Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paulo Chacha, amemwagiza Katibu Tawala wa Mkoa kumsimamisha kazi Meneja wa Wakala wa Huduma za Ununuzi Serikalini (GPSA) Mkoa wa Tabora, Mayala Mburi, kutokana na tuhuma za kumtukana matusi wateja waliokwenda kupata huduma za mafuta, akiwemo mtumishi kutoka ofisi ya Waziri Mkuu.
Maagizo hayo aliyatolea wakati alipotembelea ofisi za GPSA mkoani Tabora Jumanne, akiwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa.
RC Chacha alisema kuwa Meneja huyo alikubaliana kuwahudumia watumishi hao wa Waziri Mkuu kwa kuwapatia mafuta, lakini alivyowapokea usiku aliwatukana
Baada ya kudaiwa kutukanwa, watumishi hao walimpigia simu RC Chacha ambaye alimpigia simu meneja huyo. RC naye akatunwa matusi ya nguoni na meneja huyo.
Kwa upande wake Meneja wa GPSA mkoa wa Tabora, Mayala Mburi, akijibu tuhuma hizo ameeleza kilichomsibu mpaka kusababisha kutoa lugha za matusi kwa Mkuu wa Mkoa pamoja na wateja waliofika kituoni kupata huduma ya mafuta .
Katika hatua nyingine, RC Chacha ameagiza kusimamishwa kazi kwa watumishi wawili wa TANROADS Mkoa wa Tabora, Meshack Deogratius na Godfrey Gration, kwa tuhuma za kupokea rushwa kutoka kwa dereva wa gari lililozidisha uzito katika kituo cha kupima uzito cha Turi kilichopo mkoani Tabora.