Tafakuri yangu: Kifo cha Job Ndugai ( Spika Mstaafu)

Kila jambo lina mwanzo wa nyakati na lina mwisho pia.. Mwanzo unaweza kuwa mwema sana.. Chunga sana mwisho usije ukawa mbaya
Na mara nyingi ukiwa na mwanzo mzuri,ukasosa nguvu ya kiroho ya kupambanua mambo positively tegemea kuwa na mwisho mbaya.
 
Duh..!
Kwa hali hii bora Yesu arudi aisee Dunia haina usawa kabisa!
 
Aione Lucas Mwashambwa kwenye jalada tafadhali.
 
Asante sana Mshana....Naliona andiko ili ni moja ya maandiko bora sana duniani.....asante sana kwa maneno ya Hekima
 
Asante sana Mshana....Naliona andiko ili ni moja ya maandiko bora sana duniani.....asante sana kwa maneno ya Hekima
Sanaaa, mwamba yupo vizuri.
Nina swali kwa Mshana. Wewe ni mwandishi na mchambuzi mzuri TU wa mambo anuai. Unafikiri ni andiko Gani au uchambuzi Gani unaodhani kwako ulikuwa Bora zaidi na ulioweka rekodi, ili niupitie. I'm very serious
 
Anna Tibaijuka

@AnnaTibaijuka.

32m

Spika Ndugai. Tunaokufahamu tunakulilia kwa WEMA WAKO. RIP. Familia. Poleni. Suala la Lissu kufukuzwa Bungeni liliniuma sana. Jioni nikamfuata Spika Ndugai nyumbani kwake Kisasa kumuuliza kulikoni? Mwenzetu wote tunajua yaliyompata?. Utasemaje hujui alipo? Spika akanieleza kwa utulivu yafuatayo ambayo IN HIS TRIBUTE (kama heshima kwake) ninayaweka wazi. Labda yatasaidia kumuelewa kwa waliokerwa na kauli zake za mizaha (dry humor).

Ndugai aliniambia "Mama ni Maelekezo. Mimi nilichofanya kama Spika ni kujaribu kuokoa maisha yake kwa kumkimbiza Nairobi kutibiwa. Wengine walitaka apelekwe Muhimbili. Hatukuwa na bajeti. CHADEMA hawakuwa na fedha kulipia ndege. Nikamuomba Mbunge wa CCM mhe Turku (RIP) alipie tutamrefund". Akaendelea "Mama Lissu ni mwanasiasa. Akipona atarejea kupambana kadri Mungu atakavyomjalia. Kwa sasa ninakuwa na tahadhari kusurvive katika siasa ngumu za maelekezo huku naongoza muhimili".

Sikuwa na la kusema zaidi. Nikajua tuna safari ndefu kama taifa. Jamii haitaki kuangalia misingi ya matatizo yetu kimfumo. Tunabaki kulaumu viongozi (personalities) kana kwamba wana freedom kutekeleza majukumu yao. Mfano Utakuta mbunge analaumiwa kwa kutojenga shule, hospitali, barabara. Kwani hiyo si kazi ya Serikali kuu na Halmashauri wanaotoza kodi? Tusimlaumu Ndugai kwa mambo yaliyokuwa ya mfumo. Alipokosea Mungu amsamehe lakini kuna mazuri Mengi alifanya. Apumzike kwa amani.
 
Sanaaa, mwamba yupo vizuri.
Nina swali kwa Mshana. Wewe ni mwandishi na mchambuzi mzuri TU wa mambo anuai. Unafikiri ni andiko Gani au uchambuzi Gani unaodhani kwako ulikuwa Bora zaidi na ulioweka rekodi, ili niupitie. I'm very serious
Asante Sana lakini kwakweli sijawahi kufuatilia maana nimeandika sana
 
......Mwambie Prof. Tibaijuka ninampenda sana...lakini sitaki kukubali ASEME KWA NIABA YA JOB Kipindi hiki....Hakuumizwa TAL peke yake...Tumeumia wengi......Alitakiwa ajitetee yeye mwenyewe.....Au angejiudhulu.....Badala yake amepiga watu bakola na kuonga ili arudi madarakani....
 
Mama Samia Aangalie Sana suala la Wahuni Amsikilize Polepole na Aongoze Nchi Kama Rais Mwenye Mamlaka Kamili.
 
Mshana Jr andiko lako lime nikumbusha mbali sana miaka 18 nyuma nilibanwa na appendix nikawahishwa hospital usiku wa manane kwenye ile ward tulikuwa tunalala wawili, wawili kwenye kitanda kimoja...bedmate wangu nilimkuta ana hali nzuri kimuonekano wa nje...ila mimi watu wote ndani ya ile ward walijua muda sio mrefu nitakufa😭😭😭😭

Baada ya muda niliishiwa nguvu, nikapoteza fahamu nilikuja kushituka siku ya tatu mbele, kwenye kitanda change nikiwa peke yangu bila yule mgonjwa mwingine...!

Baadae nilipata taarifa kuwa yule mgonjwa alifariki kwa alikuwa anasubiri ndugu zake wachangishe pesa...ili afanyiwe upasuaji kwani alioza utumbo...!

Hakuna msiba uliniuma roho kama wa huyo jamaa...pesa ilisababisha akakosa huduma...tena akiwa teyari yupo hospitalini😭😭😭😭

Sijui Mungu alikuwa na kazi gani na mimi hadi nikapona siku ile...kwani hata mimi nilikichungulia kifo...isingekuwa status ya mzazi wangu kwenye ile jamii sijui ingekuwaje...!​
 
Wengi wameangamia kimwili na kiroho kwa kuziseta, kuzifharau, kuzidhihaki na kuzitendea vibaya hizi tunu mbili takatifu mbele za macho ya Mungu wetu

Kuna wakati wafao huwa hata na habari kuwa wamekufa hasa wale ambao huishi kimwili zaidi ya kiroho!

Lakini daima usishindwe na ubaya! Bali ushinde ubaya kwa mema!
Pumzika Job Ndugai ama iishi karma yako katika uhai wako mpya nje ya mwili uharibikao!

Wakati si milele❗

(6,794) Gharama matibabu Ndugai yazua jambo. Alitumia zaidi ya Dola Milioni 12 | JamiiForums Gharama matibabu Ndugai yazua jambo. Alitumia zaidi ya Dola Milioni 12

Kuna ishara za kiroho wanaoneshwa lakini hawazioni

Nimefurahi umerudi kihivi na haya,ksa kutupa ujumbe nje ya kilicho tokea Ali itusaidie maishani mwetu pia.

Naomba ufafanuzi wa haya moja baada ya ingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…