OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 457
- 773
Utafiti uliochapishwa katika Jarida la Advanced Research in Economics and Business Strategy umeonesha matumizi ya fedha taslim yanaathiri jamii katika mipango ya kuunda bei na kusababisha mfumuko wa bei. Utafiti huo uliofanywa na Francis Nyonzo, Mchumi ambaye pia alikuwa mshiriki wa moja ya program ya Fulbright nchini Marekani umetumia zaidi ya namna moja kuonesha madhara ya matumizi ya fedha taslimu.
Nyonzo ambaye ni mchumi aliyefanya kazi JamiiForums kabla ya kuenda Marekani, Michigan State University kwa program ya Hubert H. Humphrey Fellowship ametumia bei za Mabasi/dalala na bei za masoko ya mtandaoni kuonesha hayo. Kwa nauli za daladala ambazo hutozwa kwa kilometer, tafiti imeonesha kuwa watu hulipa wastani wa shilingi 32.17 zaidi. Kwa mabasi ya mikoani abiria wa ordinary hulipa zaidi huku wale wa luxery wakilipa kidogo.
Tafiti hii imepewa jina la Denominational inflation: Limited currency divisibility in cash payment systems - Tanzania as a case study. Denominational Inflation imetafsiriwa kama mfumuko wa bei unaotokana na watu kutaja bei kwa kutegemea fedha zilizokatika mzunguko. Tanzania ina Tsh 10,000 kama fedha yake kubwa na senti moja kama fedha ndogo. Hata hivyo zilizo katika mzunguko ni fedha kati ya Tsh 10,000 na Tsh 50. Hivyo bei inayotumia fedha taslimu ni ile inayoweza kulipika kwa mgawanyo wa 50. Mfano Tsh 2550, mfanyabiashara hawezi uza kitu kwa Tsh 2222 kwa kuwa kwenye fedha taslimu hizo units nyingine hazipo. Andiko hilo limeanza kwa kuonesha ni kweli kiuchumi serikali haiwezi kuendelea kutengeneza senti moja au shilingi 10 kwa kuwa itakuwa gharama kiuchumi. Hivyo tafiti inashauri kutumia njia ya digital kufanya malipo ambapo ni rahisi kulipa hizo smallest units hata senti inapohitajika.
Kwa kutumia masoko ya mtandaoni yanayofanya kazi zake nchini Tanzania, Kikuu mall na Dar shopping Mall, tafiti hii imeonesha masuala zaidi kwenye upangaji bei. Kikuu Mall wanatumia mfumo wa kidigitali kulipa bei, huku Dar shopping mall wakitumia fedha taslimu ambapo mteja hulipa akifikishiwa mzigo. Tafiti imebaini kuwa bei za Kikuu ziko flexible ambapo mtu hutumia hadi senti kufanya malipo, wakati kwenye soko linalotumia fedha taslimu hakuna bei iliyo na thamani chini ya 50 katika digits zake mbili za mwisho.
Matokeo Msingi:
Shiling 50/= iko mbioni kupotea kwenye mzunguko
Shilingi 100/= itakuwa ndio fedha ndogo kutumika kwenye mzinguko.
Ubaya wa bei kutokuwa flexible
Kwa sasa mfanyabishara akitaka utofauti wa bei ni lazima aweke bei ambayo tofauti yake ni zaidi ya 50. Yaani kama jirani anauza kitu kwa Tsh 1000, mwingine kwa ushindani anaweza kuweka Tsh950. Ili kukuza ushindani, mtu angeweza kuuza bidhaa kwa Tsh 999 na bado akaleta chachu kwenye ushindani wa biashara.
Tafiti hii imeshauri kuendelea kuchagiza matumizi ya malipo ya kidigitali ambayo yanaleta wepesi wa kulipa hadi senti. Hata hivyo tafiti imenukuu gharama kubwa za kufanya malipo mtandaoni na kushauri kupunguza gharama hizo ili zisizidi adjustment unit ya cash payments.
Unaweza kuisoma zaidi tafiti hii hapa View of Denominational inflation: Limited currency divisibility in cash payment systems – Tanzania as a case study
au shusha pdf kuisoma kwa uzuri