Tabora: Sakata la Kanisa lililojengwa kuziba barabara na kupiga muziki saa 24 kumbe ni genge la wahuni ( 5 )

Hakuna mgambo hapo wa kumkamata? mpelekeni polisi
Kuna delaying techniques zinafanya hapa, nafikiri mlungula unahusika, bado sisi wakazi wa hapa ni waungwana sana ila tumechoka ndio maana tunaweka hapa mtandaoni na wakubwa wajue kinachoendelea.
 

Hapa barabara imezibwa inayoenda Westland primary school .
 
Viongozi wa mkoa wa Tabora hebu kuweni wastaarabu hivi mnakaa ofisini kabisaaa confortable huku Kuna sintofahamu , Tena isiyo na sababu , watu kibali cha ujenzi hawana , usajili wa kanisa hawana , kibali cha kuendesha kanisa hawana , wanasumbua raia nyinyi mpo kweli ? Ndio kasi ya awamu ya tano hii ? Mbona hili suala liko wazi shule zikifelisha mtaanza kujiuliza sababu ? Hamjui kutoka hapo kwenda shule ya Msingi Itetemia na shule ya Westland haizidi mita mia ? Hamjui kwamba Westland primary school ni shule ya bweni ? Ratiba za bweni hamzijui za kujisomea prepo ? Hamjui kuwa raia hapo mtaani kuna wagonjwa , wazee , watoto wanaathirika na muziki mkubwa hata madaktari wanasema hayo ? Huyo mchungaji Jackson ana mfuko mpana kiasi gani kuwatia wote mfukoni ? Au ndio mpaka waziri wa ardhi aende ?
 
Tabora ilikuwa ya aggrey mwanri Ilitakiwa hata ubunge agombee tabora, huyu aliyopo akafundishe chuo
 
Mimi hapa naishi Chini ya spika ya msikiti nimeshalalamika sana nimeambiwa hama
 
Cheyo Mwanga Shop hili kanisa lilifukuzwa na kuondolewa kwa sababu ipi ? Kama sio huuhuu ujinga unaofanyika hapa .
Halafu pale cheyo maneno yalikuwa mengi na pia kuna waliosema pia halikustahili kuwepo kwa sababu ya makazi ya watu sasa makanisa huwa yanatakiwa yawe wapi ? kwenye mbuga za wanyama
 
Halafu pale cheyo maneno yalikuwa mengi na pia kuna waliosema pia halikustahili kuwepo kwa sababu ya makazi ya watu sasa makanisa huwa yanatakiwa yawe wapi ? kwenye mbuga za wanyama
Utaratibu wa manispaa upo , maeneo husika yapo ni suala la kufuata sheria na utaratibu . Wewe unafikiri kwanini walifukuzwa Cheyo Mwanga Shop ?
 
Hakuna conflict of interest ndugu , uko mbali hauijui adha tunayopata sisi wagonjwa wa moyo wenye wagonjwa , wazee , watoto , wanafunzi na watu wengine, yaani tuumie kwa ajili ya wajinga wachache ?
Heri hata hao ni kanisa. Kinachoendelea Rock City Mall Mwanza kinasikitisha maana kuna live band inayokesha takriban kila siku. Hakuna anayejali makelele yanayopigwa ama kubadilishwa matumizi ya maegesho ya magari katika mall hiyo kuwa eneo la kupigia dansi na madada poa kujivinjari!!! Yawezekana wapo wenye maslahi na huu "uvunjaji wa sheria za mazingira" Tunakoelekea makelele itakuwa ni kitu cha kawaida.
 
Mara nyingi hiyo ni miradi ya watu binafsi. Hawana la maana na sababu ya kupiga mayowe mitaani. Siku hizi sitaki hata kuwasikia na mabakuli yao ya kuomba msaada wa ujenzi wa makanisa maana hawana sababu ya kutojiunga na wengine zaidi utafutaji na ubinafsi tu.
 
Hilo kanisa liachwe ili litoe huduma za kiroho katika mji uliojaa ushirikina
 
Kifupi ni kwamba kujiita kanisa Ni ngao ya kujifichia hili Ni genge la wahuni wajasilia dini ambao dini hawaijui , Biblia hawaijui , kuhubiri hawajui kazi kelele tu zisizo na maana .
 
Mkuu ni kundi la wahuni wajasilia dini ambao ni watoto watoto tu hata akili hawana .
 
Hilo kanisa liachwe ili litoe huduma za kiroho katika mji uliojaa ushirikina
Komenti yako hii na uliyokomenti Jana imenishangaza Sana responsible member wa jf Kama wewe kukomenti illogical points ni ajabu . Sasa hapa Tabora unavgosema Kuna ushirikina uko wapi uje utuonyeshe ? Hao unawaona wachungaji uchwara asilimia 99% wanatumia nguvu za giza na ushahidi upo .
 
Nimeishi Tabora na Sikonge nimerogwa sana na hao Waswahili wapinga Kristo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…