kachawiiiiiiiiiiii ,kalozi kashetaniiii
 
Leo ndo nmejifunza kwamba ukiua mtu sababu ya hasira ni kuua bila kukusudia, kikubwa tu utumie mateke na vipande vya matofali
Tuna safari ndefu sana kama taifa
 
Namfahamu huyu jaji tangu akiwa wakili sijui kwa nini katoa hukumu hii na alivyo muadilifu
 
Siku akimuua Hakimu bila kukusudia ndipo akili zitawajia hapo mahakamani.
Unaijuwa Tanzania vizuri wewe, utashangaa anaua hakimu kisha anahukumiwa kwenda kupalilia shamba la tumbaku na viboko 10 tu.
 
Back
Top Bottom