Vawulence
JF-Expert Member
- Jan 4, 2009
- 1,930
- 2,118
Sikusoma Kibohehe ila najua mengi kuhusu hiyo shule.Mbona mnaona shida kumtaja Zito Kabwe kuwa alisoma hapo?Mwalimu Ndanu kwa sasa anafundisha S.T Theresia iliyoko Mailisita.Malya bado yuko BAKWATA.Kibanda cha njiwa kipo ila ni useless kwa sasa.Vyoo ni vile vile ulivyoacha,nyumba za walimu wanaishi popo kwa sasa,mabweni hayajabadilisha majina ila ni kama chuma chakavu.Hivi ulikuwa unafahamu kuwa ile shule ilifutwa na kuanzishwa upya?Kwa kweli hata mimi pamoja na udogo wangu ninafahamu wakubwa wengi waliopitia kibohehe.Halafu huyu Exaud Makyao si yule mkuu wa sekondari ya Uroki?Kwa sadala kwa sasa si mbaya japo nasikia polisi bado wanapaogopa.Walitaka kujenga kituo cha polisi kwasadala ila walipoleta matofali kurudia mengine tu yale ya mwanzo hawajayaona hadi leo.