Tabora: Polisi kuanzisha msako wa wanaotaka kujinyonga na kisha kuwapeleka Mahakamani

Tabora: Polisi kuanzisha msako wa wanaotaka kujinyonga na kisha kuwapeleka Mahakamani

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,566
Reaction score
4,013
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Barnabas Mwakalukwa amesema kufuatia kupokea taarifa ya watu wawili kujinyonga, mwaka huu wataanza msako kuwabaini wanaotaka kujinyonga

Amewakanya wanaotegemea kujinyonga kuwa tabia hizo zikome kwani wao wataanza kufanya doria na kuwakamata kabla hawajajinyonga na kisha kuwapeleka Mahakamani

Ameongeza, “Tunaomba viongozi wa Taasisi za Kiroho wafanye doria za Kiroho za kuzima matukio ya namna hiyo kwa kutoa nasaha, elimu na Wataalamu wa Afya waende kwe wagonjwa wenye matatizo ya akili ili wawape faraja kuwa bado wana nafasi ya kuwa na maisha bora.”

Amesema wakati mwingine tunapoteza Wataalamu ambao wangesaidia nchi yetu. Amesema “Tumepoteza Mwalimu, Mjasiriamali labda hawa baada ya miaka miwili wangekuwa Maprofesa au matajiri wa Afrika.”

 
Baada ya kupokea taarifa ya Watu wawili kujinyonga mpaka kupoteza maisha Tabora, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Barnabas Mwakalukwa amesema Polisi wataanza msako wa kuwabaini na kuwakamata wote wanaotarajia kujinyonga mwaka huu na kuwapelekea Mahakamani.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inachekesha lakini inaumiza. Mtu unajinyongaje wakati taifa, familia, ndugu, wazazi wako wanakutegemea?

Hapo unakuta unasomesha watoto na wewe ndio mlipa ada halafu unajinyonga.

Umesoma chuo kwa kutumia mkopo wa serekali halafu unajinyonga.

Unadaiwa na watu, banks, nk halafu unajinyonga hayo madeni alipe nani.

Wewe ni mama wa familia, watoto bado ni wadogo halafu wewe unajinyonga ili walelewe na nani?
 
Kwa hili jambo huhitaji kutumia nguvu. Ukimfunga ndo atajiua kabisa. Watu wa aina hii huwa wanashida ya kisaikolojia. Wanahitaji counseling siyo kuwakamata. Kwanza hawatawapata Coz most of them ni wasiri sana and they don't share to anyone. Hapa wamefeli kabla hawajawapata. Wangewaita wale wenye shida mbalimbali za kisaikolojia wangechukua historia na baadaye wangewasaidia coz matibabu hospitalini yanatolewa bure Influenza,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Paula Paul,
mkuu unaweza shangaa ila hayajakufika aseeh, pale unajifikiria wewe tu sijui taifa, mtoto, baba, mama unaona hawana maana
 
Hahahaaah hii ya kufungulia mwaka.
Watajuaje kama mtu anataka kujinyonga??
 
mkuu unaweza shangaa ila hayajakufika aseeh, pale unajifikiria wewe tu sijui taifa, mtoto, baba, mama unaona hawana maana
Unajua kuna watu roho zao ni ndogo, mtu kaachwa na boyfriend au girlfriend yeye anakimbilia kujinyonga.
Kafeli mtihani anakimbilia kujinyonga.
Kwa kweli napitiaga mengi magumu ila kujinyonga au kujiua halijawahi kuja kwenye akili.
 
Msako mkali jaman mambo ni meng muda ni mchache
 
Polisi wa Bongo wanauwezo mkubwa sana. Mpaka anayetaka kujinyonga wanaweza kumdaka kwa patrols zao.
Kumbe ndio maana hawadeal na mambo madogomadogo kama ya watekaji n.k
 
Inachekesha lakini inaumiza. Mtu unajinyongaje wakati taifa, familia, ndugu, wazazi wako wanakutegemea?

Hapo unakuta unasomesha watoto na wewe ndio mlipa ada halafu unajinyonga.

Umesoma chuo kwa kutumia mkopo wa serekali halafu unajinyonga.

Unadaiwa na watu, banks, nk halafu unajinyonga hayo madeni alipe nani.

Wewe ni mama wa familia, watoto bado ni wadogo halafu wewe unajinyonga ili walelewe na nani?
Mkuu hayo ni matatizo ya kisaikolojia ni kama ugonjwa tu nao pia unahitaji tiba. Mtu anaye jiondoa uhai sio kwamba aliamka tu akifikiria kujiua ni kitu alichokuwa akijiambia mda mrefu kwa hiyo ikitokea sababu tu ni dk sifuri anajitundika bila kuwaza yote hayo.
 
Back
Top Bottom