Tabora: Wanafunzi wa kidato cha 6 waliotaka kuchoma moto Shule ya Sekondari Milambo wakamatwa

Sidhani kama ni mkali.
Ila ukiangalia hapo kila mda linapotokea suala kama hili katika hii miaka mi5 sababu ni kuahirishwa kwa mahafali.
Swali ni je kuna nini nyuma ya mahafali kwa wanafunzi na
Taarifa za chini kwa chini Hueleza kwamba siku ya mahafali vijana huwa na lengo la kufanya fujo. Hivyo ili kuzuia Hali hiyo mapema shule huahirisha mahafali hayo. Kitu kinachopelekea resistance zaidi juu ya kutokufanyika kwa sherehe hizo.
Nb.
Enzi zangu shule yetu iliahirisha sherehe kama hii. Huwa nalaani mpaka Leo coz nilipanga kumleta manzi angu nijisifie kwa wana
 
Huyo atakuwa ni mtoto wa mwalimu, nesi ama askari aliyeiga mambo makubwa asiyoyaweza.

Watoto wa Feza Og huwa wanaenda mamtoni kusoma na wakitoka huko wanafikia ajira za wizarani moja kwa moja ama wanakabidhiwa makampuni na wazazi wao.
Jesuu naomba connection ya mchongo mkuu .......
 
Duniani kote kuna vibe flani la kumaliza shule wanafunzi huwa wanakuwa nalo ni kawaida sana mambo hayo na hakuna hususiano sana na life style yao
 
Chamber niliingiaga mara moja skumbuki ishu ilkua ni nn lakini sikupewa heka heka sana jamaa alkua kiongozi wao, wakat tuko chuo nikaskia jamaa alikufaga kiajabu ajabu tu.....ile shule poa sana sema lile baridii aseee🥶🥶
 
Chamber niliingiaga mara moja skumbuki ishu ilkua ni nn lakini sikupewa heka heka sana jamaa alkua kiongozi wao, wakat tuko chuo nikaskia jamaa alikufaga kiajabu ajabu tu.....ile shule poa sana sema lile baridii aseee🥶🥶
Mkuu pale njoss acha kabisa sasa imagine na ile bard alafu ndo upo.five unaambiwa umepangiwa zamu kufanya usafi nyamagana aaaaah utakubali sana
 
Hiyo shule kwa waliosoma pale kuanzia mwaka 2005 kushuka chini wanaijua vizuri
Yaani hiyo shule ilikua na historia kila baada ya miaka miwili au mitatu inatokea vurugu kubwa
Mimi nimesoma form one mpaka form four
Wakati tunaingia form one mwaka 2002 tulikuta wanafunzi waliotutangulia wamefanya vurugu na uharibifu mkubwa na kuna waliofukuzwa shule waliorudishwa walikua wanalipa faini ya uharibifu
Wakati tuko pale kulitokea vurugu kubwa wanafunzi wa milambo (wasiojulikana) walivamia Tabora Girls na kuwapiga na kuwajeruhi vibaya
Muda huo huo wanafunzi wanavamia mkuu wa shule anapiga simu polisi kwamba wanafunzi wa milambo wametuvamia zinatoka Difenda mbili moja inawahi milambo na nyingine inafuatila njia ya Tabora Girls
Cha ajabu hakuna mwanafunzi hata mmoja aliefanikiwa kukamatwa usiku huo
Hii shule ilikua inaogopwa mkoa mzima na shule zote
 
Athari za kupitisha mifailure....
Yote hiyo imevushwa form four..

Upumbavu ..
 
Utaratibu mzuri :Mahafali zifanyike kabla kuanza mitihani.

Mwanafunzi akiwa katika kipindi cha mitihani hawawezi kufanya ujinga huo,isotoshe baada ya mitihani kila mwanafunzi angetamani kwenda kwao.

Kuna tatizo mahali kati ya Shule na Viongozi wanaozisimamia shule.(Eti walikataza mahafali,kwa miaka mingine walikuwa wanafanyaje?!)
 
Watoto genye zinawazidi warudishiwe utaratibu wao wa zamani graduation kama hivi wana pelekwa Tabora girls kwa wenzao wanacheza mziki wanajiiba kisaikolojia genye zinapungua
 
Mimi nakumbuka nilikataa sherrehe yangu ya kidini maana nilikuwa muhitimu peke yangu....madogo walikasilika sana eti nimewazuia kuchangia michango na sherrehe kutokuwepo😄😄. Nikawaonea huruma ila walinilaumu sana...hili tukio limenikumbusha nikacheka sana
 
Utapeli wa waalimu,mtu mnawachangisha mahafali hamfanyi na pesa kuwarudishia mnakataa. Shule nyingi wanafanya mahafali kabla ya mitihani. Waalimu punguzeni njaa na janja janja za ovyo
 
Mkuu pale njoss acha kabisa sasa imagine na ile bard alafu ndo upo.five unaambiwa umepangiwa zamu kufanya usafi nyamagana aaaaah utakubali sana
Sisi kubeba magogo(kuni), mnayatoa chini msituni kule mnaleta juu huku jikoni....usibebe utamjua mbedule ni nani
 
Kipindi hicho Milambo ilikuwa ni ngumu mkononi damu zilimwagika sana kipindi hicho, madogo waachane na hayo mambo ni usela mavi. Tumeona mengi sana miaka hiyo.
 
Sisi kubeba magogo(kuni), mnayatoa chini msituni kule mnaleta juu huku jikoni....usibebe utamjua mbedule ni nani
Mkuu kipindi cha mwishoni walianza adhabu zao za kishamba et tunabeba molam aiseee huyo alikua BAMBA...

Mkuu ndo moja ya molamu we isikie tuu
 
Tujaribu kutafuta chanzo cha tatizo
  1. Je wanafunzi hao wote walijiunga na shule hiyo wakitokea shule gani?
  2. Je huko walikotoka walishawahi kufanya aina hiyo ya matukio?
  3. Je tabia hizo zimekuwa zikionyeshwa na wanafunzi wote?
  4. Je uongozi wa shule ulishawahi kushuhudia tabia hizo kabla yao? Ulichukua hatua gani kudhibiti hali hiyo?
 
Form six leavers wanafanya ujinga huo? Shane
Ndiyo hao tunawaza, tunawalea, tunawasomesha, mwisho wa siku wanakuwa raia wasio na muelekeo na kusababisha nchi kutokuwa na utulivu
 
Mkuu kipindi cha mwishoni walianza adhabu zao za kishamba et tunabeba molam aiseee huyo alikua BAMBA...

Mkuu ndo moja ya molamu we isikie tuu
Sisi headmaster kipindi hiko alikua ana discovery 2 mupyaaa, yani michongo ya mbao na miti ikampa hela hatari....alafu vbarua wanafunziii😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…