Tafakuri: Kuhusu No Reforms No Election, CHADEMA bado wana nafasi ya kuzungumza na Rais

awamu yapili ndo itaeleweka zaidi baada ya siku 48

Ila ,naunga mkono kwamba ccm tayari wanaidadi ya wapiga kura mkononi kila eneo ambapo tayari wameandikisha,tuone NO reforms itazuiaje hao watu
 
Huu ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani. Sioni chochote cha kuzuia uchaguzi huu.
 
Umenena vema kabisa, suala la kuwa na Tume huru Kabisa, sheria na mifumo inayoaminika kwa wote ya uchaguzi ni suala la kitaifa na siyo la Chadema peke yao.
 
kitaifa na siyo la Chadema peke yao.

Hapa chama dola kimeibinafsisha hoja ya Mabadiliko ni ya CHADEMA na Rais tu.

Wakoloni weusi wa chama dola kongwe wanatumia njia ya kugawa watanzania kuwa hoja hii ya Mabadiliko inahitajiwa na kundi moja la waTanzania wakorofi.

Inaelekea kuwa CCM imefanikiwa kubinafsisha hoja hii, na watanzania wengi wamejitoa ufahamu ni hivyo na kukubali kuwa mabadiliko ni fujo za waroho wa madaraka wanaotaka kuchukua dola kwa vurugu kutoka mikononi mwa chama dola kongwe tawala CCM.

Waswahili walisema : Ukitaka kumuua mbwa, mpe jina baya. Hoja ya Mabadiliko ya No Reforms No Election hadi sasa imekatiwa jina baya, kwa kiasi fulani CCM imefanikiwa na propaganda hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…