Subira the princess
JF-Expert Member
- Mar 3, 2018
- 3,474
- 3,744
Wasalaam,
Kuna mambo mengine yanahitaji kufikiri kwa upana hasa kipindi hiki tunapoelelea katika uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani. Nimefatilia uzinduzi wa kampeni za CCM pale uwanja wa Jamhuri Dodoma, nimeangalia nyuso za wasanii waliotumbuiza katika tamasha lile la CCM na kuona wengi wana mashaka katika kile wanachoimba. Nimeshindwa kutambua yale ni mahaba kwa CCM, njaa, au bendera fata upepo?
Wasanii wa bongo wamekuwa wakitumika na CCM kila unapofika Uchaguzi na baada ya Uchaguzi wamekuwa wakitupwa katika dustbin kama takataka nyingine zitupavyo. Hivi ni kweli wasanii hawa hawajitambui au ni njaa inawasumbua? Hivi ni kweli wasanii hawa hawaoni Uhuru wa vyombo vya habari ulivyoyumba? Hivi ni kweli wasanii hawa wamesahau yaliyowakumba katika miaka5 ya CCM? Maana kuna waliotekwa, kufungiwa nyimbo zao n.k hawayakumbuki haya au wametishwa?
Mwisho nawakumbusha wasanii wekeni maneno yangu akiba baada ya Uchaguzi kwisha CCM hao hao watawasomesha namba, CCM ni ile ile haijawahi kumtetea mnyonge.
Maendeleo yana vyama.
Nukuu ya leo "Siwezi kupeleka maendeleo jimbo mlilomchagua mpinzani". (Kauli ya Rais Magufuli akiwa Lindi)