Mm naamini ili uwe kiongozi au ili uwe mtu wa aina flani ni lazima uwe kwenye cycle flani hv, hauwezi ukawa rais kutokea sehemu ambayo haieleweki hata kama ni mtu kutoka chama pinzani kuwa rais ni lazima uwe umeishi kwenye cycle iliyoandaliwa itakayokufanya uwe rais.
Hao walinzi wa viongozi wakubwa sio rahisi uwakute kwenye aina flani ya maisha kama kupiga picha n.k mana wanakuwa wameandaliwa kwa jambo fulani hata kama jambo hilo ni gumu kutokea.
Mfano wale walinzi wa Samia, sidhani kama kuna mtu alijua mwaka flani rais atakuwa mwanamke ila wale walikuwa tayari kwenye cycle ya kuwa pale na walishaandaliwa muda mrefu bila kujua ni muda gani watakuwa kwenye hiyo nafasi.
Mfano yule aliyekuwa mlinzi wa pembeni wa Magufuli, alikuwa Facebook lakini last seen yake ilikuwa ni 2012 miaka mitatu kabla ya kuwa mlinzi wa Magufuli hiyo inaonyesha labla ndipo alipoanza kuwa kwenye cycle itakayomfanya awe mlinzi wa rais.