Tafadhali Anne Makinda jihadhari kwani Pius Msekwa si saizi yako. Msekwa katumia usomi kusema akina Halima Mdee wamefutwa Ubunge

Tafadhali Anne Makinda jihadhari kwani Pius Msekwa si saizi yako. Msekwa katumia usomi kusema akina Halima Mdee wamefutwa Ubunge

Kwani mama Anna Makinda hajui kuwa katiba ni Supreme law? Au ndio siasa za kukariri !
 
Kwa malumbano haya tunategemea maendeleo nnchi hii ilisemwa Chadema hawapo bungeni sasa tutaona maendeleo ghafla Chadema wanaingizwa bungeni na fujo zinaanza ukweli ccm wachawi na ni wagomvi.
 
Mjinga ni mjinga tu.

Mkuu hapa ndipo wengi mnapokosea.
Mtu mzima hata kama kakosea kwa maoni yako, bado anastahili lugha ya staha siyo kama hii uliyo tumia hapo juu.

Unapojisifu na kujipa hadhi ya mwanajumuiya ya wasomi basi tumia hekima na busara za kisomi katika mijadala ya kisomi.

Umejenga hoja nyingi mzuri sana kutetea maoni yako lakini lugha hii ya vijiweni imekuangusha sana.
 
Wewe wa ajabu kweli bilashaka utakuwa kilaza wewe hivi umesoma na kuelewa vizuri maoni ya Mama Makinda? Hoja yako haina mashiko umekurupuka usimlishe mama Makinda maneno yako
Mbona unakosoa bila kusahihisha alichosema mama Makinda? Wewe ndio ttzo kubwa zaid
 
Musitumie nguvu kubwa sana kumnanga huyu mama, huyu mama alikuwa mwema sana kwenye lile bunge alipokuwa spika vitu 2 nilikuwa namind sana, 1. Ile sheria ya kuwakingia vifua wabunge yeye aliitekeleza kwa nguvu zake zote hakujali upinzani wala nini 2. Mara kadhaa akimuinua Tundu Lissu - haya Tundu lissu nyi ndio wanasheria emu tuambie hapa tunafanyaje.

Lakini huyu mama alikuja akanishangaza sana wakati CCM wanasema Maalim Seif ataleta waarabu zanzibar yeye alipiga utaji na baibui la kamba kisirisiri akatinga kule Oman na kina Lukuvi kuiombea Tanzania misaada kutoka kwa Waarabu hao hao wanaowachukia.
 
Acha kudanganya watu ukidhani kila mtu ni mjinga katika taifa hili.

Mwaka 1967 TANU iliwafukuza uanachama wabunge wake kadhaa na siku hiyohiyo Tanzania nzima ikatangaziwa kama kwamba kuanzia siku hiyo si wabunge tena. Mmoja wa wabunge hao ni Masha. Mwaka huohuo ikawafukuza wanachama wengine na siku hiyohiyo ikawatangazia dunia kwamba wamefutwa uanachama. Oscar Kambona alikuwa ameshakimbia nchi yuko Uingereza na akapatia taarifa kwenye vyombo vya habari.

Wakati Julius Nyerere a TANU inawafukuza hawa wote Pius Msekwa alikuwa ndiye katibu mkuu wa TANU. Wewe na mama yako Anne Makinda mlikuwa wapi.

Mwaka 1988, CCM iliwafukuza uanachama akina Seif Sharif Hamad na wenzake na siku hiyohiyo ikatangazwa nchi nzima kuvuliwa nydhifa zao zote. Mama yako Makinda alikuwa tayari serikalini, hukumbuki na yeye hakumbuki.

Kukumbuka siyo issue, issue ni ukilaza wenu wa kupekua historia.

Narudis, CCM iandae vijana ma genious kama Nyerere alivyowaandaa hawa akina Msekwa, Generali Ulimwengu na siyo CCM ya sasa ina vijana wanajua kujipendekeza na kutafuta lipi la kusifia leo.

Mzee Msekwa amewahi sana kutoa tamko lake nazani naye anajua kinachowafukuzwa hao wabunge uanachama wao chadema sio tamko la Mbowe kwenye vyombo vya habari bali ni barua watakazoandikiwa hao watuhumiwa wakielezwa makosa yao na vifungwa na kanuni za chama chao walizovunjwa. Pia Spika wa Bunge kujulishwa rasmi kwa barua.

Sasa kabla ya haya yote kutekelezwa huwezi kusema aliyosema Mzee Msekwa. Tena barua hiya uhakikishe wahusika imewafikia, ambapo na wao wanayo haki ya kuchukua hatua za kimahakama kujitetea.
 
Wewe ndo umesema ukweli. Wamama wameshaapa na kutangazwa kuwa ni wabunge halali; huwezi kuwafuta uanachama kwa matamko ya kwenye press conference. Inabidi spika aandikiwe barua rasmi kutaarifiwa. Chadema wakimwandikia spika maana yake wanamtambua rasmi, na kwa hiyo wanatambua matokeo ya uchaguzi ulimweka kwenye uspika!
 
Uzi umeshiba kama Bikiroboto hataelewa basi ana tatizo kubwa kichwani mwake.
 
MKUU MUNGU AKUBARIKI SANA KWA HAYA MADINI ADIMU AMBAYO NI CHAKULA KIZURI CHA UBONGO 🙏🙏🙏🙏👏👏👏🥰🥰
 
Nguvu kuuuubwa
Wale tayari ni wabunge, Mpaka zile Milion tisini tayari wamepata

Na nyie mmewafukuza Sasa makelele ya nn?
 
Mzee Msekwa amewahi sana kutoa tamko lake nazani naye anajua kinachowafukuzwa hao wabunge uanachama wao chadema sio tamko la Mbowe kwenye vyombo vya habari bali ni barua watakazoandikiwa hao watuhumiwa wakielezwa makosa yao na vifungwa na kanuni za chama chao walizovunjwa. Pia Spika wa Bunge kujulishwa rasmi kwa barua.

Sasa kabla ya haya yote kutekelezwa huwezi kusema aliyosema Mzee Msekwa. Tena barua hiya uhakikishe wahusika imewafikia, ambapo na wao wanayo haki ya kuchukua hatua za kimahakama kujitetea.
Membe alipewa lini barua yake ya kufukuzwa uanachama wa CCM? Pumbavu sana wewe.
 
Tatizo ni kwamba leo Msekwa ataonekan wa maana kwa sababu kaongea jambo lenye kuwafurahisha watu fulani ila Msekwa huyohuyo siku nyengine akiongea jambo lisilowafurahisha hata kama ndio ukweli basi ataonekana ni hovyo.

Tuache hii tabia.
Huko sahihi na Ndugai aache kuinajisi katiba kwa kuwalinda kinyume na katiba na sheria, maana wakishauriana na jiwe utaona matokeo yake!
 
Back
Top Bottom