Tafadhali: Mwenye habari kamili kuhusu kuuawa kwa mwalimu huko Kinyerezi Dsm, mtaa wa Kifuru- Msitu wa Nyuki.

see.

mimi silaumu jamaa kutafuta haki yake halali mahakamani,kama ambavyo nyinyi mmefanya.
fikiria kwa mazingira yenu hayo hayo,baba mdogo angefika bei kwamba amaepaelewa pale kaamua kuwalipa baada ya kushindwa mahakamani.
ni haki yenu kukataa,lakini kuchukua hela ni uamuzi salama zaidi.

mwalimu anapewa ofa kakomaa,anataka eneo lake hataki hela,kapigwa risasi.
nini faida yake sasa!!!!
 
Ona huyu, kama huna kiwanja , huwezi jua thamani yake.

Ni sawa na mtu agonge hiyo Vits yako halafu akuombe msamaha yaishe. Utakubali ?
 
Mwenye nyumba alivamia kiwanja cha huyo mwalimu. Kesi ikaenda mahakamani. Mwenyenyumba akashindwa. Ikaamuliwa nyumba ibomolewe. Akamwomba mwalimu amuuzie. Mwalimu akakataa.
Risasi zikafuatia baadae.
Nyumba ilijengwa siku moja??
 
Labda mahusiano yao kabla, wakati na baada ya kesi yalikua halijojo sana. Na si ajabu hata huko kuomba kuuziwa ni kishari na majibu yakatoka kishari vilevile.

Ngoja tusubiri wanaolijua hili sakata watujuze.
Na hapo ndo huwa mambo yanaanzia...Unaweza kuta walileteana ubabe, Makasirikiano, madharau, mavutano...Wakapelekana Mahakamani, huko ikawa Chui na paka...Mmoja akashinda, alivyoshinda na yeye akawa mbogo, hakutaka kusikia kitu, maana anaweza kuwa alikumbuka matambo ya aliyejenga...basi Tafraji....akaona asimsamee kwa kumuuzia sasa, kama mbwai na iwe mbwai.

Asee, watu tusipende ubabe hata stage ya kwanza...tujifunze kutuliza hasira.
 
Kwa kweli wavamizi wa ardhi wanaleta sana! Ila sasa kama wamefikia mahali wameamua kutupiga risasi hii ni changamoto sasa! Hata mimi napambana na kesi ya maamuzi kavamia ardhi yangu ambayo ina hati milki ya miaka 33. Eti kauziwa na mtu ambaye anakimliki hicho kiwanja kwa mdomo yaani bila hata aibu eti anaukizwa kiwanja wala hakuna documents za serikali ya mtaa wala ofisi ya ardhi. Akapeleka kesi baraza la ardhi, hakimu mamamake eti anakuja kutoa hukumu eti kiwanja nilikipata kwa rushwa! Sasa kesi iko mahakama kuu!
 
Na hapo keshi ikiisha, hakuna mtu atamuone huruma mwenzie...najua hapo kuna uhasama balaa, utakuta hata hamsalimiani tena.

Watu tujitahidi kuelewana kabla ya mahakamani.Ila pia kuna vitu vinatia hasira sana.

Yote kwa yote; Mungu atusaidie sana[emoji120]
 
Hivi mke kapigwa risasi mbele ya mme wake?au

Inakuwaje,mme kaishiwa kupigwa mkwala tu

Kuoneshwa bastola! Au nimesikia vibaya hii taarifa

Ova
 
Kabisaa mkuu uhai ni muhimu sana. Labda tu ni ile kutotaka kua chini, kwamba nikimkubali nitaonekana mi zuzu na tambo zisizo na msingi bila kusahau chawa wanaowapa bichwa na kujiona wao ni bora zaidi.
 
Sasa mkuu eneo ni langu,nikubali kuuza kwasababu zake??

Vipi kuhusu sababu zangu kuwa sitaki kupauza,huyo mwalimu alikuwa na haki ya kukubali au kukataa.
 
Kuna mafala wawili wamejiegesha kwenye kiwanja
 
Mungu amlaze mahali pema peponi

Serikali imkamate mhusika hukumu ni kunyongwa hadi kufa.

Ukoo wake wote wasipewe umiliki wa silaha yoyote kwasababu zozote zile .

Hiyo nyumba wapewe warithi wa marehemu ili kufidia gepu la mtegemezi wao


Muuaji aamuliwe kulipa gharama za matunzo za wategemezi wa huyo mwalimu .KISHA ANYONGWE HADI KUFA .

Wito wa wananchi wa eneo hilo kupaza sauti kuhakikisha haki inatendeka.

Ni ajabu hadi leo sijasikia Polis kulizungumzia tukio kubwa kama hilo.

Hii inaashiria muuaji huenda katembeza Rushwa ili kulizima KAMA KWELI LIMETOKEA.

MWISHO,Kabla ya kununua ardhi ,Kujiridhisha kwenye ofisi za ardhi na tuuziane kwa kutumia MAAFISA WA VIAPO.Watendaji hawana mamlaka ya kusimamia uuzaji wa ardhi

Mwisho tuwe tunasisitiza mara kwa mara kwenye site zetu.

Amina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…