Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 26,483
- 40,130
VIDEO: Wananchi wa Venezuela wakishangilia anguko la Maduro na genge lake madarakani
Great Thinkers, nawakaribisha tuchambue tukio la kukamatwa rais Nicholaus Mafuro wa Venezuela
- Marekani akikutaka atakunyakua tu hata kama Uwe na Ulinzi mkali kiasi gani, yeye atakutwaa tu akikutaka.
- Ushirika na nchi za Kikomunisti kama China,Urusi,Korea Kaskazini nk haukusaidii kitu kama Marekani akikutaka.
- Urusi na China nao pia wanajali mitikasi yao ndo maana mnaweza ingia makubaliano kibao lakini siku wanaoitwa “Mabeberu” akiwemo USA wakiwa na jambo na wewe hautawaona tena.
- Rais wa Venezuela alikuwa ni Rais anayelindwa zaidi kwa Bara la Amerika ya Kusini na Caribbean lakini Marekani wametumia Dk 124 (Saa mbili na dk 4) kutua Ikulu ya Venezuela na Kumnyakua Maduro na Mke wake.
- Kikosi cha Ulinzi wa Rais Maduro kina vifaa kama Drone aina ya Mahojer 2/4 zinaweza kufanya upelelezi 24 hrs na kutuma taarifa Ikulu moja kwa moja, kina drone Za wing Loong ambazo zinazuia na kukwema makombora,mahari ya Urusi yasiyopitisha Risasi, ndege zisizopitisha risasi na zinaweza kukwepa makombora. Lakini USA wamemtwaa Chap tu.
- Marekani walikuwa wana mshutumu Rais Maduro kwa ukandamizaji wa haki Za binadamu, ila yeye akasema wanatamani mafuta yake. Wamemunyakua!
- Serikali ya Maduro inatajwa kuteka, kuua na kulawiti Wakosoaji wake, lakini serikali ikasema Mabeberu wanataka Rasilimali Maduro huko Orinoco Belt. Wamemtwaa!
- Marekani wakikukamia basi hata hawajitaji njia ndefu kama ambavyo wengi wanasema, ila anakuja mzima mzima muonyeshane makali.
- Mataifa ambayo yanakiuka haki Za raia, na kuteka wakosoaji wake basi yanatukia neno “wanatamani Rasilimali zetu” kama kichaka cha kujificha. Yamemkuta Nicolas Maduro!!
- Marekani wameingia Caracas wakakata umeme jiji zima, wakazichapa Kambi Za kijeshi Za Venezuela kisha wakamchukua Maduro waliyekuwa wanamtuhumu kuwa Mshirika wa kundi la kuuza dawa Za kulevya ja linalofanya Uhalifu la Cartel de los Soles ( cartel of the Sun).
👉🏻Je Marekani anasaidia au ana maslahi binafsi na nchi zenye Rasilimali?
Karibu Tuchambue