Ni tatizo la watanzania kukabidhi umuhimu wa mabadiliko kwa CHADEMA na Rais, wakati suala hili pamoja ya kuwa CHADEMA inajenga hoja ya No Reforms No Election inabidi sote kwa pamoja pia popote tulipo kwa nafasi zetu tujadili mabadiliko maana tumeona kwa mifano hai November 2024 uchaguzi ulivyo fanyiwa uchafuzi
Media House vyombo vya habari vialike watu wa kila namba wajadili tulichokiona 2024 ni Mabadiliko gani yanahitajika, hii tabia ya kuiachi ajenda hii ni kama Derby ya CHADEMA VS RAIS kuwa Haituhusu ni kilema na upungufu mkubwa.
Kwanini nchini Tanzania tunakabidhi kila kitu kwa kikundi kidogo kuwa ni jambo lao yaani CHADEMA na MAMA. Suala hili nyeti linahitaji mjadala mpana na wa wazi au ni mbinu ya CCM kulifanya jambo la Mabadiliko ni la CHADEMA na Rais wa nchi.
Haiwezekani kuendekeza hulka hii ya unyonge wa kukabidhi kazi ya kufikiri kwa kikundi cha watu wachache.
Mimi naamini hulka hii imetengenezwa kwa hila kubwa na CCM kuwa waTanzania wajikabidhi kwa mtu au watu wachache wafanye zoezi la kufikiri na mwishowe waseme watanzania hawahitaji mabadiliko ona ni CHADEMA tu ndiyo wanaoongoza No Reforms No Election huku wengine walio wengi hawajitojezi kulijadili kama ulivyo mjadala wa mechi ya Derby ya Yanga na Simba ilivyo shindwa kufanyika.