Tabora: Nyoka Koboko amekunywa uji wa Moto, amkimbiza Mganga wa Kienyeji

Tabora: Nyoka Koboko amekunywa uji wa Moto, amkimbiza Mganga wa Kienyeji

Kawaida nyoka wa kawaida hagongi zaidi ya Mara moja kwasababu akigongo meno hubakia je huyu kapata wapi uwezo wa kugonga mara nne?
Aisee kwa taarifa yako huyo nyoka aina ya Koboko au "Black Mamba" ana uwezo mkubwa sana wa kushambulia anaweza kugonga kundi la ng'ombe zaidi ya mia kwa kasi ya ajabu na ng'ombe wakafa kwa sumu kali aliyonayo nyoka huyo. Koboko ni habari nyingine Bro.
 
Kuna watu hawajui kitu na niwabishi hatari[emoji23][emoji23][emoji23] eti hakuna nyoka anagonga zaidi ya mara 1! Koboko anagonga zaidi ya mara 50 na kuua juu.
 
Kuna watu hawajui kitu na niwabishi hatari[emoji23][emoji23][emoji23] eti hakuna nyoka anagonga zaidi ya mara 1! Koboko anagonga zaidi ya mara 50 na kuua juu.
Huyo nyoka ni hatari kabisa, nakumbuka nilipokuwa kozi Tabora tulikuwa tukimsikia usiku au asubuhi sana akiwika kama jogoo.
 
Kawaida nyoka wa kawaida hagongi zaidi ya Mara moja kwasababu akigongo meno hubakia je huyu kapata wapi uwezo wa kugonga mara nne?
Mkuu mambo ya meno kubaki alipong'ata iyo ipo kwa nyoka watoto tu, uyu koboko anagonga adi mara 20 na milligrams ya venom ni ileile. Anatenki kubwa sana la sumu kwenye kichwa chake. Meno hayabaki
 
Na haipo chance kwa yote hayo mkuu.

Ukikimbia kumbuka huyu ndo nyoka mwenye speed kuliko wote na ukiinama uokote jiwe unakuta anakumenya utosini huyu wanavyoshauri wanaowajua ukikutana naye jitahidi uende na mood aliyo nayo(ila sijui kama inawezekana),kama akiamua kukaa pembeni bila shari elewa akija kukutisha kama anaku-attack jifanye kama haupo ila ishara yoyote utakayoonyesha kwamba upo against nae hata ukikimbia tu jua ameondoka na uhai wako.

NB:uki-survive shambulio lake hautarudi kama mwanzo lazima utapata utindio wa ubongo,98% wanaong'atwa na huyu mdudu huishia kufa 2% tu ndo huokoka japo wakiwa siyo wa kutegemewa tena kwa kubaki walemavu wa kudumu.
A real devil[emoji48]
 
Mkuu huyu uliyemchambua hapa kamwe humkuti akiishi jirani na makazi ya watu hata iweje

Huyu makazi yake ni milimani huko ukikutana nae njiani basi ujue anahama makazi na mpaka ukutane nae basi ujue hiyo njia inapita kwenye msitu mnene

Sifa yake kuu huyu ubabe ubabe yaani ukikutananae hakimbii na yeye atasimama anakuangalia unataka kufanya nini

Ishu ya kuwika kama anawinda lazima awike, au atalia kama panya

Ukipita msituni au mlimani ambako ndo maeneo anayopendelea kuishi atapiga mruzi ili ujue kuna binadamu mwenzio kumbe ndo anakuita ukijichanganya inakula kwako ukikimbia anaachana na wewe

Huyu ndo nyoka ninayemuogopa mimi

Huyo koboko huwa namalizana nae kwa sime tu maana huyo hajui kujificha huyo akiona unaelekea alipo na yeye anakufata mkutane kati kati sasa nyoka gani huyo hajui kuvizia, anakupa nafasi ya kujiandaa
Huyo nyoka 1998 makongo tunafanya usafi wa kufyeka karibu na hostel za wavulana pale si nikamuona pembeni wakati nimepiga fyekeo Ana kichwa cha jogoo na mweusi daaa niliruka mbio Afande miraji akawa anasema we mtoto wa kiume unakimbia nyoka. Nikamwambia maishani sijawahi ona nyoka kama huyu. Ndo wanfunzi wengine wakajikusanya Mawe mpk. Wakamuua mi niko mita 110,000 mbali
 
Kutokana na kutoonekana mara kwa mara na lifestyle yake mpaka leo hatujui jina lake sahihi
 
Back
Top Bottom