Tafiti: Vijana chini ya miaka 35 huamini zaidi Conspiracy theories

Tafiti: Vijana chini ya miaka 35 huamini zaidi Conspiracy theories

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Utafiti mpya uliofanywa kwa ushirikiano kati yangu na Daniel Stockemer kutoka Chuo Kikuu cha Ottawa, uliotolewa katika jarida la Political Psychology, umeonesha kuwa umri ni miongoni mwa vihisishi vikuu vya kuamini Conspiracy theories — lakini si kwa namna ambayo wengi wangetegemea.

Watu walio na umri wa chini ya miaka 35 ndio wanaoamini zaidi nadharia hizi.

Hitimisho hili limejengwa juu ya ushahidi mpana. Matokeo yalikuwa: umri mdogo ulionekana kuwa kiashiria kikubwa zaidi cha kuamini Conspiracy theories kuliko jinsia, kipato au kiwango cha elimu.

Kwa nini vijana wanaamini zaidi Conspiracy theories?

1. Kutengwa kisiasa
Vijana wengi wanajihisi wamesahaulika katika mifumo ya kisiasa inayoongozwa na watu wa vizazi viwili au vitatu vilivyotangulia. Kutokuwakilishwa huko huleta hisia za kuchoka na kutokuwa na sauti ndani ya demokrasia.

Katika mazingira haya, Conspiracy theories huwapa vijana maelezo rahisi na ya kuvutia: kwamba mfumo si tu unashindwa kufanya kazi, bali pia unadhibitiwa kwa siri na watu wabaya.

2. Mtindo wa uanaharakati
Vijana wengi siku hizi hawashiriki sana katika siasa kwa njia za kawaida kama kupiga kura, bali wanajihusisha na harakati zisizo za kawaida kama maandamano, kususia bidhaa au kampeni za mitandaoni.

Maeneo haya ya uanaharakati, hasa mitandaoni, huwa mahali panapofaa kwa Conspiracy theories kuota mizizi. Mara nyingi, harakati hizi hutumia simulizi zinazogawanya jamii — “sisi dhidi yao” — ambapo kundi dogo linaaminika kuwa safi dhidi ya mamlaka potofu.

3. Hali duni ya kujitambua (self-esteem)
Utafiti pia ulionyesha uhusiano mkubwa kati ya hali ya kujiona huna thamani (low self-esteem) na kuamini Conspiracy theories. Kwa mtu anayeona hana nguvu wala ushawishi juu ya maisha yake, kuamini kuwa kuna nguvu za siri zinazomzuia hufanya aweze kuelezea matatizo yake bila kujihisi mwenye hatia.

Hili ni jambo linalowaathiri sana vijana, kwani utafiti wa muda mrefu unaonyesha hali ya kujitambua huwa chini wakati wa ujana na huongezeka kadri mtu anavyozeeka.

Nini kifanyike?
Kwa kuimarisha uwakilishi wa vijana katika taasisi za kisiasa, tutawajengea imani kuwa mfumo unaweza kufanya kazi kwao. Hii itapunguza mvuto wa nadharia zinazodai mfumo ni wa kifisadi na haubadiliki.

Demokrasia shirikishi zaidi
Hatua hii haimaanishi kuzima ari ya vijana katika harakati. Kinyume chake, tunapaswa kuwawezesha kwa kuwapa maarifa ya kupambanua taarifa wanazokutana nazo, hasa katika mitandao ya kijamii na vikundi vya harakati.

Pia, kiunganishi kati ya nadharia hizi na hali ya kisaikolojia ya mtu kinapaswa kutazamwa kwa mapana.

Kwa kuwekeza kwenye afya ya akili na ustawi wa vijana, tunaweza kuwasaidia kuwa na nguvu ya ndani na uwezo wa kuchambua hali bila kutegemea maelezo rahisi ya kulaumu wengine.


Habari hii iliandikwa the Coversation: 3 reasons young people are more likely to believe conspiracy theories – and how we can help them discover the truth
 
Kwa Tanzania muasisi wa conspiracy theory alikua JPM ukisoma threads za Covid 19 humu utabaki mdomo wazi.
 
Hata hii taarifa kuhusu huo utafiti ni conspiracy theory pia,ya ku balance hali halisi na kuwatoa vijana kwenye reli.
 
Back
Top Bottom