Tafakuri yangu kwa Mashtaka ya Ole Sabaya

Aliyokuwa anafanya sabaya yanaakisi aliyokuwa anafanya bosi wake aliyemteua.
Mungu akasikia kilio cha watesi hao na kwa kuwa kulikuwa hakuna mamlaka ya kumtumbua jiwe (bunge lilikuwa linamuogopa) Mungu baba mwenyewe akaona heri amtumbue mwenyewe
Ukweli ni kwamba Magufuli alikuwa katili kama huyo sabaya
LIFUGUMA haaaaaa!!!!!!.
 
Sasa ni dhahiri kuwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya ameshtakiwa kwa makosa ya jinai. Amefikishwa Mahakamani huko Arusha na kusomewa mashtaka sita. Ninaandika hapa nikiamini kuwa mashtaka ya Ole Sabaya bado ni tuhuma tu hadi pale yatakapothibitishwa mahakamani kupitia ushahidi. Yaani, ukweli au la kuhusu mashtaka yake utapatikana mahakamani. Sitarajii tena Mkurugenzi wa Mashtaka kuwasilisha Hati ya Kutokuwa na Nia ya Kushtaki kama alivyofanya kwenye kesi ya Sabaya iliyopita (natania).

Kimsingi, makosa katika mashtaka yote dhidi ya Sabaya yanadaiwa kufanywa naye wakati akiwa Mkuu wa Wilaya ya Hai. Hapa ndipo tafakari yangu inapoanzia. Bila hata ufahamu wa kisheria, inafahamika kuwa Mkuu wa Wilaya pamoja na mambo mwngine ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama katika Wilaya yake. Ndiyo kusema, Mkuu wa Wilaya ndiye mlinzi kiongozi wa amani na utulivu katika Wilaya yake. Ndiye anayepaswa kuhakikisha kuwa wananchi wa Wilaya yake wanaishi kwa amani huku wakifanya shughuli zao za kimaendeleo katika kujitafutia mikate yao ya kila siku.

Haitarajiwi kuona Mkuu wa Wilaya 'akiwa kinara' wa uharibifu wa amani, utulivu na ustawi wa watu wake. Haitarajiwi pia kuona Mkuu wa Wilaya kutenda makosa ya jinai ambaye yeye mwenyewe ndiye anapambana nayo usiku na mchana ili wananchi wake wawe na amani, utulivu na ustawi. Haitarajiwi pia Mkuu wa Wilaya kutenda uhalifu ikizingatiwa pia yeye ni mwakilishi wa Rais katika Wilaya yake. Matendo yake na maneno yake yanawakilisha maono, maelekezo na taswira ya mamlaka yake ya uteuzi. HAIPENDEZI Mamlaka ya uteuzi kubeba taswira ya kijinai kwa wananchi kupitia kwa Mkuu wa Wilaya.

NI PICHA YA KUOGOFYA kuona Mkuu wa Wilaya akipokea rushwa; akitakatisha pesa; akiongoza genge la kihalifu na kadhalika. NI MAMBO YA KUTISHA kusikia au kushuhudia Mkuu wa Wilaya akikandamiza ustawi wa watu wake na kulinda kwa nguvu zake zote 'genge' lake. Tuhuma dhidi ya Sabaya zinatoa picha ya kujisahau au kujiachia kulikopitiliza kwa wateule. Au tuhuma hizo zinaonyesha jinsi tabia halisi ya mteule inapojianika pale ambapo kunapatikana nafasi ya kufanya chochote mahali popote. Mashtaka yote ni ya Arusha, bado ya mahali pengine ikiwemo Wilaya yake ya Hai. Inafikirisha sana.

Mashtaka ya Sabaya yawe funzo kwa Mamlaka ya Uteuzi. Yawe funzo katika vya kuzingatia kabla, wakati na baada ya uteuzi. Mamlaka ya uteuzi ina mikono mirefu. Ina vyombo mbalimbali vya kiuchunguzi na kiutafiti. Inafurahisha na kuleta imani na amani kwa wananchi kuona Mamlaka ya Uteuzi ikifanya kazi kubwa kuchuja wateule wake ili 'makandokando' kama ya Ole Sabaya yaepukwe. Hata kama mashtaka yote hayatathibitishwa mahakamani, kutuhumiwa tu kama kiongozi inatosha kuchafua picha ya mteule yeyote yule awaye. Kila jambo hutokea ili kutoa mafundisho kwa yajayo.
Kwa kuwa uongozi katika nchi masikini ni unatumika kama njia ya kujipatia utajiri, siyo rahisi kutenganisha viongozi wote na uovu dhidi ya wananchi.
Wakati mwingine kunakuwepo organized crimes kupitia vyama na hata serikali.
Hali inakuwa mbaya zaidi wanapokwepo viongozi wenye msimamo mkali(extremist).
 
Sasa ni dhahiri kuwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya ameshtakiwa kwa makosa ya jinai. Amefikishwa Mahakamani huko Arusha na kusomewa mashtaka sita. Ninaandika hapa nikiamini kuwa mashtaka ya Ole Sabaya bado ni tuhuma tu hadi pale yatakapothibitishwa mahakamani kupitia ushahidi. Yaani, ukweli au la kuhusu mashtaka yake utapatikana mahakamani. Sitarajii tena Mkurugenzi wa Mashtaka kuwasilisha Hati ya Kutokuwa na Nia ya Kushtaki kama alivyofanya kwenye kesi ya Sabaya iliyopita (natania).

Kimsingi, makosa katika mashtaka yote dhidi ya Sabaya yanadaiwa kufanywa naye wakati akiwa Mkuu wa Wilaya ya Hai. Hapa ndipo tafakari yangu inapoanzia. Bila hata ufahamu wa kisheria, inafahamika kuwa Mkuu wa Wilaya pamoja na mambo mwngine ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama katika Wilaya yake. Ndiyo kusema, Mkuu wa Wilaya ndiye mlinzi kiongozi wa amani na utulivu katika Wilaya yake. Ndiye anayepaswa kuhakikisha kuwa wananchi wa Wilaya yake wanaishi kwa amani huku wakifanya shughuli zao za kimaendeleo katika kujitafutia mikate yao ya kila siku.

Haitarajiwi kuona Mkuu wa Wilaya 'akiwa kinara' wa uharibifu wa amani, utulivu na ustawi wa watu wake. Haitarajiwi pia kuona Mkuu wa Wilaya kutenda makosa ya jinai ambaye yeye mwenyewe ndiye anapambana nayo usiku na mchana ili wananchi wake wawe na amani, utulivu na ustawi. Haitarajiwi pia Mkuu wa Wilaya kutenda uhalifu ikizingatiwa pia yeye ni mwakilishi wa Rais katika Wilaya yake. Matendo yake na maneno yake yanawakilisha maono, maelekezo na taswira ya mamlaka yake ya uteuzi. HAIPENDEZI Mamlaka ya uteuzi kubeba taswira ya kijinai kwa wananchi kupitia kwa Mkuu wa Wilaya.

NI PICHA YA KUOGOFYA kuona Mkuu wa Wilaya akipokea rushwa; akitakatisha pesa; akiongoza genge la kihalifu na kadhalika. NI MAMBO YA KUTISHA kusikia au kushuhudia Mkuu wa Wilaya akikandamiza ustawi wa watu wake na kulinda kwa nguvu zake zote 'genge' lake. Tuhuma dhidi ya Sabaya zinatoa picha ya kujisahau au kujiachia kulikopitiliza kwa wateule. Au tuhuma hizo zinaonyesha jinsi tabia halisi ya mteule inapojianika pale ambapo kunapatikana nafasi ya kufanya chochote mahali popote. Mashtaka yote ni ya Arusha, bado ya mahali pengine ikiwemo Wilaya yake ya Hai. Inafikirisha sana.

Mashtaka ya Sabaya yawe funzo kwa Mamlaka ya Uteuzi. Yawe funzo katika vya kuzingatia kabla, wakati na baada ya uteuzi. Mamlaka ya uteuzi ina mikono mirefu. Ina vyombo mbalimbali vya kiuchunguzi na kiutafiti. Inafurahisha na kuleta imani na amani kwa wananchi kuona Mamlaka ya Uteuzi ikifanya kazi kubwa kuchuja wateule wake ili 'makandokando' kama ya Ole Sabaya yaepukwe. Hata kama mashtaka yote hayatathibitishwa mahakamani, kutuhumiwa tu kama kiongozi inatosha kuchafua picha ya mteule yeyote yule awaye. Kila jambo hutokea ili kutoa mafundisho kwa yajayo.
Nyie sindio mlikuwa mnamsifia kwa kila kitu dikteta magufuli,,

Kipindi kile watu wanasema Sabaya Ni jambazi we ukawa kinara wakutetea hapa
 
Sikufahamu mkuu na sina maana ya kukudharau kuhusu ulimwengu wa sheria, nilicho taka ukijue tu kwamba, mleta UZI sio kilaza, ni expert wa sheria za BONGO and hence anajua ni kwanini kauleta huo uzi humu.
Kwani mimi nimesema mleta mada ni kilaza? au hukuielewa comment yangu? mleta mada nimemsoma sana humu jf na ninaweza kua na idea na anachokiandika humu,ile comment yangu kwanza haikumlenga mleta mada wa hii thd,comment yangu ilikua ni general.
 
Mh. Wakili msomi, Sabaya alikua mkuu wa wilaya Hai, ambapo anatoka aliye kuwa kiongozi wa kambi rasimi ya upinzani bungeni, na mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani! Kiongozi huyo wa upinzani alisha pewa kiapo na spika kuwa hatarudi bungeni, mkuu wa polisi wilaya aliapa hivyo hivyo!
Itoshe tu kusema kwamba ufurukunyu na ufinyokole wote wa mkuu wa wilaya, Una akisi unyumbirisi wote wa watawala wa awamu iliyo pita!
 
Sasa ni dhahiri kuwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya ameshtakiwa kwa makosa ya jinai. Amefikishwa Mahakamani huko Arusha na kusomewa mashtaka sita. Ninaandika hapa nikiamini kuwa mashtaka ya Ole Sabaya bado ni tuhuma tu hadi pale yatakapothibitishwa mahakamani kupitia ushahidi. Yaani, ukweli au la kuhusu mashtaka yake utapatikana mahakamani. Sitarajii tena Mkurugenzi wa Mashtaka kuwasilisha Hati ya Kutokuwa na Nia ya Kushtaki kama alivyofanya kwenye kesi ya Sabaya iliyopita (natania).

Kimsingi, makosa katika mashtaka yote dhidi ya Sabaya yanadaiwa kufanywa naye wakati akiwa Mkuu wa Wilaya ya Hai. Hapa ndipo tafakari yangu inapoanzia. Bila hata ufahamu wa kisheria, inafahamika kuwa Mkuu wa Wilaya pamoja na mambo mwngine ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama katika Wilaya yake. Ndiyo kusema, Mkuu wa Wilaya ndiye mlinzi kiongozi wa amani na utulivu katika Wilaya yake. Ndiye anayepaswa kuhakikisha kuwa wananchi wa Wilaya yake wanaishi kwa amani huku wakifanya shughuli zao za kimaendeleo katika kujitafutia mikate yao ya kila siku.

Haitarajiwi kuona Mkuu wa Wilaya 'akiwa kinara' wa uharibifu wa amani, utulivu na ustawi wa watu wake. Haitarajiwi pia kuona Mkuu wa Wilaya kutenda makosa ya jinai ambaye yeye mwenyewe ndiye anapambana nayo usiku na mchana ili wananchi wake wawe na amani, utulivu na ustawi. Haitarajiwi pia Mkuu wa Wilaya kutenda uhalifu ikizingatiwa pia yeye ni mwakilishi wa Rais katika Wilaya yake. Matendo yake na maneno yake yanawakilisha maono, maelekezo na taswira ya mamlaka yake ya uteuzi. HAIPENDEZI Mamlaka ya uteuzi kubeba taswira ya kijinai kwa wananchi kupitia kwa Mkuu wa Wilaya.

NI PICHA YA KUOGOFYA kuona Mkuu wa Wilaya akipokea rushwa; akitakatisha pesa; akiongoza genge la kihalifu na kadhalika. NI MAMBO YA KUTISHA kusikia au kushuhudia Mkuu wa Wilaya akikandamiza ustawi wa watu wake na kulinda kwa nguvu zake zote 'genge' lake. Tuhuma dhidi ya Sabaya zinatoa picha ya kujisahau au kujiachia kulikopitiliza kwa wateule. Au tuhuma hizo zinaonyesha jinsi tabia halisi ya mteule inapojianika pale ambapo kunapatikana nafasi ya kufanya chochote mahali popote. Mashtaka yote ni ya Arusha, bado ya mahali pengine ikiwemo Wilaya yake ya Hai. Inafikirisha sana.

Mashtaka ya Sabaya yawe funzo kwa Mamlaka ya Uteuzi. Yawe funzo katika vya kuzingatia kabla, wakati na baada ya uteuzi. Mamlaka ya uteuzi ina mikono mirefu. Ina vyombo mbalimbali vya kiuchunguzi na kiutafiti. Inafurahisha na kuleta imani na amani kwa wananchi kuona Mamlaka ya Uteuzi ikifanya kazi kubwa kuchuja wateule wake ili 'makandokando' kama ya Ole Sabaya yaepukwe. Hata kama mashtaka yote hayatathibitishwa mahakamani, kutuhumiwa tu kama kiongozi inatosha kuchafua picha ya mteule yeyote yule awaye. Kila jambo hutokea ili kutoa mafundisho kwa yajayo.
Magufuli alikuwa Ibilisi na Sabaya ndiyo kielelezo halisi cha roho yake ilivyokuwa. Ilikuwa lazima Mwendazake afe tu maana kama vigezo vyake vya kiongozi bora ni watu kama Ole Sabaya, Paul Makonda, Albert Chalamila na Gelasus Byakwana sijui nchi yetu ingekuwaje kwa miaka mingine 5.

Tujipige kifua mara 3 na tuseme "ASANTE MUNGU KWA KUTUKOMBOA KUTOKA KWA IBILISI"
 
Mkuu, unamfahamu vizuri mleta UZI!? Ni wakili mwandamizi wa mahakama kuu na mahakama ya rufaa so unachangia uzi wa proffesinal au expert wa sheria za bongo. Msome kwenye nyuzi zingine
Ila enzi ya mwanakwendazake kuna wakati alijutoaga ufahamu, katika kusaka teuzi! Credit kwake, amejirudi!
 
Sasa ni dhahiri kuwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya ameshtakiwa kwa makosa ya jinai. Amefikishwa Mahakamani huko Arusha na kusomewa mashtaka sita. Ninaandika hapa nikiamini kuwa mashtaka ya Ole Sabaya bado ni tuhuma tu hadi pale yatakapothibitishwa mahakamani kupitia ushahidi. Yaani, ukweli au la kuhusu mashtaka yake utapatikana mahakamani. Sitarajii tena Mkurugenzi wa Mashtaka kuwasilisha Hati ya Kutokuwa na Nia ya Kushtaki kama alivyofanya kwenye kesi ya Sabaya iliyopita (natania).

Kimsingi, makosa katika mashtaka yote dhidi ya Sabaya yanadaiwa kufanywa naye wakati akiwa Mkuu wa Wilaya ya Hai. Hapa ndipo tafakari yangu inapoanzia. Bila hata ufahamu wa kisheria, inafahamika kuwa Mkuu wa Wilaya pamoja na mambo mwngine ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama katika Wilaya yake. Ndiyo kusema, Mkuu wa Wilaya ndiye mlinzi kiongozi wa amani na utulivu katika Wilaya yake. Ndiye anayepaswa kuhakikisha kuwa wananchi wa Wilaya yake wanaishi kwa amani huku wakifanya shughuli zao za kimaendeleo katika kujitafutia mikate yao ya kila siku.

Haitarajiwi kuona Mkuu wa Wilaya 'akiwa kinara' wa uharibifu wa amani, utulivu na ustawi wa watu wake. Haitarajiwi pia kuona Mkuu wa Wilaya kutenda makosa ya jinai ambaye yeye mwenyewe ndiye anapambana nayo usiku na mchana ili wananchi wake wawe na amani, utulivu na ustawi. Haitarajiwi pia Mkuu wa Wilaya kutenda uhalifu ikizingatiwa pia yeye ni mwakilishi wa Rais katika Wilaya yake. Matendo yake na maneno yake yanawakilisha maono, maelekezo na taswira ya mamlaka yake ya uteuzi. HAIPENDEZI Mamlaka ya uteuzi kubeba taswira ya kijinai kwa wananchi kupitia kwa Mkuu wa Wilaya.

NI PICHA YA KUOGOFYA kuona Mkuu wa Wilaya akipokea rushwa; akitakatisha pesa; akiongoza genge la kihalifu na kadhalika. NI MAMBO YA KUTISHA kusikia au kushuhudia Mkuu wa Wilaya akikandamiza ustawi wa watu wake na kulinda kwa nguvu zake zote 'genge' lake. Tuhuma dhidi ya Sabaya zinatoa picha ya kujisahau au kujiachia kulikopitiliza kwa wateule. Au tuhuma hizo zinaonyesha jinsi tabia halisi ya mteule inapojianika pale ambapo kunapatikana nafasi ya kufanya chochote mahali popote. Mashtaka yote ni ya Arusha, bado ya mahali pengine ikiwemo Wilaya yake ya Hai. Inafikirisha sana.

Mashtaka ya Sabaya yawe funzo kwa Mamlaka ya Uteuzi. Yawe funzo katika vya kuzingatia kabla, wakati na baada ya uteuzi. Mamlaka ya uteuzi ina mikono mirefu. Ina vyombo mbalimbali vya kiuchunguzi na kiutafiti. Inafurahisha na kuleta imani na amani kwa wananchi kuona Mamlaka ya Uteuzi ikifanya kazi kubwa kuchuja wateule wake ili 'makandokando' kama ya Ole Sabaya yaepukwe. Hata kama mashtaka yote hayatathibitishwa mahakamani, kutuhumiwa tu kama kiongozi inatosha kuchafua picha ya mteule yeyote yule awaye. Kila jambo hutokea ili kutoa mafundisho kwa yajayo.

Petro umezunguka sana, Sabaya alipata nguvu ya kutenda huo uovu maana aliyemteua alikuwa muovu na dhalimu. Unyama na ukatili mwingi ulikuwa na baraka za boss wake, japo unyama mwingine alijiongeza. Katika hilo group la Sabaya, yuko pia Makonda, kila uchafu aliofanya Sabaya, Makonda pia alifanya ila vyombo vya habari vilifungwa midomo. Wakati wakifanya unyama huu, walishurutisha watanzania wote tuamini kuwa wao ni wazalendo!

Uchafu wote wa viongozi wengi kipindi cha Magu uko wazi, ila watu wanakaa kimya, kwani ni utamaduni kufumbia uchafu wa wanasiasa wa ccm nchi hii.
 
Back
Top Bottom