Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 5,119
- 4,569
Moja ya sera ambayo imekuwa ikipigiwa kelele na kambi ya Tundu Lissu ni ya kuweka muda wa ukomo wa viongozi wa chama cha siasa cha chadema. Kwamba kiwe ni vipindi vya miaka mitano mitano vizivyozidi viwili.
Ukiitafakari sera hiyo utagundua kuwa kiuhalisia wenye umri kama wa Tundu Lissu, sera hiyo haiwahusu kwani baada ya vipindi hivyo viwili watakuwa wana umri wa miaka 70 au zaidi na hivyo kutokuwa na nguvu kimwili za kuhimili misukosuko ya kuongoza siasa za upinzani.
Vipaji vya uongozi mara nyingi huanza kujitokeza na kujengeka kwenye umri wa ujana. Kwa mfano Mwalimu Nyerere alianza kuwa Mwenyekiti wa chama cha TANU akiwa na umri wa miaka 32 mwaka 1952 na kufanikisha tukapata uhuru kutoka kwenye makucha ya mkoloni. Baada ya hapo aliendelea kuwa Mwenyekiti wa chama hicho kilichobadili jina baadaye kuwa CCM (1977) kwa muda wa miaka mingine 28 zaidi hadi alipoamua kustaafu uenyekiti mwaka 1990 akiwa na umri wa miaka 68 kwa sababu ya uzee.
Sasa chukulia kijana wa CHADEMA kama Pambalu akachaguliwa leo kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA akiwa na umri wa miaka 30. Akakiongoza cha hicho vizuri sana kuliko hata watangulizi wake. Baada ya miaka mitano akachaguliwa tena kwa muhula wa pili.
Akafanya vizuri zaidi na kukifanya chama kubakiza sentimita chache kushika dola, atalazimika kwa sheria hii ya Tundu (aka tundulism) kuachia ngazi akiwa na umri wa miaka 40 tu. Kipaji chake cha uongozi kitakuwa kipigwa spana badala ya kukiendeleza.
Itabidi akakahangaike kutafute kazi ya aina nyingine katika umri huo mdogo. Tumeshuhudia jinsi sera ya aina hiyo ilivyopiga spana kipaji cha uongozi cha Zitto Kabwe kwenye umri huo mdogo. Nyota yake imezimwa na sera hiyo, hata ubunge wa Kigoma ni ngumu tena kuupata.
Vijana kuweni makini na mkatae kata kata hiyo tundulism policy.