johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
cc: FayzaFoxMtu akiwa na tabia za ajabu ajabu ( mbaya) anaitwa mswahili , makazi ya watu wenye maisha ya chini kama mwananyamara vingunguti kunaitwa uswahilini, ukiwa na tabia mbaya unaambiwa unatabia za kiswahili, dawa za kienyeji zinaitwa dawa za kiswahili.
So nini maana halisi ya kiswahili, uswahili, waswahili na waswahili ?
Hii ramani ya Wapi ? Sambia, kenia,hiyo Kilimanjaro nimeshidwa ata kuinakili ni shida
Mswahili ni mtu yeyote hasiyejali haki za binadamu
Baba jescaKama nan
Kaka No comment, Ila Mswahili atakuja na hoja ya kukosoaSitaki kusadiki kwamba ukisikia neno "mswahili au uswahili" huelewi kabisa maana yake najua kuna maana unayoipata aidha moja au zaidi.
Katika kujibu hoja yako kwanza maana halisi ya mswahili ni mzawa wa upwa ya pwani ya Afrika mashariki ambaye lugha yake ni kiswahili na ana uswahili kama utamaduni wake. Katika hilo basi "Mswahili" ni huyo mtu niliyrmuelezea hapo juu na "Uswahili" ni utamaduni wake.
Nikiongelea utamaduni naongelea taratibu zote za maisha ya jamii fulani hivyo basi maana nyingi za swahili zimetokana na tabia na vitendo mbalimbali ambavyo vimedhihirika katika jamii hii ya waswahili.
Mwisho, pamoja na hayo yote tukumbuke pia lugha ina sifa kama ya kiumbe hai ya kuzaliwa, kukua na mwisho hufa. Katika hatua ya kuzaliwa na kukua lugha huathiriwa na mtu mmojammoja, mazingira ya kijografia, kikundi cha watu fulani, biashara na uchumi hivya basi maana inaweza kubadilika kutokana na mtumiaji au watumiaji wa lugha, kazi ambayo lugha inatumika kuifanya na mahali inapotumika na hivyo basi zote hizo zinaweza kuwa maana za "Mswahili" au "Uswahili" kutokana na sababu nilizokwisha kuzieleza.
Naomba kuwasilisha hoja.
Waswahili wanajua mengi,ustaarabu ulianzia kwao,akiwa amesoma ni mwerevu hat kama amesoma ni mwerevu.Nilipata kumsikia mtu akisema hangependa aitwe "mswahili". Nikapatwa na maswali mengi kichwani kwani mtu huyu alikua mzawa, mweusi na anaishi DSM.
Kabla sijamtaka undani kwa kauli yake hii, nilidhani uswahili ni title ya mtu mwenye ngozi nyeusi na anayeishi au anayetoka kwenye jamii ya watu wa mwambao. Baada ya kuongea na huyu mtu, niligundua kuwa hata mzungu na watu wa bara wanaweza kuwa waswahili!
Kinachomfanya mtu awe mswahili kumbe ni "hulka" - kubwa mbili zikiwa (1) kuongea zaidi ya matendo na (2) kujifanya kujua kila kitu.
Kwa mtizamo huu, Tanzania tuna waswahili kibao, Tutafika kweli?
========================
========================
=============================
=========================
Waswahili watu was pwani na wrote waliokubali kupokea uislamu na mambo ya Asia na Arabu.Waswahili wamesambaa nchi nzima karibu kila kabila sasa lina waswahili.Wadau mswahili ni nani mbona wote tunaongea kiswahili ila kuna baadhi wanaitwa waswahili pamoja na kwamba wana lugha za makabila yao wengine hapana?