Tafadhali wadau naomba mnisaidie 5m Tshs nikakomboe hazina

Status
Not open for further replies.
Wadau, huyu nimemfahamu.....ni tapeli fulani hivi sasa anataka kula vichwa hapa JF. Intelijensia ya Kova isingeelekeza nguvu kuzuia maandamano halali ya Wananchi, watu kama ndio wangekuwa sehemu ya kupandishwa cheo kutokana na utendaji uliotukuka!
 
Jamani hii kitu haina utapeli wowote wale nilioongea nao ana kwa ana wamenielewa na hawakuwa na shaka yoyote. Ila walishindwa tu uwezo wa kunisaidia. Nyote mnaokandia kama tungewasiliana nikawapa details mgeweza kuelewa. Hakuna utapeli hapa na mimi sijatapeliwa Wanaijeria hawahusiki kabisa. Labda suala la collateral hilo naona laweza kuwa ndio kikwazo lakini mchakato mzima ni wa halali kabisa. Kuhusu kulipa mara 2 kwani kuna tatizo gani? Sihitaji mkopo wa biashara bali ni kama nilivyoeleza juu. Kwa hiyo tusikokotoe kibiashara. Whoever is interested ani pm I am serious.
 
Wadau, huyu nimemfahamu.....ni tapeli fulani hivi sasa anataka kula vichwa hapa JF. Intelijensia ya Kova isingeelekeza nguvu kuzuia maandamano halali ya Wananchi, watu kama ndio wangekuwa sehemu ya kupandishwa cheo kutokana na utendaji uliotukuka!

Mtazamo wako tu mimi sio tapeli na sijawahi kufanya utapeli wowote.
 

MKuu, naomba nikuulize swali moja la msingi; HIYO PESA UNALIPWA KWA AJILI YA NINI (Umefanya biashara na mtu, ni deni unalipwa, ulikuwa mwajiriwa)?, fafanua kidogo hapo mkuu kwa jinsi ulivoiweka naona kama unataka kuibiwa au umeshaibiwa tayari! Funguka tuone kama tunaweza kupigana tafu!
 
Pole sana kwa matatizo yaliyokupata ndg yangu pesa ni kitu kingine kabisa watu sasa hivi wameshapoteza iman watu wanataka uweke kitu rehan akupe hela hapo utapata ila useme mtu akupe tu bila dhamana hapo utachemka

Nimekuelewa sana mkuu na mimi hofu yangu ipo hapo.
 
Huyo jamaa ni tapeli tu. Umkopeshe akulipe mara2 ya pesa ko dunia ya wapi hiyo

Kulipwa mara mbili wala haina maneni inategemea ni biashara gani anafanya, mashaka yangu ni kwamba yeye ndiye kalizwa, maana ramani siisomi hapa! Huyo mwanasheria wake yeye kaiogopa deal, maana angeichangamkia faster akakopa hata hiyo pesa, si anauhakika atapata twice in less than a month!
 
Huna collateral yeyote? Au ndugu akuthamini ungepewa mikopo binafsi ya dharura watu kukuamini ngumu

Nashukuru sana Mama Joe labda nijaribu namna ya kupata mkppo. Nikifanikisha hili suala nitawafahamisha.
 
Nadhani huyo kapigwa maana kwenye mitandao kuna udanganyifu sana.

 

Nitakujibu kwa pm.
 

Nitakujibu kwa pm kesho vumilia kidogo mkuu.
 
Samahani,
akaunti yako ya M-PESA haina kiwango cha kutosha kutuma Tsh5,000,000 kwa ISRAEL NSIBU
Salio lako la M-PESA ni Tsh 0.00

Pole sana mkuu nilikua na nia..
 

Sijawahi kutoa ofa ya namna hiyo kwa mwanasheria wangu. Kimsingi mwanasheria yuko upande wangu nitaku pm utaelewa tu.
 
Kuna jamaa kule Morogoro (SUA) aliingia mkenge huu huu wa hawa matapeli, 2008. Alitakiwa alipie na alilipa Tshs million 21 kama gharama za kuhamisha pesa( dollar 3bn) kutoka benki moja kule South Africa kuja kwenye akaunti yake CRDB. Hadi leo hajapokea hela yoyote kutoka SA zaidi ya kulipa madeni (sababu pesa aliyowatumia alikopa benki) na kupata stroke. Jihadhari, chukua hatua!
 

katika stori hii nilitegemea utasema uko kwenye kambi ya wakimbizi senegal
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…