Tabora: Wahamiaji haramu 32 wakamatwa wakitokea Kigoma na wana vitambulisho vya kupigia kura

Tabora: Wahamiaji haramu 32 wakamatwa wakitokea Kigoma na wana vitambulisho vya kupigia kura

Waandishi waifuatilie vizuri hii ishu. Wamekutwa na vitambulisho wa kupiga kura, na baadhi wana barua za utambulisho, tuanzie hapo; walivipata kupitia mitaa au vijiji gani, ili viongozi wa serikali za mitaa wasio waaminifu waadhibishwe kisheria.
 
CHADEMA kuweni makini na hawa wanaongia nchini huko boda mwezi huu... Yataingizwa mengi..
Jiwe linajua lishafeli..
Wahamiaji haramu 32 raia wa Burundi wamekamatwa Mkoani Tabora wakitokea Mkoa wa Kigoma kuelekea Mikoa ya DSM na Mbeya katika upekuzi watatu wamekutwa na vitambulishio vya kupigia kura vya Tanzania na sita wakiwa na barua za utambulisho kutoka kwa Watendaji wa Kata za Mkoa wa Kigoma na DSM.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Afisa Uhamiaji Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Amiru Sadick Salim amesema Wahamiaji 25 kati yao wamekamatwa Wilayani Urambo wakiwa ndani ya treni kutoka Kigoma kwenda DSM huku wengine saba kituo kikuu cha mabasi Tabora wakitoka Kigoma kuelekea Mbeya.

View attachment 1592829
 
Lissu ameanza kuandaa Timu yake ya Vurugu baada ya kushindwa. Mwaka huu ataogea barafu, yeye na vibaraka wake. JPM tano tena.
Lissu na wakimbizi,sio kibaraka was mtu Mimi ila hapo umeongozwa na mihemko.punguza jazba utapasuka ,mkuu
 
Hawa wamejaa mikoa ya kanda ya ziwa kama vibarua kwenye mashamba hasa Rukwa,Tabora(mashamba ya tumbaku),Geita,Kigoma wilaya zote,Mwanza,Kagera(Biharumulo).
Hii mipaka aliyetuweka Beberu ilitugawa sana.
 
Usalama wa taifa hakuna wanachofanya takataka kabisa. Raia wa nchi jirani wanapataje access ya vitambulisho vya kura.
 
Back
Top Bottom