Tafakuri na Kandaka binti wa ardhi ys Nubia, Tanzania imekataa

Hekari

Member
Joined
Jul 3, 2021
Posts
8
Reaction score
10
Hali ya ukungu na baridi kiasi ulioitawala June 6 2019 haikuzuia misafara isiyoisha ya magari ya jeshi katika mji wa khartoum. na kila walipopita nyuma waliacha miili ya mamia ya raia imelala katika Kila Kona ya mji huo ikiwa imeondokewa na baraka ya uhai. Hapa wananchi wakaanza kuiona adha ya Ile sauti tamu na maridhawa ya binti alaa salah.

Na hata siku zilivyozidi kwenda akapotea kabisa katika mboni za macho yao wasijue kapitia uchochoro gani kukimbia matatizo yaliyokuwa yanaikabili Sudan siku Hadi siku.

Miezi michache kabla ya machungu hayo binti mmoja mwenye Haiba Ta nehesi anaonekana juu ya paa la gari akiwa amevalia mavazi meupe na blauzi nyeusi huku umati wa watu ukiwa umemzunguka naye hakufanya ajizi aliendelea kuwaburudisha Kwa sauti yake murua iliyokuwa ikihamasisha ukombozi, aliendelea kuhama mashairi baada ya mashairi yote yakihamasisha ukombozi wa Sudan dhidi ya utawala uliokomaa Kwa miaka 30 wa OMAR HASSAN AL BASHIR. ambae mnamo December 2018 chini ya serikali ya kulishihudiwa mfumuko wa bei Sudan hasa kupanda Kwa gharama za mafuta na vyakula.

Wanafunzi, wafanyakazi na wananchi wa kawaida waliendelea kuandamana Kila panapokucha kwenye mitaa wakidai mabadiliko hapa ndipo jina la mwanadada alaa salah binti wa miaka 22 tu Kwa kipindi kile Tena akiwa mwanafunzi wa chuo na architect mtarajiwa. Alikuwa alama muhimu Kwa mapinduzi ya sudani akiwa katika msitari wa mbele katika maandamano ya kupinga utawala wa OMAR HASSAN AL BASHIR. Na hapa ndipo alipopachikwa jina la kandaka wakimfananisha na malkia wa kabila ya kush katika historia ya zaman ya sudani

1000008722.jpg

"Alaa salah akiwa katikati ya waandamanaji katika mji wa khartoum huku akiongoza wimbo maarufu wa mapinduzi Kwa wakati huo ""thawra"

Maandamano yaliendelea kuutikisa mji wa khartoum Kila panapokucha na hali ikazidi kumuelemea HASSAN AL BASHIR. Mamia Kwa maelfu waliendelea kujitokeza barabarani wakihanikiza raisi atoke madarakani maandamano ambayo yaliendelea Hadi kufikia mwaka 2019.

Mnamo April 6 2019 siku ambayo ni siku ya kumbukumbu ya mapinduzi ya mtawala nimeiri yaliyofanyika 1985. Siku hii ilikuwa ni siku ya kipekee watu wote wakiita siku ya ukombozi wa sudani. Watu waliandmana Kwa juhudi kubwa huku mwanadada kandaka aliendelea kupita na upepo wa umaarufu aliendelea kuimba shairi lake maarufu " I was raised to love our home....... Fighting for bread are fighting for freedom.

Baada ya maandamano kuwa makubwa hatimaye vikosi vya jeshi vikiongozwa na Ahmed awad ibn Auf likaona isiwe tabu jion ya tar 11 April 2019 wakaamua kumpiga chini HASSAN AL BASHIR na kuunda serikali ya mpito ya kijeshi ambayo ilikuwa chini ya Gen. Abdel Fattah al-Burhan.

Machafuko yalitulia Kwa muda lakini ni kama hawakuwa wanyonge wakakusanya nguvu Tena baada ya Kuona mambo hayaendi chini ya serikali ya mpito ya kijeshi, basi 6 June 2019 wakaamua kurudi barabarani lakini hwakuamini macho yao kwani hawakuwa wakipambana na BASHIR Tena bali wanapingana serikali ya kijeshi hapo ndipo waliposhuhudia wakipungua mmoja baada ya mwingne kw mirindimo ya risasi, khartoum ikawa haikaliki ni kama walikaribisha jini la machafuko hivi Kwa kujidai Wana mapinduzi Hadi Leo hii hali si sawia Hadi viwanja vya mpira vinageuka viwanja vya vita( uwanja wa Al hilal Omdurman).

Miaka ikapita na siku zikaenda Sudan ikawa chaka la Vita na migogoro ya kisiasa na kuondolewa miongoni mwa nchi wanachama wa UN. Watu wakabaki kujiuliza yuwapi shujaa ALAA SALAH kandaka binti wa ardhi ya Nubia?.

Wakati natafakari kupotea Kwa alaa salah binti wa Nubia na kuwaachia wenzake matatizo lukuki Kwa kivuli Cha mapindunzi mara naona ujumbe katika miongoni mwa mitandao ya kijamii ikihamasisha kuwa tupo wengi tutoke ikiwa imeambatana na picha za kikundi Cha watu kadhaa wakidai kutafuta uhuru wao wakanikimbusha 6 April wafuasi wa kandaka walipokuwa wakihamasisha mapinduzi kama kumbukumbu ya mapinduzi dhidi ya nimeiri ya 1985. Lakini nikaingiza gagaziko Kwa maswali haya

1. Mbna kandaka wetu hatumuoni barabarani akiwa anatuimbia na kutuhamasisha kama binti alaa salah?

2. Mapinduzi yakitokea yakatuletea hali ya ardhi ya Nubia je kandaka atakuwa hapa kuteseka na sisi ? Au ataendelea kupost wanae wakitunukiwa vyeti vya ubora kutoka shule Bora za taifa nambari one duniani?

3.if yatatokea ya Nubia je Kuna mwananchi wa kiwango Cha chini atanufaika? Je watoto wa ardhi hii ya mkwawa hawatakuwa wamefanikisha kumtafutia umaarufu kandaka aliyeko katika ardhi ya Franklin? Fighting for fame of others( Mary, Kim, hill new) as the formula.

4. Nisiwaze sana nitaumia ila nahisi vijana wa mkwawa wamekuwa waelewa hawatoki had wawaone wakina Ms. alaa salah wapo mbele.
 
View attachment 3513638

Mimi kama Kiranja wa jamii naamini kwamba na ninakuhakikishia hili; hawa unaowasema wameingilia kati tu agenda ya wananchi na kwa kifupi hawa ndio wanaoharibu

Wananchi wana mengi mioyoni mwao walipofikia hawakuhitaji msukomo wowote wa hawa kina binti sayuni! Kuja kwao mbele kumeharibu agenda ya wananchi
 
Ukweli ninkwamba raia wamechoka... msijipe moyo, na kadri siku zinakwenda hali itakuwa mbaya, kikubwa washaurini hao mabwana zenu wajue kula na vipofu, nchi hii sio ya elimu kuwa tabu, miundombinu kipengele, maji shida, afya matatizo, umeme wa tabu, ajira tatizo.. wakati serikali inatumia pesa vibaya na kibaya zaidi wanaiba sana.
Kama hawatobadilika ipo siku yatatokea makubwa zaidi ya yale ya 29th October..

KADRI UNAVYOMZINGUA PAKA, HUZIDI NYANYUA MKIA.
 
Back
Top Bottom