Tafakuri: Kuna nini nyuma ya mashambulizi haya kwa Makamba?

Tafakuri: Kuna nini nyuma ya mashambulizi haya kwa Makamba?

NIMEONA

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2019
Posts
3,862
Reaction score
5,693
Kumekuwa na mfululizo wa threads za kumpondea Makamba kila uchao!

Akijikwaa basi inafunguliwa thread hasi dhidi yake;

Akikohoa basi inafunguliwa thread hasi dhidi yake;

Akisalimia basi inafunguliwa thread hasi dhidi yake;

Akisalimia hali hiyohiyo;

Akitoa zawadi, kama wanavyofanya wengine ambao walikuwa wanagawa mpaka hela, hali hiyohiyo;

Akikaa kimya hali hiyohiyo;

Threads zote hizi, zinakuwa na shutuma moja au mbili tu kuu; MAKAMBA MWIZI NA ALIFELI KIDATO CHA NNE ingawa kuna ulazimishaji wa nyingine pia kuwa eti ANAMSEMA MAREHEMU JPM! Cha kuchekesha, threads zote hizo hakuna hata moja inayotoa ushahidi wa huo wizi na huko kufeli kwake.

Na cha kuchekesha zaidi ni kuwa baadhi ya wanaotoa shutuma hizo wamefeli vibaya, katika elimu hadi maisha, na ushahidi wa kufeli kwao upo wazi kabisa kuliko huyo Makamba.

Hili jambo, kwa jicho la tatu, linafikirisha sana. Kwa hakika hapa kuna kitu si bure hii. Labda uwe poyoyo ndio hutoona kuwa kuna jambo la hila limejificha hapa!

Yule Musiba alipokuwa anakesha na kuwezeshwa vizuri kumtukana Makamba huyu, alijibu kidogo tu lkn kwa ufasaha kabisa kuwa, 'Siwezi kujibizana na mjinga!'

Juzi hapa kawajibu kidogo tu hawa wachambaji wa mitandaoni kuwa wasilete upuuzi wao, basi wamejifanya kubadili gia na kulipeleka jibu hilo kwa kamati ya bunge wakiamini litamuathiri zaidi na mamia ya threads sasa yanafunguliwa kwa ajili hiyo.

Unless proved otherwise, nitaendelea kuuona usmart wa Makamba vizuri kabisa katika nafasi ya uongozi alionao na hata kuzidi hiyo!
 
Shida ya Makamba Jr ni kutegemea siasa kuendesha maisha yake.

Lingine huwa akiongea anajiona "smart" sana kuliko wasikilizaji, ila ktk wababaishaji no 1 ni huyo Jamaa.

Lingine kama upo karibu yake mwambie, aombe apewe wizara nyepesi. Hana ajuacho. Atatukana Kila mtu awamu hii.
 
Mtatumia kila njia kumsafisha.

ila ubovu wa makamba hasa suala la kukatika katika ovyo na mgao wa umeme hauhitaji elimu ya chuo kikuu kugundua kua jamaa Ni mbabaishaji au anatuhujumu kwa maksudi kabisa.
 
Shida ya Makamba Jr ni kutegemea siasa kuendesha maisha yake.
Lingine huwa akiongea anajiona "smart" sana kuliko wasikilizaji, ila ktk wababaishaji no 1 ni huyo Jamaa.
Lingine kama upo karibu yake mwambie, aombe apewe wizara nyepesi. Hana ajuacho. Atatukana Kila mtu awamu
Pumba. Unatumwa na waliotumbuliwa@. Jitafakari wewe kabla hajajitafakari.

Taadhali: Usiokote makopo jalalani ndugu, hohooo
 
kumekuwa na mfululizo wa threads za kumpondea Makamba kila uchao.......!

Akijikwaa basi inafunguliwa thread hasi dhidi yake;
Akikohoa basi inafunguliwa thread hasi dhidi yake;
Akisalimia basi inafunguliwa thread hasi dhidi yake;
Akisalimia hali hiyohiyo;
Akitoa zawadi, km wanavyofanya wengine ambao walikuwa wanagawa mpaka hela, hali hiyohiyo;
Akikaa kimya hali hiyohiyo;

Threads zote hizi, zinakuwa na shutuma moja au mbili tu kuu; MAKAMBA MWIZI NA ALIFELI KIDATO CHANNE ingawa kuna ulazimishaji wa nyingine pia kuwa eti ANAMSEMA MAREHEMU JPM! Cha kuchekesha, threads zote hizo hakuna hata moja inayotoa ushahidi wa huo wizi na huko kufeli kwake. Na cha kuchekesha zaidi ni kuwa baadhi ya wanaotoa shutuma hizo wamefeli vibaya, katika elimu hadi maisha, na ushahidi wa kufeli kwao upo wazi kabisa kuliko huyo Makamba.

Hili jambo, kwa jicho la tatu, linafikirisha sana.......kwa hakika hapa kuna kitu si bure hii.....labda uwe poyoyo ndo hutoona kuwa kuna jambo la hila limejificha hapa!

Yule musiba alipokuwa anakesha na kuwezeshwa vizuri kumtukana Makamba huyu, alijibu kidogo tu lkn kwa ufasaha kabisa kuwa, 'Siwezi kujibizana na mjinga!'

Juzi hapa kawajibu kidogo tu hawa wachambaji wa mitandaoni kuwa wasilete upuuzi wao, basi wamejifanya kubadili gia na kulipeleka jibu hilo kwa kamati ya bunge wakiamini litamuathiri zaidi na mamia ya threads sasa yanafunguliwa kwa ajili hiyo.

Unless proved otherwise, nitaendelea kuuona usmart wa Makamba vizuri kabisa katika nafasi ya uongozi alionao na hata kuzidi hiyo!!
Sawa bwana makamba
 
Makamba blah blah na confidence za ovyo kwenye media Ni nyingi mno ila kiuhalisia utendaji wake Ni sifuri,

Ameturudisha nyuma Sana kimaendeleo hasa upande wa umeme, Upuuz wa mgao,majenereta na kukatika katika ovyo kwa umeme tulishaanza kusahau kabisa watanzania[emoji3525]
 
Shida ya Makamba Jr ni kutegemea siasa kuendesha maisha yake.
Lingine huwa akiongea anajiona "smart" sana kuliko wasikilizaji, ila ktk wababaishaji no 1 ni huyo Jamaa.
Lingine kama upo karibu yake mwambie, aombe apewe wizara nyepesi. Hana ajuacho. Atatukana Kila mtu awamu hii.
Makamba

wizara ya mazingira na muungano alifanya vizur Sana, huku kwenye wizara zinazogusa maisha ya wengi na zenye changamoto Sana ameprove failure sana, haziwezi kabisa.

Kuna kipindi flan tulidhan angeweza kua presidential material, ila Hii wizara ya nishati imemshushia credibility mno.
 
Mtatumia kila njia kumsafisha
ila ubovu wa makamba hasa suala la kukatika katika ovyo na mgao wa umeme hauhitaji elimu ya chuo kikuu kugundua kua jamaa Ni mbabaishaji au anatuhujumu kwa maksudi kabisa.
Yani afanye hujuma Halafu tiss wanamuangalia tu ! Mkuu labda hujui gvt coordination inavyofanya kazi kila waziri na wizara kuna nyoka maalumu wanaoripoti kwà mama direct kila kitu sasa hiyo hujuma anaifanyia wapi?
 
Kingine suala la makamba kuona kila anayemkosoa anatamani uwaziri wake anakua anakosea sana, Ni immaturity ya Hali ya juu mno kisiasa na kiuongozi.

Anatuonesha watz kua kumbe akili yake keshaiset kua uwaziri kwake Ni ulaji na sio kuhudumia watu.

Anajitia ujuaji mwingi ilhali anazidi kukosea kila kukicha,

Suala la umeme kuakatika katika hajalimaliza, keshahamia kwenye matumizi ya gesi kama nishati, bila kujua kipato Cha watanzania waliowengi kuafford gesi Ni mtihani maana bei iko juu mno.

Anajificha kwenye kivuli utunzaji wa mazingira kila anapokwenda na makamera utadhani amekua waziri wa mazingira
 
Yani afanye hujuma Halafu tiss wanamuangalia tu ! Mkuu labda hujui gvt coordination inavyofanya kazi kila waziri na wizara kuna nyoka maalumu wanaoripoti kwà mama direct kila kitu sasa hiyo hujuma anaifanyia wapi?
Hiyo Government Cordination ilikuwepo tangia EPA? anzia enzi za RADA? RICHMOND? IPTL? au imeanza juzi?
 
Back
Top Bottom