Tafsiri halisi ya neno Mswahili

Tafsiri halisi ya neno Mswahili

Mtu akiwa na tabia za ajabu ajabu ( mbaya) anaitwa mswahili , makazi ya watu wenye maisha ya chini kama mwananyamara vingunguti kunaitwa uswahilini, ukiwa na tabia mbaya unaambiwa unatabia za kiswahili, dawa za kienyeji zinaitwa dawa za kiswahili.

So nini maana halisi ya kiswahili, uswahili, waswahili na waswahili ?
cc: FayzaFox
 
Uswahili kiswahili n.k nivitu vya hovyohovyo visivyo na mpangilio ,fujo, ujaja, penye kutaka vigu bila ya kufanya kazi. Kiufupi kitu swahili ni tus kwa mtu anayejua maana halis. Pitia kamus huru
 
kichwa cha apo juu chahusika
Mswahili-mjuzi wa kiswahili
Najua kuna watakao dhani maana ile nyingine ya mtu muongo, mhuni mhuni, au mtu wa mwambao wa pwani

Najua watu mpo mnaokijua kiswahili vizur

DOCUMENTARY - kwa kiswahili lina maana gan'


Kma kuna neno linakutatiza waweza kuliandika najua wapo watu wanaweza kua wanalijua

Pamoja sana ...
images.jpeg
 
Hii ramani ya Wapi ? Sambia, kenia,hiyo Kilimanjaro nimeshidwa ata kuinakili ni shida
 
Wadau mswahili ni nani mbona wote tunaongea kiswahili ila kuna baadhi wanaitwa waswahili pamoja na kwamba wana lugha za makabila yao wengine hapana?
 
Hata wakenya ukiwaita waswahili wanachukia vibaya Sana wenyewe huwaita watu wa pwani. Mombasa plain kushika chini Tanga mpaka unguja
 
Kwa kumbukumbu zangu za seco zinaniambia kuna maana 5 ya neno "Mswahili"
  • Mtu mjanja mjanja
  • Mtu anayeongea kiswahili
  • Mtu anayeishi maeneo ya pwani
Zingine malizieni nimesahau
 
Sitaki kusadiki kwamba ukisikia neno "mswahili au uswahili" huelewi kabisa maana yake najua kuna maana unayoipata aidha moja au zaidi.
Katika kujibu hoja yako kwanza maana halisi ya mswahili ni mzawa wa upwa ya pwani ya Afrika mashariki ambaye lugha yake ni kiswahili na ana uswahili kama utamaduni wake. Katika hilo basi "Mswahili" ni huyo mtu niliyrmuelezea hapo juu na "Uswahili" ni utamaduni wake.
Nikiongelea utamaduni naongelea taratibu zote za maisha ya jamii fulani hivyo basi maana nyingi za swahili zimetokana na tabia na vitendo mbalimbali ambavyo vimedhihirika katika jamii hii ya waswahili.
Mwisho, pamoja na hayo yote tukumbuke pia lugha ina sifa kama ya kiumbe hai ya kuzaliwa, kukua na mwisho hufa. Katika hatua ya kuzaliwa na kukua lugha huathiriwa na mtu mmojammoja, mazingira ya kijografia, kikundi cha watu fulani, biashara na uchumi hivya basi maana inaweza kubadilika kutokana na mtumiaji au watumiaji wa lugha, kazi ambayo lugha inatumika kuifanya na mahali inapotumika na hivyo basi zote hizo zinaweza kuwa maana za "Mswahili" au "Uswahili" kutokana na sababu nilizokwisha kuzieleza.
Naomba kuwasilisha hoja.
Kaka No comment, Ila Mswahili atakuja na hoja ya kukosoa
 
Nilipata kumsikia mtu akisema hangependa aitwe "mswahili". Nikapatwa na maswali mengi kichwani kwani mtu huyu alikua mzawa, mweusi na anaishi DSM.

Kabla sijamtaka undani kwa kauli yake hii, nilidhani uswahili ni title ya mtu mwenye ngozi nyeusi na anayeishi au anayetoka kwenye jamii ya watu wa mwambao. Baada ya kuongea na huyu mtu, niligundua kuwa hata mzungu na watu wa bara wanaweza kuwa waswahili!

Kinachomfanya mtu awe mswahili kumbe ni "hulka" - kubwa mbili zikiwa (1) kuongea zaidi ya matendo na (2) kujifanya kujua kila kitu.

Kwa mtizamo huu, Tanzania tuna waswahili kibao, Tutafika kweli?

========================

========================

=============================

=========================
Waswahili wanajua mengi,ustaarabu ulianzia kwao,akiwa amesoma ni mwerevu hat kama amesoma ni mwerevu.
Wanaishi mjini hivyo wanaona mengi.Wamefanikiwa kuenezabutamaduni wao bara zima la Afrika na dunia imeanza kuiga.
Huongea kiswahili fasaha.
Mademu wao wanajua kujipamba na kumtunza mme,wanaume wa kiswahili mke kwao ni pambo sio katapila la kumzalishia.Hawapigi wake zao bali hupiga kwa upande wa kanga.
Huoa wake wengi kwa sababu hawapendi uzinzi.nk nk wataendeleza waswahili wenzangu.
 
Wadau mswahili ni nani mbona wote tunaongea kiswahili ila kuna baadhi wanaitwa waswahili pamoja na kwamba wana lugha za makabila yao wengine hapana?
Waswahili watu was pwani na wrote waliokubali kupokea uislamu na mambo ya Asia na Arabu.Waswahili wamesambaa nchi nzima karibu kila kabila sasa lina waswahili.
 
Back
Top Bottom