Sitaki kusadiki kwamba ukisikia neno "mswahili au uswahili" huelewi kabisa maana yake najua kuna maana unayoipata aidha moja au zaidi.
Katika kujibu hoja yako kwanza maana halisi ya mswahili ni mzawa wa upwa ya pwani ya Afrika mashariki ambaye lugha yake ni kiswahili na ana uswahili kama utamaduni wake. Katika hilo basi "Mswahili" ni huyo mtu niliyrmuelezea hapo juu na "Uswahili" ni utamaduni wake.
Nikiongelea utamaduni naongelea taratibu zote za maisha ya jamii fulani hivyo basi maana nyingi za swahili zimetokana na tabia na vitendo mbalimbali ambavyo vimedhihirika katika jamii hii ya waswahili.
Mwisho, pamoja na hayo yote tukumbuke pia lugha ina sifa kama ya kiumbe hai ya kuzaliwa, kukua na mwisho hufa. Katika hatua ya kuzaliwa na kukua lugha huathiriwa na mtu mmojammoja, mazingira ya kijografia, kikundi cha watu fulani, biashara na uchumi hivya basi maana inaweza kubadilika kutokana na mtumiaji au watumiaji wa lugha, kazi ambayo lugha inatumika kuifanya na mahali inapotumika na hivyo basi zote hizo zinaweza kuwa maana za "Mswahili" au "Uswahili" kutokana na sababu nilizokwisha kuzieleza.
Naomba kuwasilisha hoja.