No Reform No Election: Tafakuri ya Mtanziko wa Kisiasa
Mimi ni mzalendo na mchambuzi wa mambo ninatafakari dhana ya No Reform No Election kwa kina, ninapata tatizo kuelewa Chadema inataka nini hasa.
Ni kweli upinzani, ikiwemo Chadema, zimepata maumivu sana kwa uchaguzi wa 2019/2020 na hali ikaendelea 2024.
Hoja ya mabadiliko ya sheria kabla ya uchaguzi ni ya muhimu ili kuwa na uchaguzi ulio huru na haki inaeleweka na watu wengi, lakini ukiangalia sana kinachokosekana siyo mabadiliko ya sheria pekee bali pia uzalendo na utashi wa kisiasa kwa watendaji wa serikali, viongozi wa siasa, na viongozi wa dini.
Mimi ninaamini Mwenyekiti wa CCM Taifa akitoa maelekezo kwa serikali na mahsusi kwa Tume na vyombo vyote vya serikali kwa waraka wa kimamlaka na hatua zitakazochukuliwa kwa anaye kiuka, upande wa Chadema wajue bila hivyo na wasipopata sapoti ya serikali wakishiriki uchaguzi wataambulia wabunge 2 au hakuna.
Vivyo hivyo kwa vyama vingine vya upinzani. Wasiposhiriki uchaguzi watapoteza kuwa chama cha upinzani.
Hapa ndipo wanapaswa watumie sayansi ya siasa. Mimi nashauri bado wanayo nafasi ya kuwasiliana na Rais, serikali, viongozi wa dini, nchi za nje na wadau wengineo kubadili hali iliyopo na mitazamo ya kisiasa.
Vinginevyo, mtanziko huu unahitaji njia mbalimbali mbadala na ikiwezekana kufanya mikutano na makongamano, warsha na wadau mbalimbali ikiwemo serikali kujadili suala hili.