Tafakuri: Ni upi hasa unyeti wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar?

Mtoa mada acha unafiki. Unahoji 'unyeti' wa Muungano wetu, wakati huo huo unajifanya kusema huna lengo la kuuvunja bali unataka 'kuuimarisha'. Unaweza kuimarisha kitu ambacho hata hujui 'unyeti' wake? Au hujui maana ya neno 'unyeti'?
Satu, naomba nikuulize swali moja tu...je muungano unaweza kudumu Wazanzibari wakiinyima kura CCM?
 
Satu, naomba nikuulize swali moja tu...je muungano unaweza kudumu Wazanzibari wakiinyima kura CCM?

Kabla sijakujibu, onesha kwanza rangi yako halisi. Unapenda Muungano uwepo na udumu? Kama unapenda Muungano uwepo, kwa nini unahoji 'unyeti' wake kama si mnafiki wewe?

Mimi napenda Muungano wetu na nataka udumu kwa sababu najua 'unyeti' wake.
 
Kwa inavyoonekana huu Muungano uliundwa kwasababu za kimaslahi ya usalama wa Tanganyika, maana Zanzibar iko karibu mno na Tanganyika hvyo Kama kusingekua na Muungano basi ingekua njia rahisi mno ya adui zetu kuingia Tanganyika...
Mtazamo wa kizamani huo usio na uhalisia. vipi mipaka ya nchi sehemu zingine, mbona kwa upande Kenya Mombasa imepakana na Pemba? Au mbona hatukauungana na Burundi au rwanda
 
Mtoa mada acha unafiki. Unahoji 'unyeti' wa Muungano wetu, wakati huo huo unajifanya kusema huna lengo la kuuvunja bali unataka 'kuuimarisha'. Unaweza kuimarisha kitu ambacho hata hujui 'unyeti' wake? Au hujui maana ya neno 'unyeti'?...
Mbona uingereza imejitoa EU?
 
Kwa inavyoonekana huu Muungano uliundwa kwasababu za kimaslahi ya usalama wa Tanganyika, maana Zanzibar iko karibu mno na Tanganyika hvyo Kama kusingekua na Muungano basi ingekua njia rahisi mno ya adui zetu kuingia Tanganyika...
Zanzibar na Kenya au Uganda ni ipi iko karibu? Zanzibar mapka upande boti lakini Kenya, Uganda etc unavuka kwa miguu. Hili suala la kusema adui ataitumia Zanzibar ni porojo tu. BTW siku hizi adui akitaka kukuvamia ni rahisi sana na siyo lazima ategemee kakisiwa kadogo kama Zanzibar.
 
Aliyeanzisha mchakato wa katiba mpya aliliona mapema hili. Lengo mojawapo liikuwa ni kuunusuru Muungano wenyewe hasa baada ya Maalim na Karume kukutana kule Zanzibar na kuunda katiba inayosema Zanzibar ni nchi wakadefine hadi mipaka ya nchi hiyo!

Lakini Magufuli alipoingia madarakani akagoma kuendelea na mchakato wa katiba mpya, matokeo yake Zimwi la kutoukubali Muungano limepewa nguvu mpya!

Serikali itambue tu kuwa Katiba ya mwaka 1977 hasa katika masuala ya muungano haitokidhi matakwa ya Wazanzibari, Na wataendelea kuukataa kwa maneno mpaka hapo watakapoamua kuukataa kwa vitendo!.

Kama tunautaka muungano, basi tuje na katibya mpya sasa hivi, tukijifanya tunafumba macho kisha tukadhani wale tunaowapandikiza Zanzibar tukitokea Dodoma wataulinda muungano kwa niaba yetu ipo siku tutaamka na kukuta maelfu ya Wazanzibar mitaani hawautaki huo muungano, utawafanya nini, utawapiga risasi? —Na muungano utaishia hapo!
 
Kabla sijakujibu, onesha kwanza rangi yako halisi. Unapenda Muungano uwepo na udumu? Kama unapenda Muungano uwepo, kwa nini unahoji 'unyeti' wake kama si mnafiki wewe?

Mimi napenda Muungano wetu na nataka udumu kwa sababu najua 'unyeti' wake.
Satu, Muungano kama ulivyo sasa ni wa kilaghai, ni wa hila na haupo kwa maslahi ya Watanzania wote bali kwa maslahi ya CCM. Kwa jinsi ulivyo, kama CCM haipo, muungano haupo, umekufa.

Satu, utakuwa na akili fupi sana kama hata hili unashindwa kuliona. Unajua kwa nini jeshi linapelekwa Unguja? Inapelekwa kwa sababu Wazanzibari hawaitaki CCM na dalili zipo za kushindwa.

Satu unaniita mnafiki kwa kutaka Muungano uimarishwe na nyufa zilizojitokeza zishughulikiwe. Unaponiita mnafiki sikushangai kwani hata kaswali kadogo sana umeshindwa kujibu, pole.

Satu, huu mjadala unakuzidi kimo.
 
Ngoja nikachukue jembe nikalime mihogo, hata siwaelewi
 
UK ipoje? Prime Minister wa UK ni nani?? Na wa England ni nani?? Na Bunge la UK ni Lipi na la England ni lipi ? Vs lile is Scotland , Ireland na Wales?
 
Chadema wametuletea mgombea wa Urais
 
Nini unyeti wa Muungano wa UK, USA n.k ukiujua huo utaujua unyeti wa Muungano wetu
 
Tunashukuru Mh Tundu Lissu ameweka wazi kila kitu.
Mkuu, fikiria sasa, ndiyo Sieph kashinda uraisi, na wazanzibari wakavunja muungano,
Nitajie faida moja tu ya Lisu atakayoipata kutokana na kuvunjika muungano,

Nitajie pia faida ya ACT itakayopata kutoka Zanzibar kuja huku bara ikiwa muungano utavunjwa

Na kisha unitajie manufaa ya Chadema yatayapatikana huku bara Baada ya kuvunjika muungano
 
Duuh, umepiga nyundo ya kisogo huyu ndugu...

Niliisoma comment yake hii 👇 👇
Kabla sijakujibu, onesha kwanza rangi yako halisi. Unapenda Muungano uwepo na udumu? Kama unapenda Muungano uwepo, kwa nini unahoji 'unyeti' wake kama si mnafiki wewe?

Mimi napenda Muungano wetu na nataka udumu kwa sababu najua 'unyeti' wake.

Kabla sijaijibu nikaamua kuona watu wengine watamjibu nini. Thank God kuwa, umemjibu vizuri sana na ni kweli kabisa mjadala huu hauwezi, umemzidi kimo kwa mbali sana huyu ndugu...

Kwanza hata hajui hata mahali pa kulitumia neno "mnafiki" au "unafiki". Anadhani linaweza kutumika popote wakati wowote...

Wewe unajaribu kueleza kasoro za muungano na namna ya kuzirekebisha, jamaa anakurupuka kutoka huko alikokuwa bila hata kusoma kwa makini ili kujua logic ya mjadala ndipo aseme/aandike lakini anaishia kusema tu;

" .....acha unafiki" something which is out of the context kabisa....!!

Duuh, MATAGA ni tatizo kwelikweli, wengi zaidi ya 99% ufahamu wao ni below standards....
 
Katiba ya Zanzibar inaruhu kura ya maoni kwa jambo kubwa kama hili ..siku akitangazwa Maalim Seif ajenda kuu ni hio. Nyinyi endeleeni kufuta chaguzi, muibe kura, muikalie Zanzibar kwa mtutu wa bunduki, muwachagulie rais Dodoma lakini siku mkijichanganya tu huu Muungano tunauvunja. HATUUTAKI HATA KUUSIKIA.
 
UK ipoje? Prime Minister wa UK ni nani?? Na wa England ni nani?? Na Bunge la UK ni Lipi na la England ni lipi ? Vs lile is Scotland , Ireland na Wales?

Nini unyeti wa Muungano wa UK, USA n.k ukiujua huo utaujua unyeti wa Muungano wetu
Ndugu yangu August, kwa kweli sikutegema hoja dhaifu kama hizi kutolewa na mtu kama wewe ambaye niliamini unao uelewa wa mambo kwa kiwango cha juu kuliko idadi kubwa ya vijana wa Lumumba walioko humu ndani...au nakosea? Katika utetezi wako unataja UK na unataja USA, are you serious kweli? UK haina Rais, kweli si kweli? USA ina Rais moja kweli si kweli? Tanzania inao Rais wawili, Makamu wa Rais wawili, Waziri wakuu wawili (kumbuka Zanzibar ina Waziri Kiongozi).

Je ndugu yangu August, umewahi kuzipitia Katiba za hizo nchi mbili unazozilinganisha na Tanzania? Hebu kuwa mkweli ndugu yangu, niliuliza swali sijapewa jibu lake hivyo nakupa nafasi unijibu, Je CCM ikikataliwa na kushindwa uchaguzi upande moja wa muungano, huo muungano utaendelea kuwepo? Katika hizo nchi ulizozitolea mfano, je kushindwa kwa chama kilicho madarakani kuna athari gani kwa muungano wao mpaka vyombo vya dola vitumike kulazimisha ushindi kwa chama tawala?
 
Mdogo mdogo tutafika tu
 
Bila muungano hakuna Chama cha Mapinduzi.

Chama cha Mapinduzi hutumika kuyaenzi mapinduzi ya serikali ya Sultani. No Zanzibar in the picture No CCM
Sultani hajawahi kuwa na serikali. Iliyovamiwa na kuangushwa ni serikali iliyokuwa ikiongozwa na Muhammed Shamte wa chama cha ZPPP. Mpemba wa Ole huyo
 
Sultani hajawahi kuwa na serikali. Iliyovamiwa na kuangushwa ni serikali iliyokuwa ikiongozwa na Muhammed Shamte wa chama cha ZPPP. Mpemba wa Ole huyo
Sultani alikuwa kiongozi wa nchi
Mohammed Shamte alikuwa kiongozi wa serikali.
 
Siku ukivunjika ndo utajua km una umuhimu au laaa!
 
Hao maadui ambao wataweza kuitumia Zanzibar kuivamia Tanganyika ni kina nani? Mbona hawatajwi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…