Michael mbano
JF-Expert Member
- Apr 4, 2022
- 820
- 570
Wiki hii nilikuwa kwenye matembezi yangu mtaani mzazi fulani akiwa hoi anatoka shamba akakimbiliwa na mwanaye mtoto akamwambia mzazi,kule shule wameagiza traksut mzazi akaonekana kuzidi kuchoka mana hali ngumu ya maisha inampiga na mtoto ndiyo hivyo.Ukimuangalia mtoto kavaa yebo ametoka shule simuda.Je ikiwa hali ya wazazi wengi si nzuri kiuchumi ni sahihi serikali kuagiza watoto wawe na track?Mana ukikaguwa wanafunzi ktk shule wengi hawajakamilisha mavazi mtoto viatu husika vya shule,soksi,na sweta vyote muhimu mzazi hakukamilisha je trak?Karibu kwa ushauri