Tabora: Wahamiaji haramu 32 wakamatwa wakitokea Kigoma na wana vitambulisho vya kupigia kura

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Wahamiaji haramu 32 raia wa Burundi wamekamatwa Mkoani Tabora wakitokea Mkoa wa Kigoma kuelekea Mikoa ya DSM na Mbeya katika upekuzi watatu wamekutwa na vitambulishio vya kupigia kura vya Tanzania na sita wakiwa na barua za utambulisho kutoka kwa Watendaji wa Kata za Mkoa wa Kigoma na DSM.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Afisa Uhamiaji Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Amiru Sadick Salim amesema Wahamiaji 25 kati yao wamekamatwa Wilayani Urambo wakiwa ndani ya treni kutoka Kigoma kwenda DSM huku wengine saba kituo kikuu cha mabasi Tabora wakitoka Kigoma kuelekea Mbeya.

Screenshot-2020-10-07-at-10.16.40-660x400.png
 
View attachment 1592829
Lissu ameanza kuandaa Timu yake ya Vurugu baada ya kushindwa. Mwaka huu ataogea barafu, yeye na vibaraka wake. JPM tano tena.
 
Bongo raha sana hahaha inaonekana alie wapa ivo vitambulisho kacheza uku na kule kawaingiza mjini
 
hao ni ndugu zake Magufuli wamekuja kupiga kura
Ndugu zake Magufuli wamekamatwa na police wa chadema😁😁😁😁😁
Nyie watu mnajichanganya hadi mnachanganyikiwa😂😂😂😂😂😂😂
 
ni kwamba kikosi wamejichanganya wataachiwa tu kwa order toka juu
 
Kumekuchaaaaa😀 wawaachie wanakuja kuona Flyover na mandege..ni wapiga kura wetu hao.

Everyday is Saturday.............................😎
 
hua wanatumia mbinu gani kuwakamata ili nisije nikakamatwa na mimi ?
 
Bongo raha sana hahaha inaonekana alie wapa ivo vitambulisho kacheza uku na kule kawaingiza mjini
wakati wa kujiandikisha hawana maswali mengi unachosema ndio wanaandika wao hawanaga mambo mengi.

kama wanaweza waka_fake NIDA waone kama watatoboa
 
Hao ndo wamekuja kukata watu mapanga ndio tabia za kule kukata watu mapanga
 
Hao wapo wengi Sana... Huku mtaani ht hivi vitambulisho vya uraia vikihakikiwa wengine watakuwa wahaamiaji Haram...
 
Back
Top Bottom