mcshonde
Member
- Jul 15, 2022
- 66
- 154
Edward Snowden, mtaalamu wa Kompyuta na wakala wa zamani wa shirika la usalama wa taifa Marekani, NSA. Alipamba vichwa vya habari ulimwenguni baada ya kufichua udukuzi mkubwa unaofanywa na NSA duniani kote..huku akitajwa kuwa ni shujaa, msaliti, mzalendo na muasi. Aliamua kuweka ukweli hadharani.
Katika moja ya mahojiano aliyofanyiwa aliwahi kueleza kuwa Marekani kulikuwa na kitengo cha kulisha watu taarifa zenye chembe chembe za uongo. Taarifa hizo zilipaswa zitoke kwenye mamlaka kubwa kubwa pamoja na kuchapishwa kwenye magazeti kwa jina (by line) ya mwandishi anayeaminika na jamii. Alichokuwa anafanya ni kujenga ukaribu na mwandishi husika na kumpa taarifa za kweli kabisa.
Fact tupu...katika kuzoeana naye..anampa "za ndani" za uongo anayotaka isambae...kwa kuwa ni Exclusive ya moto...mwandishi huyu atawatafuta mabalozi/ watu ambao wanahusika ili kupata uthibitisho, kumbe nao wameshapenyezewa huo uongo ukweli. Mwisho wa siku akijumlisha na mambo tisa ya kweli aliyoambiwa na akina Snowden..la kumi analibeba kama lilivyo. Linachapishwa gazetini...watu wanaamini.
Kuna muda mstari kati ya uongo na ukweli unachanganya. Mpaka wake haujulikani. Kinachobaki ni imani/trust. Imani kuwa kilichoandikwa ni sahihi. Kinachosemwa na tunayemuamini ni sahihi. Hata macho yetu na akili ya kawaida (common sense) ikituonyesha walakini, tunaamua tunaishi humo humo labda kwa sababu yale tisa ni kweli kabisa huku moja ambalo ni hatari kuliko yote..ni uongo.