Yule wa kipindi kilee, aliyependa kusafiri kama Vasco da Gama aliungwa mkono na walioitwa wanamtandao.
Na yule aliyekuwa akipenda kazi na kuongea kwa kujiamini sana aliungwa mkono na abiria waliouchukia ufisadi. Japo baadaye huyu nahodha alibadilika na kuwa katili asiyeelezeka. Akachukiwa na watu wote wakiwemo wa boti yake mwenyewe.
Lakini huyu wa sasa anaungwa mkono na nani? Kwanza kaingia kwa bahati mbaya. Na siyo siri tena kwamba kundi kubwa ndani ya boti yake mwenyewe halikumtaka awe nahodha. Sababu zilizotolewa na kundi hili ni mbili...1. Udhaifu wa kijinsia 2. Anatoka upande wa wachache.
Salama yake ilikuwa ni kuungana na wale wengi waliokuwa wakikwazwa na ukatili na majivuno ya yule nahodha aliyetwaliwa. Lkn pia angepatana na manahodha wa boti shindani.
Haya yangemsaidi kuzima figisu za ndani ya boti yake. Na kumpa uimara ktk unahodha wake
Lakini kwa kuwa kaingia kwa bahati mbaya, hapendwi hata na wale wa boti yake mwenyewe na anarudia makosa ya nahodha aliyetwaliwa basi anajiweka kwenye hatari ya kushindwa kazi mapema sana.