Tafsiri halisi ya neno Mswahili

Tafsiri halisi ya neno Mswahili

1. Mkaazi wa Upwa wa Afrika Mashariki (Kutokea Sofala hadi Barawa, Somalia na visiwa vilivyo ndani yake)
2. Mtu yeyote anayezungumza lugha ya Kiswahili
3. Mkaazi wa maeneo duni yanayofahamika kama 'Uswahilini'
4. Mtu mwenye tabia za zinazoonekana za ajabu kwa watu walioamili ustaarabu wa kisasa. Unaweza kusikia "Anapenda sana umbea, ana mambo ya Kiswahili.
5. Anayeamini au kushiriki katika Ushirikina nae huitwa Mswahili.

Naamini nimejibu swali lako kwa kiasi fulani, karibu!

kweli kabisa majibu yamejitosheleza ahsante sana!
 
Habarini wadau,

Kwa kawaida neno mswahili limekuwa likitumiwa kumaanisha haya

-Mtu wa hali ya chini (kiuchumi) na anayeishi uswahilini

-Pia mara nyingine humaanisha mtu ambaye ana sound nyingi au muongomuongo,utaskia "Acha uswahili wewe"

-Pia watu wengi wa mikoani (especcially wakristo) wanawachukulia waswahili ni waislam wa pwani,Dsm na hata zanzibar

-Lakini pia watoto wa mjini wanawachukulia mswahili ni mjanja mfano utaskia "Mimi ndio mtoto wa kiswahili/kiswazi huwezi niingiza kingi"

SWALI: Mswahili haswa ni nani? Au ni yeyote anayezungumza kiswahili? Kuna kabila la Waswahili?
 
Uswahili ni tabia zaidi. Tabia za udanganyifu, kutojali ahadi, kuongea bila mantiki, kujadili yasiyowahusu, n.k. Mwenye tabia hizo ndio Mswahili.
 
Duuh,kumbe ndio maana wabongo wengine hawataki kuitwa waswahili hata mbele ya wageni...
 
Mtu muongo muongo asiyefata utaratibu,mlala nje,mwizi,asiyejari muda nk nk.!
 
Habarini wadau

Kwa kawaida neno mswahili limekuwa likitumiwa kumaanisha haya

-mtu wa hali ya chini (kiuchumi) na anayeishi uswahilini

-Pia mara nyingine humaanisha mtu ambaye ana sound nyingi au muongomuongo,utaskia "Acha uswahili wewe"

-Pia watu wengi wa mikoani (especcially wakristo) wanawachukulia waswahili ni waislam wa pwani,Dsm na hata zanzibar

-Lakini pia watoto wa mjini wanawachukulia mswahili ni mjanja mfano utaskia "Mimi ndio mtoto wa kiswahili/kiswazi huwezi niingiza kingi"

SWALI: Mswahili haswa ni nani? Au ni yeyote anayezungumza kiswahili? Kuna kabila la Waswahili?

Mswahili ni mtu mswahili
 
Mkuu hii dada yetu FaizaFoxy atapingana sana nawewe
Well, sidhani. Mswahili pia inaweza kuwa na maana tofauti kutokana na context. Uswahili pia navyoelewa ni utamaduni, nikiwa nje ya bongo i am Swahili, kwa sababu nazungumza kiswahili na mambo mengine.

Context tunayoijadili hapa ndio kama nilivyoelezea hapo awali.
 
Last edited by a moderator:
Watu wenye dharau ndio wanapenda sana kutumia hili neno kuwaita wenzao!siku hizi hata ukiwa maskini watu wenye nazo watakuita mswahili!!.
 
Mswahili ni mwenyeji Wa pwani ya Africa mashariki wengine mmedandia tu
 
Anakotokea mamaangu, waislamu ndio huitwa waswahili,(Haijalishi kabila wala kabila lake)
kwao baba Mswahili ni mtu asiye wa asili ya kule kwao (Huko haijalishi dini)

Kwa mimi mswahili ni anayeishi tamaduni za kiswahili kuanzia asili yake, lugha, mavazi vyakula na tamaduni zingine. (uswahili/sahel =Pwani)
 
sasa mtihani umeshaujibu sisi unatuuliza nini?
 
Habarini wadau,

Kwa kawaida neno mswahili limekuwa likitumiwa kumaanisha haya

-Mtu wa hali ya chini (kiuchumi) na anayeishi uswahilini

-Pia mara nyingine humaanisha mtu ambaye ana sound nyingi au muongomuongo,utaskia "Acha uswahili wewe"

-Pia watu wengi wa mikoani (especcially wakristo) wanawachukulia waswahili ni waislam wa pwani,Dsm na hata zanzibar

-Lakini pia watoto wa mjini wanawachukulia mswahili ni mjanja mfano utaskia "Mimi ndio mtoto wa kiswahili/kiswazi huwezi niingiza kingi"

SWALI: Mswahili haswa ni nani? Au ni yeyote anayezungumza kiswahili? Kuna kabila la Waswahili?

Mswahili kilugha ni mwenyeji wa Pwani ya Afrika Mashariki hususani Zanzibar,Quilo (Kilwa ya sasa) na sehemu za bara ambazo zilipata kuhusiana na watu toka bara Arabu kibiashara.

Kisheria Mswahili ni mwenyeji wa Afrika Mashariki ambaye ni mzungumzaji wa Kiswahili ila kuna maana nyingin nyingi lakini kilugha hayo ni misimu na hayaondoi maana halisi la neno Mswahili.
 
Hivi mkuu Zanzibar huwa hawana lugha za makabila kama bara? Wao ni kiswahili tu? Nisaidie pls
 
Back
Top Bottom