Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu

Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu

Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu-5
Basi bana baada ya kupata hasara nilirudi kwa Bibi nikaanza kulia yaani ndoto yangu ya kusoma ndio imezima hivyo ,bahati nzuri Dada yangu yule mwalimu alikuja kumsalimia Bibi akanikuta Nina majonzi akaniambia kama unataka kusoma twende shuleni anapofundisha ili nirudie darasa ,kwa kuwa nilihitaji kusoma ilibidi nikubali kuliko kukaa karibu na kina mjomba ,basi tulisafiri nae mpaka sengerema akanitafutia nafasi ya kurudia nakumbuka ilikuwa mwezi wa kwanza ,nilisoma kwa uchungu sana hatimae tukafanya mtihani wa darasa la Saba ,matokeo Kuna kutoka nikawa nimefaulu shule Fulani ya kata , secondary nilijitahid kusoma japo nilipitia misuko suko mingi yaani ilianza kunitokea hali ya kunigwa usiku unakuwa kama umeshikwa na jinamizi yaani unaona na kusikia kinachoendelea lakini huwezi kuongea Wala kujibu ,nilijitahid kusoma hivyo hivyo mpaka tulivyofika form four baadae tukafanya final ,mwezi wa pili mwaka uliofuatia matokeo yakatoka .

Itaendelea

===
Muendelezo soma Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu
 
Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu-6
Matekeo yalitoka nikawa nimepata division 4 ya 26 ,kwa kweli niliumia sana sababu matarajio yangu nilitaka kwenda chuo Cha ufundi mbeya kinaitwa Mistry kwa hiyo kwa matokeo hayo nisingeweza kuchagulia ,baadae ikabidi nirudi kule visiwani kufanya kazi ndogondogo ,mama yangu afya yake nae ilikuwa imeshakuwa sawa baadae muda wa ku apply vyuo ulivyofika nilikuwa na pesa ya mama kama laki 8 hiv ,nikaenda kuomba chuo fulani Cha afya kozi ya utabibu sababu mama alikataa kabisa kunisomesha ,Mimi nikaona niingie hivyo hivyo kibabe ,nilivyoanza chuo nikawa napita kwenye misikiti kuomba msaada wa kusomeshwa ,nilitembea sana lakini sikubahatika kupata msaada baadae nikarudishwa nyumbani kwa sababu ya ada, nikarudi kwa mama

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app

===

Muendelezo soma Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu
 
Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu-6
Matekeo yalitoka nikawa nimepata division 4 ya 26 ,kwa kweli niliumia sana sababu matarajio yangu nilitaka kwenda chuo Cha ufundi mbeya kinaitwa Mistry kwa hiyo kwa matokeo hayo nisingeweza kuchagulia ,baadae ikabidi nirudi kule visiwani kufanya kazi ndogondogo ,mama yangu afya yake nae ilikuwa imeshakuwa sawa baadae muda wa ku apply vyuo ulivyofika nilikuwa na pesa ya mama kama laki 8 hiv ,nikaenda kuomba chuo fulani Cha afya kozi ya utabibu sababu mama alikataa kabisa kunisomesha ,Mimi nikaona niingie hivyo hivyo kibabe ,nilivyoanza chuo nikawa napita kwenye misikiti kuomba msaada wa kusomeshwa ,nilitembea sana lakini sikubahatika kupata msaada baadae nikarudishwa nyumbani kwa sababu ya ada, nikarudi kwa mama

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
Lete mwendelezo mkuu
 
Mimi ni kijana nilizaliwa mwaka 88 Mwanza mjini, tuliishi kwenye nyumba ya familia ile nyumba tuliishi familia mbili babu alikuwa na wake watatu hivyo pale walekaa Bibi zangu wawili na watoto wao ambao Kila Bibi alikuwa na watoto Saba Kila mtoto alikuwa na watoto wake pia hivyo waligawana vyumba, Bibi mwingine yeye hakuzaa, japo babu alikuwa na nyumba nyingine tatu.

Kila Bibi alikuwa amepewa nyumba moja na nyumba hizi zilikuwa zimejengea mitaa tofauti, kwa kifupi maisha hayakuwa mazuri pale tuliishi kigumu gumu, uwezo wangu darasani pia haukuwa mzuri japo nilikuwa siwi wa mwisho mwaka 2000 walielewana wauze ile nyumba sisi tulienda kuishi na Bibi yetu ambae alikuwa ameacha chumba kimoja katika ile nyumba waliogawiwa, vyumba vingine walikuwa wamepangisha Kodi watoto ndio waliokuwa wanachukua yeye hakupewa kitu.

Bibi yangu alikuwa mpole sana, watoto wa kiume ndio walipanga pembeni watoto wa kike walikaa na mama yao pamoja na wajukuu wale wa kiume pia kula walikuwa wanakula pale kwa bibi ,Bibi yangu alikuwa anajishughulisha na biashara ndogo ndogo aliweza kutulisha wote na matumizi madogo madogo alikuwa anatupatia ,kwakweli maisha Yale yalikuwa yananiumiza sana yaani kulala ni tabu wajukuu wengi mna lala mpaka uvunguni nilijaribu kwenda kwa mzee wangu kukaa sababu yeye alikuwa na nyumba kubwa tu ,lakin yule mke wake akakataa Mimi kukaa pale yule mwanamke alisusia Kila kitu akasema kama Mimi nakaa pale basi yeye ataondoka.

Baba ikabidi anifukuze ila niligoma kuondoka baadae baba akaniita pembeni kwa upole akanieleza nirudi tu kwa mama yangu akaniambia hanichukii ila Sasa hivi ni ngumu kumuelewa ila nikiwa mkubwa nitakuja kumuelewa basi bwana ikabidi niondoke zangu niende kwa Bibi tuliishi hivyo hivyo kwa tabu aise ,mwaka 2002 nilimaliza darasa la Saba sikufanikiwa kufaulu Bibi nae alikuwa ameshachoka Kila siku anaumwa baadae Bibi alishindwa kabisa kuendelea kufanya biashara ikabidi apumzike huwezi amini watoto walishindwa kumtunza kabisa yule mzee.

Itaendelea
I
Mtu mzima unalia kuteswa na familia yako si uondoke tu waachie familia yako.

Vijana waliozaliwa miaka ya 80 hawana akili kama hizi zako.
 
Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu -7

Nilivyorudi kwa mama nikamuelekeza umuhimu wa hiyo elimu ninayopata, pia tokea nimeingia chuo mungu alimjaalia sana mama yangu biashara zake zilikuwa zinaenda vizuri. Kuna wale matajiri walikuwa wananunua dagaa, pia walinisaidia kumshauri mama. Basi mama akalainika aka-nipa ada niliyokuwa naidai pia akahaidi atanisomesha kwa roho moja. Unajua, mama yangu muamko wa kusomesha alikuwa hana kabisa. Kuna dada yangu alifaulu vizuri tu, lakini alishindwa kumsomesha wakati kuna watu wanafanya biashara ndogo ndogo lakini wanamudu kusomesha watoto wao. Hivyo mama alipata moyo nakuanza kusapoti hii, ilifungua njia mpaka kwa wadogo zangu. Basi, mimi nirudi zangu chuo, aise nilijitahid sana kusoma yaani muda wote nilikuwa maeneo ya chuo sina cha jumamosi wala jumapili. Ni msuli kwenda mbele.

Sasa pale chuo, kulikuwa na msichana mmoja aliyekuwa anapiga msuli hatari. Alikuwa anaitwa Catherine na mara kwa mara angekesha kusoma. Nilivutiwa na juhudi zake za kusoma na tukaunda kikundi cha kujisomea. Kikundi hicho kilinisaidia sana na hata ufaulu wangu uliongezeka. Catherine alikuwa rafiki yangu mkubwa ingawa alizidi umri wangu kwa miaka mitatu.

Katika kusoma sisi wawili tukajikuta tukipendana na hatimaye tukawa wapenzi. Nilikuwa nikilala chini kwa mkeka wangu (jamvi) getoni kwangu, lakini baada ya mapenzi kuwa moto sana, nilihama kwenda kuishi na Catherine na tulianza kuishi kama mke na mume. Tulipiga msuli kama kawaida yetu na tulifurahia kila wakati.
Catherine alikuwa rafiki yangu mkubwa na tulikuwa na uhusiano wa karibu hata kama tulikuwa wapenzi. Wakati mwingine ilikuwa ngumu kwangu kuwa na ujasiri wa kumfanya awe mpenzi wangu kwa sababu nilikuwa bado mgeni kwenye mambo ya mapenzi. Kwa hiyo, tulizidi kuishi kama wapenzi wa karibu na kufurahia uhusiano wetu.

Siku moja Catherine alinipanga kwa mapema kwamba ilikuwa ni siku ya zawadi. Siku hiyo ilikuwa na maana kubwa kwetu na nilijua itakuwa siku ya kipekee.

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app

Muendelezo Soma Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu
 
Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu -8
Basi bana usiku ukafika tulitoka tukaenda gesti mbali kidogo na tunapokaa ,tulivyofika tukafanya malipo then tuka choma ndani ,dah kumbe Catherine alikuwa hajawahi kabisa kufanya tendo japo haikuwa rahisi hatimae nilifanikiwa.

Asubuhi ilivyofika Catherine aliongea Mambo mengi sana ,alisema nihakikishe nakuja kumuoa sababu alisema atakae mpa usichana wake ndio mume wake japo dini tulitofautiana lakini siyo shida kwenye mapenzi ya kweli ,basi tokea siku hiyo masomo yalienda tukichoka tulikuwa tunajipooza ila uyu msichana alikuwa yupo vizuri sana kichwani tulikuwa tunasoma wote lakini alikuwa ananiacha mbali sana .

Basi tukaweka mipango ya kuoana baada ya kumaliza chuo ,tuliendelea kusoma mpaka tulivyofika mwaka wa mwisho lakini haikuwa rahisi kufika hapo Kuna muda nilikuwa nakosa ada nasaidiwa na watu wengine kama Dada na mjomba wangu mmoja hivi .

Mwisho wa siku tulifanya mtihani wa mwisho na Kila mtu akarudi kwao .

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app

Muendelezo soma Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu
 
Back
Top Bottom