Thiago Silva
JF-Expert Member
- Nov 1, 2014
- 322
- 177
1. Mkaazi wa Upwa wa Afrika Mashariki (Kutokea Sofala hadi Barawa, Somalia na visiwa vilivyo ndani yake)
2. Mtu yeyote anayezungumza lugha ya Kiswahili
3. Mkaazi wa maeneo duni yanayofahamika kama 'Uswahilini'
4. Mtu mwenye tabia za zinazoonekana za ajabu kwa watu walioamili ustaarabu wa kisasa. Unaweza kusikia "Anapenda sana umbea, ana mambo ya Kiswahili.
5. Anayeamini au kushiriki katika Ushirikina nae huitwa Mswahili.
Naamini nimejibu swali lako kwa kiasi fulani, karibu!
Uswahili ni tabia zaidi. Tabia za udanganyifu, kutojali ahadi, kuongea bila mantiki, kujadili yasiyowahusu, n.k. Mwenye tabia hizo ndio Mswahili.
Duuh,kumbe ndio maana wabongo wengine hawataki kuitwa waswahili hata mbele ya wageni...
Habarini wadau
Kwa kawaida neno mswahili limekuwa likitumiwa kumaanisha haya
-mtu wa hali ya chini (kiuchumi) na anayeishi uswahilini
-Pia mara nyingine humaanisha mtu ambaye ana sound nyingi au muongomuongo,utaskia "Acha uswahili wewe"
-Pia watu wengi wa mikoani (especcially wakristo) wanawachukulia waswahili ni waislam wa pwani,Dsm na hata zanzibar
-Lakini pia watoto wa mjini wanawachukulia mswahili ni mjanja mfano utaskia "Mimi ndio mtoto wa kiswahili/kiswazi huwezi niingiza kingi"
SWALI: Mswahili haswa ni nani? Au ni yeyote anayezungumza kiswahili? Kuna kabila la Waswahili?
Well, sidhani. Mswahili pia inaweza kuwa na maana tofauti kutokana na context. Uswahili pia navyoelewa ni utamaduni, nikiwa nje ya bongo i am Swahili, kwa sababu nazungumza kiswahili na mambo mengine.Mkuu hii dada yetu FaizaFoxy atapingana sana nawewe
SWALI: Mswahili haswa ni nani? Au ni yeyote anayezungumza kiswahili? Kuna kabila la Waswahili?
Yeah, hakuna kejeli kama kuitwa Mswahili, kifupi ni kumaanisha hujastaarabika kabisa.
Habarini wadau,
Kwa kawaida neno mswahili limekuwa likitumiwa kumaanisha haya
-Mtu wa hali ya chini (kiuchumi) na anayeishi uswahilini
-Pia mara nyingine humaanisha mtu ambaye ana sound nyingi au muongomuongo,utaskia "Acha uswahili wewe"
-Pia watu wengi wa mikoani (especcially wakristo) wanawachukulia waswahili ni waislam wa pwani,Dsm na hata zanzibar
-Lakini pia watoto wa mjini wanawachukulia mswahili ni mjanja mfano utaskia "Mimi ndio mtoto wa kiswahili/kiswazi huwezi niingiza kingi"
SWALI: Mswahili haswa ni nani? Au ni yeyote anayezungumza kiswahili? Kuna kabila la Waswahili?
Mswahili kilugha ni mwenyeji wa Pwani ya Afrika Mashariki hususani Zanzibar,Quilo (Kilwa ya sasa) na sehemu za bara ambazo zilipata kuhusiana na watu toka bara Arabu kibiashara.
Kisheria Mswahili ni mwenyeji wa Afrika Mashariki ambaye ni mzungumzaji wa Kiswahili ila kuna maana nyingin nyingi lakini kilugha hayo ni misimu na hayaondoi maana halisi la neno Mswahili.