Tabora: RC Paulo Chacha amsimamisha kazi Meneja GPSA kwa kutukana wateja

Wakuu,

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paulo Chacha, amemwagiza Katibu Tawala wa Mkoa kumsimamisha kazi Meneja wa Wakala wa Huduma za Ununuzi Serikalini (GPSA) Mkoa wa Tabora, Mayala Mburi, kutokana na tuhuma za kumtukana matusi wateja waliokwenda kupata huduma za mafuta, akiwemo mtumishi kutoka ofisi ya Waziri Mkuu.

Maagizo hayo aliyatolea wakati alipotembelea ofisi za GPSA mkoani Tabora Jumanne, akiwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa.

RC Chacha alisema kuwa Meneja huyo alikubaliana kuwahudumia watumishi hao wa Waziri Mkuu kwa kuwapatia mafuta, lakini alivyowapokea usiku aliwatukana

Baada ya kudaiwa kutukanwa, watumishi hao walimpigia simu RC Chacha ambaye alimpigia simu meneja huyo. RC naye akatunwa matusi ya nguoni na meneja huyo.

Kwa upande wake Meneja wa GPSA mkoa wa Tabora, Mayala Mburi, akijibu tuhuma hizo ameeleza kilichomsibu mpaka kusababisha kutoa lugha za matusi kwa Mkuu wa Mkoa pamoja na wateja waliofika kituoni kupata huduma ya mafuta .

Katika hatua nyingine, RC Chacha ameagiza kusimamishwa kazi kwa watumishi wawili wa TANROADS Mkoa wa Tabora, Meshack Deogratius na Godfrey Gration, kwa tuhuma za kupokea rushwa kutoka kwa dereva wa gari lililozidisha uzito katika kituo cha kupima uzito cha Turi kilichopo mkoani Tabora.

Asamehewe tu maana Watumishi wa uma karibia wote hawana nidhamu kwa wananchi
 
Karukwaa mtu hapooo
 
Siamini kama ni kweli, inahitajika tume huru, hawa wakuu wa mikoa wakinyimwa mafuta ya dili huwa wanageuka na kuanza kutumia madaraka yao vibaya, kama alimtukana kwanini hakumpeleka polisi?
 
kwa bahati mbaya sana, pombe imegarimu wengi, haijawahi kumwacha mtu salama. ona sasa hapo amemtukana mkuu wa mkoa kuwa akome kumpigia akiwa kwenye starehe, kama alivyokoma kunyonya ziwa la mama yake.
Alimrekodi? sina hakika kama ni kweli japo hata simjui huyo Meneja hapa kuna hitaji tume huru
 
Taratibu za utumishi wa umma zinasemaje mtumishi anapokuwa amemaliza muda wa kazi kwa siku?tukumbuke hayo matusi hakuyatoa mchana muda wa kazi though siujui mkataba wake unasemaje.

Kwa sababu simu amepigiwa (na mkuu wa mkoa anakiri) saa tano usiku na huo ni muda kila mtu anafanya yake anayoyajua,kutukana watu kweli ni kosa haipendezi silitetei hilo but waangalie na mazingira yenyewe tukio lilipotokea.
Na sidhani kama ni kweli kamtukana, itakuwa walipishana dili
 
Kosa Moja halimfukuzishi mke. Cha msingi na muhimu ni taratibu za kiutumishi zifuatwe na asionewe mtu.
 
kwa bahati mbaya sana, pombe imegarimu wengi, haijawahi kumwacha mtu salama. ona sasa hapo amemtukana mkuu wa mkoa kuwa akome kumpigia akiwa kwenye starehe, kama alivyokoma kunyonya ziwa la mama yake.
Sawa amemwambia hivyo lakini umezingatia ilikuwa saa ngapi?

Angekuwa amemjibu hivyo 08:30 AM to 16:00 AM ule muda angetakiwa awajibike ofisini then ingekuwa kesi lakini mtu mchana kutwa amewajibika kuitumikia ofisi yako saa tano usiku mtu amepumzika na mkewe unampigia wa kazi gani?
 
Hawa viongozi wa kisiasa wana shida mingi sana.
 
Taratibu za utumishi wa umma zinasemaje mtumishi anapokuwa amemaliza muda wa kazi kwa siku?tukumbuke hayo matusi hakuyatoa mchana muda wa kazi though siujui mkataba wake unasemaje ila kisheria mkuu wa mkoa ndiye ameingilia uhuru wa jamaa.

Kwa sababu simu amepigiwa (na mkuu wa mkoa anakiri) saa tano usiku na huo ni muda kila mtu anafanya yake anayoyajua,kutukana watu kweli ni kosa haipendezi silitetei hilo but waangalie na mazingira yenyewe tukio lilipotokea.
Manager ndio mtu wa kwanza katika Ofisi ivo anatakiwa Kuwa responsible muda wowote ule atakapohitajika, Ndio image ya Ofisi ndio mana unakuta analipwa mpaka incentives ambazo wengine hawalipwi tafsri yake ni Kuwa being a Manager is the full time job
 
Wakuu,

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paulo Chacha, amemwagiza Katibu Tawala wa Mkoa kumsimamisha kazi Meneja wa Wakala wa Huduma za Ununuzi Serikalini (GPSA) Mkoa wa Tabora, Mayala Mburi, kutokana na tuhuma za kumtukana matusi wateja waliokwenda kupata huduma za mafuta, akiwemo mtumishi kutoka ofisi ya Waziri Mkuu.

Maagizo hayo aliyatolea wakati alipotembelea ofisi za GPSA mkoani Tabora Jumanne, akiwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa.

RC Chacha alisema kuwa Meneja huyo alikubaliana kuwahudumia watumishi hao wa Waziri Mkuu kwa kuwapatia mafuta, lakini alivyowapokea usiku aliwatukana

Baada ya kudaiwa kutukanwa, watumishi hao walimpigia simu RC Chacha ambaye alimpigia simu meneja huyo. RC naye akatunwa matusi ya nguoni na meneja huyo.

Kwa upande wake Meneja wa GPSA mkoa wa Tabora, Mayala Mburi, akijibu tuhuma hizo ameeleza kilichomsibu mpaka kusababisha kutoa lugha za matusi kwa Mkuu wa Mkoa pamoja na wateja waliofika kituoni kupata huduma ya mafuta .

Katika hatua nyingine, RC Chacha ameagiza kusimamishwa kazi kwa watumishi wawili wa TANROADS Mkoa wa Tabora, Meshack Deogratius na Godfrey Gration, kwa tuhuma za kupokea rushwa kutoka kwa dereva wa gari lililozidisha uzito katika kituo cha kupima uzito cha Turi kilichopo mkoani Tabora.

Walevi tukamtete mwamba jamani mwenzetu karikorogaa huko...
Pombe sio chai jamani..
 
Watu wanajua kuroga jamani...huyo jamaa aliyemfanyia mwenzake hivyo Mungu anamuona
 
Sema Mkuu wa Mkoa ana deka sana tumatusi huto tu ndo ana maindi? Wananchi wanatukanwa kila siku na bado hawaachi kutaka huduma za hao wakoo.
 
hajalewa muda wa kazi,na hakuwa eneo la kazi kwa muda huo, na huo muda walio mtafuta haukuwa muda wa kazi full stop. Alisikika mwanasheria mmoja kutoka kibosho.
Kamishna Mkuu wa TRA alipigiwa Simu na shujaa Magufuli saa 8 usiku hakupokea

Alipoamka Asubuhi akakuta Msigwa ameshatangaza Utumbuzi 😀😀
 
Ukisikia ule msemo wa "pombe siyo chai" ndiyo umetembea sasa na jamaa yetu Mayala Mburi! Kutoka kuwa Boss mpaka kwenda kushinda ukisoma tu magazeti kwenye ofisi ya RAS! Siyo kazi nyepesi hata kidogo.
 
Back
Top Bottom