TAFAKURI CWT: Kwani umoja wa walimu hawawezi kumiliki kampuni/kitengo chao cha ujenzi wakawa wanajenga shule zao wenyewe kama wafanyavyo SUMA JKT?

TAFAKURI CWT: Kwani umoja wa walimu hawawezi kumiliki kampuni/kitengo chao cha ujenzi wakawa wanajenga shule zao wenyewe kama wafanyavyo SUMA JKT?

Mbona walipojenga jengo la kitega uchumi hamkuwapinga? Tena wakaamua kuweka na ofisi zao humo humo...!!!

Sasa inakuwaje wao kuanzisha kampuni ya ujenzi mnapiga kelele namna hii?

Katika suala la chakula mbona wanakijiji wanalima mahindi yao kama chakula huko vijijini?
Mkuu una kitu inaitwa narrow view.
Parochial in fact.
 
Habari zenu waheshimiwa wa humu jamiiforums.

Eti ndugu zangu;

Kwani umoja wa walimu hawawezi kumiliki kampuni/kitengo chao cha ujenzi wakawa wanajenga shule zao wenyewe (Primary & Secondary) kama wafanyavyo SUMA JKT?

Kwanini tenda apewe mkandarasi mwingine wakati walimu wanaweza kuunda umoja wao kisha wakafungua kampuni kuuuubwa sana ya ujenzi wakawa wanachukua tenda za ujenzi wa shule za msingi pamoja na secondary.

Kwani CWT si ni chama cha walimu Tanzania? Au mimi ndio sijui? Yale makato wanayoyapata kutoka kwa walimu si wanaweza kukusanya mtaji wa kutosha wa kufungua kampuni ya ujenzi na kuwa wanapiga pesa ya maana?

NB: Mimi Infantry Soldier sio askari jeshi wala mtumishi wa ofisi yoyote ya serikali bali ni raia mwema ninayeipenda sana Tanzania yangu.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
SUMA JKT wa kale wapi?
 
Back
Top Bottom