Tafadhali usikikate kitunguu maji ukakibakisha ili kesho yake ukitumie tena haifai kabisa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363





Unapotumia kitunguu maji kukikata usikibakishe ili kesho yake ukitumie tena. kile kitunguu Maji

unacho kibakisha

kinageuka Sumu na kinatengeneza wadudu wa sumu. Ukikitumia kile kitunguu Maji kilicho bakia jana yake ulicho kikata

huenda utapatwa Maradhi kwenye Utumbo wako au hata nyonga yako ikadhurika na kukusababisha ule chakula

chenye sumu tafadhali usifanye hivyo kabisa.
 

Attachments

  • kitunguu maji.jpg
    107.4 KB · Views: 1,444
Ina maana hiyo sumu au backteria havifi hata ukipika ?? au madhara zaidi ni kwa kukitumia kitunguu kilicholala kama kachumbari?
 
Ina maana hiyo sumu au backteria havifi hata ukipika ?? au madhara zaidi ni kwa kukitumia kitunguu kilicholala kama kachumbari?
Mkuu madhara kukitumia hicho kitunguu Maji ulichokikata na kikalala usiku kucha pasipo na wewe kukitumia tena mpaka siku ya pili yake ndio wewe unataka kukitumia ndipo hapo kinakuletea madhara sio kachumbari si utaiweka kwenye friji?
 
hujaeleweka wala kuelezea ukaeleweka MziziMkavu funguka zaidi maana hao bacteria wangekua sumu basi ingekua balaa...
 
Last edited by a moderator:
Kama ni hivo watu wengi wangekuwa washakufa

Ni kweli kabisa watanzania wengi tungekuwa saa hizi marehemu, wewe MziziMkavu hebu uliza kwenu hamkawahi kupikia kitunguu wacha cha jana hata cha juzi. Mimi nakumbuka kabisa kitunguu kwetu kilikuwa hakipikii mara moja mpaka na ukubwa wangu huu sijaona mtu amekufa kwa kula kitunguu cha jana au juzi, wacha tu kitunguu cha kupika tunakula hata kitunguu kibichi kwenye kachumbari. HIYO NI UONGO KABISA KWETU LABDA HUKO KWA WAZUNGU AU VYA KICHINA.
JOKE: KUNA WAKATI WACHAGA WALIKUWA HAWALI MIHOGO WANASEMA MIHOGO INASUMU. KWANI KUNA MMOJA WAO ALIWAHI KULA MUHOGO AKAFA.
 
Nadhani kijijini wote wanaumwa, nakumbuka kule hakuna umeme achilia mbali fridge na mwendo wa kukata kitunguu kitumike kesho yake ndio kawaida.Hizi tafiti nadhani zinategemea ni watu wa sehem gani ndio wanaathirika na hao bakteria.
 
Mkuu hii habari nadhani ishawahi kanushwa maana kuna wakati ilisambaa sana kama 'hoax'.

Kitunguu kinaweza hifadhiwa ndani ya jokofu kwa takribani muda wa siku 7 na kikawa 'fresh' kwa matumizi ya binadamu.

Kwa mujibu wa Dr Joe Schwarcz, mwanasayansi na mwandishi kutoka Chuo Kikuu cha McGrill:
Kitunguu kilichokatwa huwa kina 'enzymes' ambayo husababisha kutengenezwa kwa tindikali ya 'sulphuric'. Kwa kawaida tindikali hii huwa inazuia ukuaji wa vijidudu.

Wakati pekee ambapo kitunguu kama chakula kingine kinaweza kuwa 'contaminated' ni namna tu ya 'handling'.

Hivyo hakuna namna nyingine yoyote ya kikemikali ambayo inavifanya vitunguu kutengeneza sumu kwa dhana kuwa pindi unapokikata huwa kama sumaku kwa bakteria.

Sources:
http://oss.mcgill.ca/yasked/onionsbacteria.pdf

www.onions-usa.org/img/site_specific/uploads/Cut_Onion_Statement.pdf
 
Hapo mzizimkavu umeprove failure aisee maana uliulizwa hata kikipikwa vijidudu havifi?au ni kikitumika kwa kchumbari yaani hiko kilicholala bt ukajibu off point,i think jamaa f inageuka something else i cant trust majibu wala ushauri hapa tena honest speaking modes tusaidieni plz
 
Hapo mzizimkavu umeprove failure aisee maana uliulizwa hata kikipikwa vijidudu havifi?au ni kikitumika kwa kchumbari yaani hiko kilicholala bt ukajibu off point,i think jamii f inageuka something else i cant trust majibu wala ushauri hapa tena honest speaking modes tusaidieni plz
 
Kitunguu ukishatia kwenye moto bacteria wanakufa.hata kachumbari unapoweka ndimu au vinegar bacteria wanazya safari.mpaka sasa nshapika sana na kubakisha vitunguu na kutumia hata baada ya siku 3.hamna sumu yoyoote
 
Elewa dhana ya Forums...sio kila ukionacho hapa ni sahihi au batili, una nafasi ya kufanya uchunguzi.

Una nafasi huru ya kueleza nawe fikra zako pevu ukiwa ama na vyanzo makini au tafakari makini.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…