Tabora wanahitaji msukumo wa ziada kiuchumi

Tabora wanahitaji msukumo wa ziada kiuchumi

Mkuu tabora unayoisema hapa sio kweli ,tabora inajitahidi japo mzunguko pesa sio mzuri ,roma haikujengwa kwa siku moja.
[/QUOT
Roma haikujengwa siku moja huo msemo hautumiki Kwa Tabora. Kumbuka kuwa Kisarawe na Tabora ni miongoni mwa halmashauri za mwanzo kabisa tangu wakati wa mkoloni, kudumaa kiasi hiki sio Sawa, mbaya zaidi wilaya zote na majimbo yote miaka yote ni CCM inaongoza.
 
nimekuelewa sana mkuu, sijui tatizo la sehemu nyingi ambazo waislamu ndio wengi, kazi ya hizo sehemu ni musikitini, kahawa na ubakaji period, angalia tanga miaka ya nyuma mji ulikuwa wa mbele sana sasa elimu ni madarasa tu

Kama ulivyosema sehemu wakiwa Waislam wengi hakuna maendeleo. Vivyo hivyo nchi ikiongozwa na Wakristo wengi hususan huku Kusini mwa Sahara isahau kupata maendeleo. Mfano mzuri ni Tanzania ambayo asilimia tisini ya viongozi na watumishi wa umma ni Wakristo ndiyo maana nchi iko hoi bin taaban. Maendeleo hakuna na kiwango cha umasikini kipo juu.
 
Maeneo mengi yanafikika law urahisi ndiyo maana hakuna daladala za magari
Daladala ni magari yanayofanya routes za ndani ya mji. Nitajie mitaa ya Tabora na routes zake za daladala. Mfano, nitajie daladala zinazoelekea Hospital ya rufaa ya Mkoa (kitete)
 
Kama ulivyosema sehemu wakiwa Waislam wengi hakuna maendeleo. Vivyo hivyo nchi ikiongozwa na Wakristo wengi hususan huku Kusini mwa Sahara isahau kupata maendeleo. Mfano mzuri ni Tanzania ambayo asilimia tisini ya viongozi na watumishi wa umma ni Wakristo ndiyo maana nchi iko hoi bin taaban. Maendeleo hakuna na kiwango cha umasikini kipo juu.
Ni ngumu kukubaliana na nadhalia hii. Oman, Dubai, Singapore, Malaysia, turkey, Egypt, Qatar, Kuwait, Moroco, Saudia, nk ni nchi zinazoongozwa na waislamu lakini ziko mbele kiuchumi. China ni nchi ya kipagani lakini iko mbele, Ulaya na Amerika kuna wakristo wengi na wako mbele kiuchumi pia. Nadhalia yako haina mashiko. Ziko factors nyingine Tu za kuifanya Tabora iwe vile ilivyo lakini sio waarabu wala wazungu
 
Uhalifu umezidi Tabora, hadi Mkuu wa Mkoa ameamua wananchi kupiga kura ya maoni kuwatambua wabakaji na wahalifu, huoni kwamba hali imekithiri?

Lakini uhalifu Tabora haukuanza leo, hata Tip Tipu yule mhalifu aliyekuwa akichoma nyumba za watu na kukamata watu wa kwenda kuuzwa alikuwa na asili ya Tabora.
 
Njoo Chemu-Chemu tutunishe Misuli ,Kisha Twende zetu Ng'ambo tukapate Mataputapu.
 
Ni ngumu kukubaliana na nadhalia hii. Oman, Dubai, Singapore, Malaysia, turkey, Egypt, Qatar, Kuwait, Moroco, Saudia, nk ni nchi zinazoongozwa na waislamu lakini ziko mbele kiuchumi. China ni nchi ya kipagani lakini iko mbele, Ulaya na Amerika kuna wakristo wengi na wako mbele kiuchumi pia. Nadhalia yako haina mashiko. Ziko factors nyingine Tu za kuifanya Tabora iwe vile ilivyo lakini sio waarabu wala wazungu

Mkuu hiyo comment niliitoa kumjibu jamaa mmoja anayejiita THE SEAL aliyesema kuwa Tabora haina maendeleo kwa sababu Waislam ni wengi na sehemu ambazo Waislam ni wengi hakuna maendeleo kwa sababu Waislam ni wavivu. Ndiyo nikamjibu hivyo.
 
Nmekaa Tabora miaka 3, Tabora maeneo mengi ni ya serikali na hayaendelezwi.
Mfano mzuri ni Magereza, Boma, Airport.
Biashara zinaenda wastani mfano nguo zinapata soko sana.
Kuna vyuo vingi mfano chuo cha uhazili, St. Augustine, AMUCTA na vyuo vidogo vinavyochangamsha mji na mabaharia.
Changamoto ya mkoa wa Tabora ni maji. Tabora kuna uhaba wa maji sana hali inayofanya pasifae kwa maisha.
Muda si mrefu wataanza kupata maji kutoka Victoria na kwa spidi ya Mh. Mwamri Tabora itakua Toronto.
Mkifanikiwa kuwaangamiza wale koboko tutakuja kuwekeza
 
Mji ukikua koboko wataondoka...Koboko wako kwenye mapori kama ya Inonelwa, Msangi, Kalunde, Igombe na mapori mengine.
 
Nasikia ni moja kati ya mkoa hatari kwa wapendamaendeleo especially wageni
Tabora mjini bado kuna nyumba nyingi za udongo, usafiri wa baiskeli, bodaboda kidogo Sana, taxi chache na kuukuu, daladala moja Tu. Hakuna kiwanda kama vipo labda 2 vidogo vya kuchapisha au mikate (mtanisahihisha).

Lakini hata maduka mengi hasa ya wenyeji hiwa yanafunguliwa saa 3 asubuhi na kufungwa saa 12 jioni. Nyumba zenye hadhi ya kulala watumishi sio rahisi kupatikana, mitaa ya wenyeji kuna wakora wengi.

Kwaakili yangu nilidhani kuwa maeneo ya karibu na airport kungekuwa kunauzwa bidha za Tabora kama vile asali, karanga, tumbaku na vitu mingine vinavyopatikana Tabora ili wanaosafiri kwa ndege pia wawe wanasaidia kukuza uchumi wa Tabora Kwa kuzinunua bidhaa zao Kwa urahisi. Lakini airport Yao imezunguukwa na majani Tu hakuna biashara yoyote inayofanyika maeneo yale.

Mzunguuko wa hela sio mkubwa sana hivyo maisha sio rahisi sana.

Nadhani Tabora inahitaji jicho la ziada.
 
Back
Top Bottom