Tafsiri halisi ya neno Mswahili

Tafsiri halisi ya neno Mswahili

Mtu akiwa na tabia za ajabu ajabu ( mbaya) anaitwa mswahili , makazi ya watu wenye maisha ya chini kama mwananyamara vingunguti kunaitwa uswahilini, ukiwa na tabia mbaya unaambiwa unatabia za kiswahili, dawa za kienyeji zinaitwa dawa za kiswahili.

So nini maana halisi ya kiswahili, uswahili, waswahili na waswahili ?
 
MSWAHILI NI MTU ANAEOGOPA KUWAJIBIKA BAADA YA KUFANYA MADUDU ETI KWA KIGEZO CHA NJAA
 
Mtu akiwa na tabia za ajabu ajabu ( mbaya) anaitwa mswahili , makazi ya watu wenye maisha ya chini kama mwananyamara vingunguti kunaitwa uswahilini, ukiwa na tabia mbaya unaambiwa unatabia za kiswahili, dawa za kienyeji zinaitwa dawa za kiswahili.
So nini maana halisi ya kiswahili, uswahili, waswahili na waswahili ?
Mimi nikimuona mtu na kadi ya ccm huwa namuona mswahili sana
 
Ni Wa- Afrca wote kwa ujumla wao, na mazingira yao. na vitu yao. lakini wale watu wasomi wa juu hasa hasa waliosomeana kuishi western countries wana tabia za kizungu zungu hivi. kitajiritajiri, kipesa pesa, wanaongea kizungu fluently, bila kuchomekea maneno ya kiswahili kama Tatanyarusare ruya Mtibita. hawanuki vikwapa wala majasho, hata asipo pafyume. wana harufu kama sukari iliyokaangwa kwa mbaaali hivi. siyo malimbukeni.

Wa africa wanaoishi maeneo machafu machafu, na mitaro ya maji kunuka, hakuna maji bomba bali wanakunywa maji ya visima km vijijjini vya chumvi, nyumba hazipo kwenye mpangilio mzuri halafu zimebanana, muda wowote zinabomolewa.

wanakula sana vitumbua na chai za rangi asubuhi .sometimes kiporo cha ubwabwa wa nazi. kama Kipawa ya zamani- kushoto. Tabata kwa chura, Mombasa, kwa mtogole, Temeke wailes nk, vitoto viiingi na miziki mingi inafanya kuwe na kelele km quater za polisi vijana.
wenyeji wengi wana kaa mbele ya vibaraza kila wakati. wakiona mtu msafii anapita karibu yao, basi mmoja wao anajifanya kuimba mchiriku, hapo ujue wamekutamani, ukiwapa mgongo tu, wananyamaza hapo ujue sasa wanateta. utasikia ''hawa wageni hapa!'' au hawa watoto ni wa Tatanyakibombo, wameshuka na pipa kuja kula krismas! AAAHAAAA!

HUO NDIYO USWAHILI MKUU UPO?
 
Mtu akiwa na tabia za ajabu ajabu ( mbaya) anaitwa mswahili , makazi ya watu wenye maisha ya chini kama mwananyamara vingunguti kunaitwa uswahilini, ukiwa na tabia mbaya unaambiwa unatabia za kiswahili, dawa za kienyeji zinaitwa dawa za kiswahili.

So nini maana halisi ya kiswahili, uswahili, waswahili na waswahili ?
ongezea hapo waislam huitwa waswahili na wakristo
 
Mtu akiwa na tabia za ajabu ajabu ( mbaya) anaitwa mswahili , makazi ya watu wenye maisha ya chini kama mwananyamara vingunguti kunaitwa uswahilini, ukiwa na tabia mbaya unaambiwa unatabia za kiswahili, dawa za kienyeji zinaitwa dawa za kiswahili.

So nini maana halisi ya kiswahili, uswahili, waswahili na waswahili ?
Ukisikia mtu anamwambia mwenzake wa uswahilini ujue yeye anajiona Mzungu. Ila akifika uzunguni anatengwa anaambiwa yeye MTU mweusi hana nafasi uzunguni.
 
Waafrika wenye asili ya kibantu.. Ndio haswa wenye asili ya uswahili...
 
Mtu akiwa na tabia za ajabu ajabu ( mbaya) anaitwa mswahili , makazi ya watu wenye maisha ya chini kama mwananyamara vingunguti kunaitwa uswahilini, ukiwa na tabia mbaya unaambiwa unatabia za kiswahili, dawa za kienyeji zinaitwa dawa za kiswahili.

So nini maana halisi ya kiswahili, uswahili, waswahili na waswahili ?
Sitaki kusadiki kwamba ukisikia neno "mswahili au uswahili" huelewi kabisa maana yake najua kuna maana unayoipata aidha moja au zaidi.
Katika kujibu hoja yako kwanza maana halisi ya mswahili ni mzawa wa upwa ya pwani ya Afrika mashariki ambaye lugha yake ni kiswahili na ana uswahili kama utamaduni wake. Katika hilo basi "Mswahili" ni huyo mtu niliyrmuelezea hapo juu na "Uswahili" ni utamaduni wake.
Nikiongelea utamaduni naongelea taratibu zote za maisha ya jamii fulani hivyo basi maana nyingi za swahili zimetokana na tabia na vitendo mbalimbali ambavyo vimedhihirika katika jamii hii ya waswahili.
Mwisho, pamoja na hayo yote tukumbuke pia lugha ina sifa kama ya kiumbe hai ya kuzaliwa, kukua na mwisho hufa. Katika hatua ya kuzaliwa na kukua lugha huathiriwa na mtu mmojammoja, mazingira ya kijografia, kikundi cha watu fulani, biashara na uchumi hivya basi maana inaweza kubadilika kutokana na mtumiaji au watumiaji wa lugha, kazi ambayo lugha inatumika kuifanya na mahali inapotumika na hivyo basi zote hizo zinaweza kuwa maana za "Mswahili" au "Uswahili" kutokana na sababu nilizokwisha kuzieleza.
Naomba kuwasilisha hoja.
 
Back
Top Bottom